The Priest
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 1,029
- 256
Hapo kwenye red,sasa mlijuaje kama hamna intelligence ya kutosha...siasa bwanaHatimaye CHADEMA tumevuka tanuru jingine la uchaguzi huu.Namshukuru MUNGU sana.Ndugu zangu CHADEMA hivi sasa imekua na kuwa na maadui wengi sana.Tunapigwa na vyama vyote vya siasa iwe chama kilichopo maradarakani au vya upinzani.Uchaguzi huu ulikuwa ni mtihani mwingine kwa chama.Wagombea wengi sana walijitokeza katika nafasi mbalimbali zilizotangazwa.Mwanzoni tulifurahi sana tukijua kuwa chama kimekuwa sana lakini humo humo wagombea ambao hawakuwa na nia njema na CHADEMA walijitokeza.Katika kila nafasii kulikuwa na wagombea ambao hawakuwaserious na lengo la kuitaka nafasi hiyo,wengine walikuwa wapo kwaajili ya kugawa kura,wengine waliomba kwaajili ya kuuza sura na wengine waliomba kwaajili ya maslahi binafsi/maslahi ya watu binafsi na kuna wengine walikuwa wanadhamira njema kabisa ya kutaka kuwatumikia vijana na kukijenga chama kwa maslahi ya chama.Pamoja na kwamba CHADEMA hatuna Kitengo thabiti cha Intelejensia(Kwa maana ya watu wenye Taaluma hii ).lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya.Baadhi yao wakaenguliwa kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za chama na baadhi walishindwa kwenye sanduku la kura. Binafsi nilikuwa naziangalia nafasi nyeti ili zipate viongozi wazuri wenye nia nzuri ya kujenga chama na waliogombea kwa ridhaa zao sio kwa kuwekwa au kushawishiwa na watu fulani.
Nafasi ya Uenyekiti nimefurahi ameshinda John Heche na ndio alikuwa chaguo langu tangu mwanzo 2009.Heche ana misimamo anaweza kusimamia misimamo yake na anamalengo mazuri na BAVICHA.Amegombea kwa ridhaa yake. HONGERA chalii Heche.
Nasubiri kuona tunapata Katibu Mkuu , Mwekahazina na Mratibu wa Uhamasishaji wazuri kwa maslahi ya chama.
Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.