Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara

Mi nafikiri amejali zaidi maslahi ya taifa kusimamia sheria. Kwanza ni fedha kidogo kubomoa jengo hilo na kujenga lingine ukilinganisha na kupitisha barabara sehemu nyingine ambayo sio tu haikupangwa, bali pia kuna majengo mengine yatakayo bomolewa. Pili, kwa kuchelewa kupanua bara bara kwaajili ya kupanga sehemu nyingine ya kuipitisha, mabilioni ya fedha za wananchi yatazidi kupotea kwenye foleni kupitia mafuta na kazi zao kuchelewa. Tatu, kuendeleza tabia ya sheria kupinda kila ikifika kwenye fedha nyingi mazara yake ni makubwa kiasi kwamba hakuna thamani yake ki-fedha kwani hata usalama wa taifa unakua mashakani. Nne, kazi ya magufuli kama waziri wa ujenzi ni kuhakikisha barabara zinajengwa kwa mujibu wa sheria (bila kuvunja sheria) wala sio vinginevyo. Sasa anaesema magufuli ni ana wazimu nafikiri ni mvivu wa kufikiria!
 
Ama umekwepa kujibu swali langu au ni swali gumu kidogo kwako

mkuu no way jengo la tanesco kuvunjwa ni ufisadi sio suala la kusema wamevunja sheria au la. as far as road reserve is there for public use and tanesco building is there for public use inabidi tufumbie macho ukizingatia hakuna athari kwa barabara yetu ya morogoro
 
haiwezekani kuchezea shilingi chooni kwa kuvunja jengo kama la tanesco linalo cost mabilioni ya shilingi, ni bora tuwalipe dowans kuliko kuvunja jengo lile
 
Hizi flyover mnazotaka kujenga dar jiulize zitajengwaje makutano ya Morogoro Road na Mandela road kama gorofa hilo halibomolewi. Waziri kaona mbali zaidi kuliko wachangiaji wengi wanavyochangia hapa. Kumbuka flyover zinahitaji eneo kubwa sana ili kupisha ramps za entrance and exit, vinginevyo tutacheza usanii wa kisiasa tu bila kufuata hoja za kiteknologia
Big up Maguvuli, go ahead.
Tanescobuild.jpg


cross-3.jpg

images
 
Inashangaza sana kumwita binadamu mwendawazimu bila sababu ya msingi. Magufuri ana focus mahitaji ya Watz miaka ijayo ambapo hicho kijengo ni peanut ukilinganisha na hayo mahitaji. Sheria ni Msumeno, kama imebomolewa nyumba ya bibi yangu kisa iko kwenye Rd reserve ni sawa na kubolewa hiyo.
 
Hizi flyover mnazotaka kujenga dar jiulize zitajengwaje makutano ya Morogoro Road na Mandela road kama gorofa hilo halibomolewi. Waziri kaona mbali zaidi kuliko wachangiaji wengi wanavyochangia hapa. Kumbuka flyover zinahitaji eneo kubwa sana ili kupisha ramps za entrance and exit, vinginevyo tutacheza usanii wa kisiasa tu bila kufuata hoja za kiteknologia
Big up Maguvuli, go ahead.

cross-3.jpg

images

Wanaotakiwa kulaumiwa ni wale walioruhusu ujenzi wa jengo hilo na ni serikali yenyewe bila kufuata taratibu za hifadhi ya barabara. Miundombinu ya sasa tunaona haikidhi je kwa kizazi kijacho tuonekane na sisi tungali wajinga hivyo?
Hapana Mheshimiwa Magufuli go ahead.
 
Sioni kwa nini jengo la TANESCO ubungo livunjwe!
Tutakuwa tunajirudisha nyuma badala ya kusonga mbele.

Katika maisha huwa kuna makosa yanafanyika. na kosa ikifanyika huwezi kuliondoa hata kama wewe ni rais ila unaweza kukataa lisifanyike tena. Huwezi kwenda hospitali ukatumia hela ya kula kuondoa makovu ya majeraha ya zamani. Afadhali hiyo hela uile ushibe ukafanye kazi.

Badala ya kupoteza nguvu nyingi zilizotumika kujenga majengo ya serikali na ya watu binafsi, ni vema serikali ikabuni mji mwingine kuliko kuendelea kupoteza mali na muda wa watu.

