John Kitime anena "Tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi"

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Hii nimeiona Facebook Wall ya Mzee John Kitime na nikaona si vibaya kuileta hapa tuijadili maana ina ukweli mkubwa sana ndani na mafundisho kwa jamii yetu.

John Kitime

Dah hii kali, jamaa alikuwa amelazwa, zikatakiwa laki5 afanyiwe operesheni, ndugu wakapiga chenga mwezi mzima hawana pesa mpaka akafariki. Siku mbili baada ya hapo walikuwa wameshachangia,
Sanduku-700,000.00
Usafiri- 1,500,000.00
Tshirt- 400,000.00
Chakula- 1,237,000.00
MASHADA-237,000.00

Halafu wanadai,'TULIMPENDA LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAIDI'.....UNAFIKIIIIIIIIIIIII​IIIIIIIIIIIIIII
 
Walishindwa kuchanga pesa chache ili apone,wameweza changa nyingi.Duniani kuna mambo
 
Haya mambo haya,yanatia hasira sana,tena wale ndugu wenye pesa waliokataa kumsaidia mgonjwa ndo hao wanaomobilize michango na wanakamilisha michakato!
Walishindwa kuchanga pesa chache ili apone,wameweza changa nyingi.Duniani kuna mambo
 
Hii inanikumbusha wimbo wa Sikinde uitwao "HURUMA KWA WAGONJWA".

Wimbo huu unaelezea umuhimu wa kuwasaidia ndugu wakiwa hai. Wao husubiri siku ya mazishi ili kujionyesha na Makamera ya bei mbaya, suti na viatu vya bei juu. Kwenye misiba kweli sura kuuza ni rahisi kuliko kwenye magonjwa hospital.

Taratibu tutafika maana kama tumeshaanza kuliongea, ina maana wengi linatutibua.
 
tena wale walio piga chenga wakati wa ugonjwa
msibani wanakuwa wapo mbele mbele sana tu ili waonekane.
 
Sana tu Mkuu. Yaani wauza sura Hospital wanaikimbia kama ukoma. Hospital hauzi vizuri kama Misiba.

Na hasa kama msiba upo Dar. Ona Mr. Eboo (M-Masaai) amefariki na kuzikiwa kijijini kwao, Wauza sura wakasepa.

Watu walipiga mahesabu wakaona, duu, ukienda hadi Arusha na huko kwenye mazishi hakuna hata Camera..... Jamaa wakapiga mahesabu na kuja na jibu la "Kama ni noma na iwe noma.......", Arusha haendi mtu.
tena wale walio piga chenga wakati wa ugonjwa
msibani wanakuwa wapo mbele mbele sana tu ili waonekane.
 
Pole zake. Kila kifo ni matokeo ya uzembe. Nani katili ndugu au hospital walioshindwa kumuhudumia kisa hana laki5.
 
Watu wanatafutia sifa kwa marehemu tu. mgonjwa halipi!
Kaaz kwel kwel!
 
hii ipo sana. Wakati mwingine bora kuepuka lawama kwa kuchangia matibabu hata kama mnajua mgonjwa hatapona
 
Jamani msiba wa nan?Au ndo jamaa mmoja kasema J.M.Msofee ikiwa ndiye alikuwa na wadhfa gan?
 
Muwe mnasoma thread na kuielewa kabla ya kupost, hakuna msiba hapa, angel kakumbuka hili lililoandikwa hapa pengine lilitokea kwenye msiba wa babu yake

Jamani msiba wa nan?Au ndo jamaa mmoja kasema J.M.Msofee ikiwa ndiye alikuwa na wadhfa gan?
 
eeh Mungu mwingi wa rehema nakuomba unipe ujasiri wa kuchangia wagonjwa na uniondolee ujasiri wa kuchangia harusi,sendoff,get together na kipaimara AMEN
 
Duuu, hilo nalo neno. Wanaita Mchango wa ONE WAY TICKET and never come back.

Wanakuja kabisa na suti nzito ili wakuage na milele usiwasumbue tena, khaaa!!!
Wanajua huo ndo mchango wao wa mwisho kwa muhusika.
 
Hii ni kawaida kwa binadamu hasa wanafiki, na hasa pale wanapo changia harusi pia kwa mamilioni huku vijana wakikosa karo na hata wakiambiwa wachangishe pesa za karo huta waona....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom