John Magufuli, kutaka kuwe na Wizara ya Miundombinu ni matumizi mabaya ya rasimali fedha

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Wanabodi,

Leo moja ya habari nyeti ni juu ya ombi au pendekezo la Waziri John Magufuli kutaka kuwe na Wizara ya Miundombinu kwa jiji hili la Dar es Salaam.

Dr. Magufuli kwa mtazamo wake anahisi wizara hiyo ikiundwa basi msongamano wa Magari au 'traffic jam' itatoweka hapa mjini,
kwangu naziona hizi kama ni fiksi kwakweli,Magufuli jam haitaondoka kwa kuunda wizara mpya, hvi huoni kuwa utatupa mzigo wa kulipia kodi hiyo wizara?

Tafuta mbinu nyingine ya kuondoa foleni,siyo hii
 
Hii kali, kutakuwa na wizara na waziri wake atasimamia na kuratibu shughuli jijini Dar es Salaam

London,New York,Tokyo na Johanesberg zitaitaji serikali zenye rais mwenye mamlaka kamili
 
Me nikajiuliza
je kuna wazir wa miund0mbinu London au Nairobi au Lagos?
Ina maana tuendako kutakuwa na wizara ya afya Dar maana hocpitali zimeelemewa,wizara ya ulinzi wa raia,maana kuna uhalifu,wizara ya ombaomba,
Hii kali, kutakuwa na wizara na waziri wake atasimamia na kuratibu shughuli jijini Dar es Salaam

London,New York,Tokyo na Johanesberg zitaitaji serikali zenye rais mwenye mamlaka kamili
 
Hii ni sawa na kusema ule mpango wa kujenga barabara za juu kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi na kupunguza foleni ambao ulitakiwa uanze kufanya kazi mwanzoni mwa mwaka 2012 umefeli!!

Ikiwa kila kitu mnashindwa, kuna sababu gani ya kubaki huko madarakani na kuendelea kula kodi zetu kupita mishahara minono na posho?
 
Na sisi mwanza tutahitaji waziri wa miundo mbinu,MAGUFULI UMEBUG STEP,JIPANGE UPYA
 
arudishe nyumba ya umma aliyojigawia na kujenga lami iliyoishia sebuleni kwake...fly-overs zimemshinda akili hilo.
 
Jamani DSM ni uso wa TZ na inahitaji uwekezaji mkubwa kama ambao China iliwahi fanya kwenye miji yake mikubwa ya Beijing & Shanghai kwenye miaka ya 90 (kulikuwa na wizara maalum na ilikuwa inatumia 10% ya pato la taifa kwenye miji hii). Tukumbuke pia kwamba hata sisi huko nyuma tulishawahi kuwa na wizara ya CDA, ambayo ndiyo imeifikisha Dodoma hapo ilipo (vinginevyo bado ingekuwa kama Manyoni au Singida). Kwa hiyo nadhani Magufuli ana hoja nzuri tu/tuiunge mkono.
 
Me nikajiuliza
je kuna wazir wa miund0mbinu London au Nairobi au Lagos?
Ina maana tuendako kutakuwa na wizara ya afya Dar maana hocpitali zimeelemewa,wizara ya ulinzi wa raia,maana kuna uhalifu,wizara ya ombaomba,

Msikurupuke, Uione Wizara ya Miundo Mbinu ya Jiji la Nairobi, Ministry of Nairobi Metropolian Development, Nairobi Metro, mawaziri wake hawa Ministry of Nairobi Metropolitan Development.

Jiji la Dar es Salaam linahitaji mpango mahsusi kabisa wa kukabiliana na upungufu wa miundombinu ukilinganisha na mahitaji yake, Wizara ya Ujenzi na ile ya Uchukuzi kama zilivyo sasa zina mambo mengi sana ya kufanya nchi nzima hivyo haitaweza kuconcetrate katika kutatua tatizo la eneo moja tu, Dar es Salaam, ambalo ni tatizo la kimsingi na linaathiri shughuli nyingi za kiuchumi ambazo indirect zinaathiri nchi nzima kiuchumi.

Kwa kutambua kuwa Dar es Salaam ina matatizo maalumu, yanayohitaji solution maalumu ambazo hazitaweza kupatikana kwa mfumo uliopo sasa, one more time Magufuli anadhibitisha kuwa ni kiongozi makini, mwenye vision na asiyependa blah blah, namuunga mkono sana Dr.Magufuli kwa kuliona hilo..
 
yeye angesema taasisi za serikali hazina ushirikiano au master plan ya Pamoja ktk miundombinu barabara,umeme,maji safi na taka,ardhi
 
Jamani Watanzania Tuache Ushabiki wa Kisiasa...na tusiongee vitu bila logic,kufikiria au kutofanya utafiti

Wenzetu Kenya...,wana wizara maalumu ya jiji la Nairobi ambako wameweza kushughulikia mambo mbalimbali na kutatua kero zinalozisakama jiji la Nairobi kama barabara,maji,usalama na vilevile wameweza kuwa na mipango mirefu na endelevu ya jiji la nairobi

Mfano mzuri pia Tanzania tuna kanda maalumu ya ulinzi wa jiji la Dar es salaam,tuna pia ulinzi maalumu katika wilaya ya tarime ambapo kuna matukio mengi

Jamani Dk.John Magufuli sio mjinga eti kaamka leo asubuhi ndio kasema...,hilo suala kalifanyia utafiti,kaona mazuri yake na tathmini zake..kama mnavyomjua yeye ni mtu wa kufuata utaratibu wenye kuelewa wanamwelewa ila wenye ulemavu wa fikra mnaleta siasa..huyu ndio raisi tunayemtaka msimamo kama paul kagame siyo kwenda kuhonga makanisani na kutumia vijana kumsafisha kwenye JF..

Moto wa Dk.John Magufuli Lowasa hatii mguu...,bila yeye leo CCM wangelikosa jimbo la Igunga..,bila yeye leo Uvuvi haramu bado ungekuwa tatizo kanda la Ziwa,Tukumbuke 2005 alifanya nini kwenye sekta ya barabara...Watanzania jamani tusimkosee heshima huyu jamaa

Hana tuhuma yeyote ya wizi,ufisadi..,hana kampuni yeyota ya biashara amekuwa mwadilifu,mchapakazi,na anafuata sheria invyosema ndio maana suala la bomoa bomoa lilimletea matatizo kdg..JOHN POMBE MAGUFULI wil be the next President of Tanzania kama CCM hamtaki CHADEMA tunamtaka

Aachani Kumchafua mzee wa watu! John Magufuli fanya kazi...,achana na hao wanaonza kufanya kampeni za uraisi mapema paka wanakigawa chama na watanzania! BECAUSE GOD LOVES TANZANIA AND MAGUFULI WIL BE THE NEXT PRESIDENT..GOD CAN'T GIVE US A THIEVE TO BE OUR PRESIDENT
 
hawa ndio walewale wezi tu, hiyo itakuwa ni njia nyingine ya kujipatia mahela kiulaini........kuna kitu gani cha maana walichofanya hata katika miji midogo mpaka waone kuna umuhimu wa Dar kuwa na wizara maalum....hovyooooo
 
Ametuonyesha umuhimu wa kuwa na katiba mpya ambayo itaweka wazi idadi ya wizara na majina yake kwani mtu kama huyo ambaye ni miongoni mwa wagombea watarajiwa wa urais wa chama chake endapo akiwa ndiye kiongozi wa nchi anaweza kujiamulia kuweka mawizara kibao yasiyo na tija.

Kwani Meya wa jiji na City Council kazi yake ni nini? Au kukiwa na wizara hiyo inamaana Dar es salaam City council haitakuwepo au kutafutiana ulaji tu.

Hizo wizara nyingine tulizo nazo mbona hatuoni lolote la maana wanalolifanya? Marekani na ukubwa wake pamoja na utajiri wake wana wizara 6 tu na mambop yao supa.
 
yeye angesema taasisi za serikali hazina ushirikiano au master plan ya Pamoja ktk miundombinu barabara,umeme,maji safi na taka,ardhi

Wewe wasema, lakini pamoja na mipango na ushirikiano wa taasisi za serikali nchini, lakini kwa uwezo wetu wa kiuchumi, Dar es Salaam inahitaji sasa priority maalum ili kuweza kumaliza matatizo ya miundombinu iliyonayo, with time mtatambua jinsi hii point ya Magufuli ilivyo na akili..
 
Jamani DSM ni uso wa TZ na inahitaji uwekezaji mkubwa kama ambao China iliwahi fanya kwenye miji yake mikubwa ya Beijing & Shanghai kwenye miaka ya 90 (kulikuwa na wizara maalum na ilikuwa inatumia 10% ya pato la taifa kwenye miji hii). Tukumbuke pia kwamba hata sisi huko nyuma tulishawahi kuwa na wizara ya CDA, ambayo ndiyo imeifikisha Dodoma hapo ilipo (vinginevyo bado ingekuwa kama Manyoni au Singida). Kwa hiyo nadhani Magufuli ana hoja nzuri tu/tuiunge mkono.

Jirani zetu Kenya wanafanya hili. Wamejifunza toka nchi nyingine na sasa wana wizara. Dar ikisimama nchi nzima itasimama. Kila kitu kiko hapa Dar es Salaam. Hivyo huwezi kulinganisha Tanzania na nchi nyingine zenye 'alternative cities kwa huduma muhimu za jamii. Hapa kwetu ni DAR or nothing!

Watu wanaweza kubeza hili wazo la Magufuli lakini hebu takae chini na kutafakari kwa makini. Kuna Wizara za hovyo kabisa na hata mawaziri wa hizo wizara sina hakika wanafanya nini cha maana. Mfano hapo chini:

1.Wassira - mahusiano (kitengo ndani ya wizara kingetosha)
2. Lukuvi - uratibu (kitengo kingetosha)
3. Mary Nagu - uwekezaji (Wizara ya viwanda na biashara zinafanya nini?)
4. Mathias Chikawe - Utawala bora (hii ni cross-cutting issue, huwezi kuwa na wizara ya katiba na sheria halafu ukawa na wizara nyingine ya utawala bora!)

Ukitazama hizo wizara nne ni kupoteza kodi za watanzania. Ni afadhali mara mia kuwa na Wizara itakayohusika na Dar es Salaam kuliko kuendelea kuwa na usanii wa wakina Wassira. Hatuwezi kushindana na nchi jirani kama Dar es Salaam itaendelea kuwa kama ilivyo sasa.
 
Jamani Watanzania Tuache Ushabiki wa Kisiasa...na tusiongee vitu bila logic,kufikiria au kutofanya utafiti

Wenzetu Kenya...,wana wizara maalumu ya jiji la Nairobi ambako wameweza kushughulikia mambo mbalimbali na kutatua kero zinalozisakama jiji la Nairobi kama barabara,maji,usalama na vilevile wameweza kuwa na mipango mirefu na endelevu ya jiji la nairobi

Mfano mzuri pia Tanzania tuna kanda maalumu ya ulinzi wa jiji la Dar es salaam,tuna pia ulinzi maalumu katika wilaya ya tarime ambapo kuna matukio mengi

Jamani Dk.John Magufuli sio mjinga eti kaamka leo asubuhi ndio kasema...,hilo suala kalifanyia utafiti,kaona mazuri yake na tathmini zake..kama mnavyomjua yeye ni mtu wa kufuata utaratibu wenye kuelewa wanamwelewa ila wenye ulemavu wa fikra mnaleta siasa..huyu ndio raisi tunayemtaka msimamo kama paul kagame siyo kwenda kuhonga makanisani na kutumia vijana kumsafisha kwenye JF..

Moto wa Dk.John Magufuli Lowasa hatii mguu...,bila yeye leo CCM wangelikosa jimbo la Igunga..,bila yeye leo Uvuvi haramu bado ungekuwa tatizo kanda la Ziwa,Tukumbuke 2005 alifanya nini kwenye sekta ya barabara...Watanzania jamani tusimkosee heshima huyu jamaa

Hana tuhuma yeyote ya wizi,ufisadi..,hana kampuni yeyota ya biashara amekuwa mwadilifu,mchapakazi,na anafuata sheria invyosema ndio maana suala la bomoa bomoa lilimletea matatizo kdg..JOHN POMBE MAGUFULI wil be the next President of Tanzania kama CCM hamtaki CHADEMA tunamtaka

Aachani Kumchafua mzee wa watu! John Magufuli fanya kazi...,achana na hao wanaonza kufanya kampeni za uraisi mapema paka wanakigawa chama na watanzania! BECAUSE GOD LOVES TANZANIA AND MAGUFULI WIL BE THE NEXT PRESIDENT..GOD CAN'T GIVE US A THIEVE TO BE OUR PRESIDENT

Hizo sehemu 2 nyekundu - mara tuache ushabiki wa kisiasa, mara fulani will be the next president: Si wewe ndiye mshabiki wa kisiasa?
 
Nadhani Magufuli ana point nzuri. Kama cda ilivyofanya kazi ya kuipaisha Dodoma, Dar sasa hivi inahitaji the same thing. Matatizo ya Dar ni makubwa kiasi kwamba bila kuwepo mkakati maalum wa kitaifa wa muda mrefu, utafika wakati badala ya kuwa Jiji kitakuwa kijiji. Endeleeni tu kudharau ushauri wa Magufuli muone matokeo ya kazi za kina Masaburi.
 
Back
Top Bottom