Ushauri wangu. Jiji jipya la Dar es salaam litengewe eneo ambalo halijajengwa, nje kabisa ya mji uliopo sasa. Huu wa sasa uitwe Dar Kongwe, na mji mpya wa kitaalamu wenye magorofa na mafly-over anayofikiria Mheshimiwa Magufuli.

Huu mkongwe uachwe hivyo hiyo na barabara zake finyu uwe historia ya tulikotoka.
Watoto na wajukuu zetu watafurahi huona nyumba za zamani na mitaa ya zamani. Tusiharibu historia jamani, mbona Tanzania bado ina eneo kubwa tuu. Si vibaya shirika kama TANESCO wakaweka historia, kuwa makao makuu yake yalikuwa mtaa fulani, baadaye yakahamishiwa Mji mkongwe eneo la ubungo, na sasa (wakati huo) tuko Dar Mpya (New Dar).

Tutakaposema tumeendelea tuwe na reference. Tusijilinganishe na ulaya tu, ila na miji yetu ya zamani. Historia ni muhimu Magufuli. Acheni kuvunja nyumba za watu. Bora mkawaadhibu kwa kutaifisha hizo nyumba zao kuliko kuzivunya.

Tengeni maeneo mapya yasiyo na watu mjenge miji mipya. mpeleke huduma huko.

Matatizo ya sasa yanaweza kumalizwa bila kupanua barabara.
1. Weka mabasi makubwa, safi ya kusafirisha abiria. Hakuna mtu ataendesha gari binafsi bila sababu kama kuna usafiri wa maana wa raia.
2. Zuia magari yasiyo ya abiria wakati wa asubuhi na jioni.
3. Jenga fly-over kwenye barabara za makutano zenye upana unaolingana na huu wa sasa. Hamna haja ya kuongeza upana mwingine. Utakuwa unajiongezea kazi bure.
4. Ubungo isiwe kituo kikuu cha mabasi yaendayo nje ya Dar na daladala. Yaani ubungo isiwe mwisho wa route za daladala. Miisho ya route ziwe nje ya mji. Katikati ni kusimama na kuchukua au kuacha abiria. Baada ya dakika tano, basi lisiruhusiwe kuendelea kusimama.

Wakati tukiwa tunafanya haya, Jiji jipya lipimwe kwa hizo hela za kuwalipa watu fidia na kuvunja majengo ya watu.
 
Muuliza hii hoja ungeuliza swali ungejibiwa vizuri sana na kupata elimu ya bure, kwa kifupi

1. Thamani ya barabara itakayopita pale hata iwe ni lane moja thamani yake ni kubwa dynamically mara nyingi sana zaidi ya any standing structures!

2. Ukifocus miaka 50 au 100 ijayo we need six lanes or 8 lanes highways....

Ningekueleza in details whay that building is chaos! siyo Magufuli ni wataalamu, tatizo kubwa ni kuwa masterplan za mji zinachakachuliwa kila siku na siasa inatawala na wanasiasa hao ni kama nyie!

mwanafunzi wa certificate NIT au diploma ya civil engineering DIT, MIST au Arsuha tech wanajua vyema kabisa , achilia mbali watu wa degree ya kwanza mlimani au URP ardhi institut

This is common practise even in developed world especially USA where they have even specialised contractors for demolition!

Try to search in your google you will be amazed

Guys learn to look things in different direction hii ni aibu kubwa !! STOP!

Mkuu, asante kwa hilo somo na nimekuwekea sanksi. Lakini usitegemee Mwiba aweze kukuelewa kabisaaaaaaa
 
Ingependeza zaidi kama mji ungeendelzwa kwa kuzingatia taswila iliyopo kuliko bomoabomoa zisizokwisha kama vile nchi ndio kwanza inaanza wakati ilikuwepo na maamuzi yalishakufanywa.

Inawezekana viongozi wetu wanataka kuiona Dar kama new york 5years to come, wakijifunza kutoka Mumbai (Mumbai) mji ambao kwa kiasi fulani uliendelezwa bila bomoabomoa na kubalance maisha ya sasa ya wananchi na wahindi wamejenga Metropolitan City Delhi. Tusikomae sana na Dar wakati investment kubwa imefanyika na ni bora kujenga metropolitan city Tabora au else where.

Nakubaliana kabisa na mtoa hoja kwamba si sawa kubomoa majengo ambayo hata payback bado. Wanasiasa wakiwa kazini ni noma wanaweza fanya lolote kupata uhakika wa kuongoza hata kama vita.
 
Hawa ndo watanzania! Kusovolve tatizo la trafic wanataka, na kuvunja sheria na kujenga kiholela wanataka! Sheria lazima ifuatwe hakuna cha gharama, ndo watajifunza. VUNJA!
 
Wanaotakiwa kulaumiwa ni wale walioruhusu ujenzi wa jengo hilo na ni serikali yenyewe bila kufuata taratibu za hifadhi ya barabara. Miundombinu ya sasa tunaona haikidhi je kwa kizazi kijacho tuonekane na sisi tungali wajinga hivyo?
Hapana Mheshimiwa Magufuli go ahead.

Nani alikuambia fly-over zinachukua eneo kubwa?
Acheni huo ushabiki. Wataalamu wana-design kitu kwa kufuata matakwa ya mteja. Msitumie hoja za kitaalamu kutufilisi. Acheni kutumia hela zetu vibaya. Kama mnataka fly-over eneo la sasa la barabara linatosha. Si lazima kituo cha mabasi kiwe ubungo.
 
Nani alikuambia fly-over zinachukua eneo kubwa?
Acheni huo ushabiki. Wataalamu wana-design kitu kwa kufuata matakwa ya mteja. Msitumie hoja za kitaalamu kutufilisi. Acheni kutumia hela zetu vibaya. Kama mnataka fly-over eneo la sasa la barabara linatosha. Si lazima kituo cha mabasi kiwe ubungo.

Mkuu unawaza leo na jana tu? huwazi miaka 50 ijayo? hata kama ujeenzi wa flyover hauhitajiki je zile lanes tatu zitatosha at that particular junction?? kuna comment muwe mnaona aibu jamani, tifauti gani ya nyie na hawa waliotufikisha hapa? we are taliking professionally here not politically! umeelezwa pia faida ya barabara ni kubwa kuliko thamani ya lile jengo pale! au hili nalo hutaki unataka lecture? usipoelewa hapa sema kwa adabu ili ufundishwe!

By the way flyover zinahitaji space!! dont talk like ngwini! au unataka kusema zile flyover za india??

ebu zinonyeshe hizo zisizohitaji space, uliwekewa mpaka picha !
 
Magufuli, ukikosa pesa ya kubomoa Hilo jengo la Tanesco sema tukuchangie. Tunahitaji kuondoa kero ya usafiri na foleni kwa mamilioni ya watz kwa siku na kwa miaka mingi ijayo badala ya watu asiozidi 200 kukaa kwenye kiyoyozi kutwa moja.
 
ilo jengo lenyewe bayaa ata likivunjwa hakuna atakaye limiss, kuna mawili either livunjwe kupisha upanuzi wa barabara au tanesco walipie gharama za ziada zitakazotumika kuifanyia barabara marekebisho around the building.
 
Nyie mbona mnadiscuss ujinga? mnalijua lile gorofa la masaki lililobomolewa kwa kuwa kule hakukutakiwa kuwepo jengo lefu kama lile? mnajua gharama za jengo lile? Nyie ni wafuasi wa serikali ambayo inawaonea wananchi na nyie mmekubali. Sheria haijalishi serikali au mtu binafsi. Unaponibomolea kijumba changu kidogo ni sawa na yule unayembomolea gorofa. Mmeshafanya projection in twenty five years mahitaji ya ile bara bara yatakuwaje?
Magufuli yuko sawa myie ndio mmepotoka

Kwani kubomolewa lile ghorofa ni jambo la kujisifia?
Kwa vile fulani alikosea, basi na wewe ukosee?
Sheria tunazitunga wenyewe na wenyewe twaweza kuziondoa.
Kubomoa nyumba za watu si haki. Ni serikali hii hii ya CCM ndio iliruhusu makosa hayo yatendeke.

Wawajibishwa kwanza walioruhusu ujenzi holela kama mnaweza. wengine wao ndio wakubwa serikalini lakini kwa namna moja au nyingine walichangia makosa haya.

Badala ya kubomoa nyumba za watu na majengo ya umma, kajengeni kule ambako hakuna makazi ya watu.
Bora mjenge reli za kuingia mjini kuliko kupanua barabara.
 
Tusidanganyane kujenga mji mpya wa dar na uliopo ubaki mji mkongwe. Dar ni jiji kubwa sana na ni source ya uchumi wa Taifa. Mbona tumewajengea maeneo wamachinga lakini kesho yake wanarudi kariakoo na sokoine?
Kumbuka mji mkuu wa Dodoma umetushinda, je imekaa sawa ya kujenga upya jiji la dar lenye umri zaidi ya karne tatu? Naona hapa ni nadharia tu.
Bora bomoa bomoa hata miundombinu ya jiji inaweza eleweka kuliko ilivyo sasa. Hata majiji makuu makuu nimeshuhudia Mashion zinabomomlewa kupisha mambo ya kisasa utanielezaje kuhusu hili la Tanesco?
Karibuni nitawaletea pic ya bomoabomoa jiji fulani kuupisha ujenza wa kisasa.
 
Sheria tunazitunga wenyewe
na hizi sheria tulizitunga tukijua kuna mazezeta kama tanesko hukwamisha maendeleo.mpaka hapo zitakapobadilishwa,magufuli ana haki ya kutekeleza majukumu yake bila kuangalia nani kavunja sheria.
MAGUFULI haya majengo yasipovunjwa nitahakikisha nyavu za makokoro ulizochoma kule mlingotini unazilipa!!
IKIWEZEKANA HILI JENGO LIVUNJWE HATA KESHO.aaaagh!@¥*
 
Strategically, kama majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe.

Kabla ya kumwona Magufuli hana akili ni lazima wote mnaopinga uamuzi wa Magufuli kujiuliza maswali.

Hivi ni nani aliyeamuru ujenzi wa majengo haya ya mabilioni bila kukaa chini na kupanga kila kitu kikamilifu??
Master plan ionyeshayo eneo la Barabara ilichorwa mwaka gani?
Kama Master plan ilikuwepo kabla ya ujenzi wa barabara ni kwa nini Tanesco iliendelea na ujenzi katika eneo la barbara? Ni kwa nini serikali haikuizuia Tanesci kujenga akatika eneo la barbara?

Eneo la Ubungo ni Entrence na Exit kuu ya jiji la Dar, kama kwa namna yeyote ile majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe kupisha upanuzi wowote wa barabara uiliopangwa hapo awali. Comparatively thamani ya majengo hayo ni ndogo sana ukilinganisha na hasara itakayosababishwa ya kuzuia upanuzi wa barabara.


Kama kwa akili zenu mnamuona Magufuli ni Punguani kwa kushikiria msimamo wake wa kubomoa majengo yote yaliyomo katika eneo la barabara! Mnamuonaje na mtamwita jina gani mtu aliyeng'ang'ania kujenga majengo ya thamani kubwa katika eneo la barabara?

Kulikuwa na Busara gani kujenga majengo hayo ndani yana eneo la barabara??

Ni nani aliyekuwa Waziri wa wizara husika wakati wa ujenzi huo?? Na ninani aliyekuwa Bosi wa Tanesco wakati huo??

Serikali ya CCM ilikuwa wapi na mastar plan yake wakati Tanesco wakijenga katika eneo la barabara??

Kipimo na Ujinga,Upunguani Uhuni na Utovu wa Nidhanmu Tanzania ni nini??

Magufuli ni Punguani, aliyesimama kidete kujenga katika eneo la barabara tutamwitaje??
mzee nakuunga mkono, unajua hii inchi ii iendelee sasa inabidi wapatikane "punguani" wengine kama Magufuli kama watano tu..ni bora tuanze upya kuliko kuendelea na maupumbavu yanayofanyika saiz..kwani wakati hayo majengo yanajengwa walikuwa hawajui kama ni barabara...BOMOA TUUUU...p.%^$**fu!! ndio tutie akili kwamba vitu huwa vinakwenda kwa mipango, na nnahakika wakibomoa leo kesho ndio watakuwa makini zaidi katika haya mambo la sivyo ujinga huu utaendelea kila silku kujifanya wanaweka majengo ya serikali maeneo yasioruhusiwa wakati wakipeana viwanja wenyewe kwenye maeneo yanayoruhusiwa..huu si ujinga...!!?? VUNJAAAA.. kesho ndo watatia akili kwamba mmh tukijenga hapa tena watavunja kama walivyovunja tanesco!! nchi yenyewe ishaoza hii..
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom