John chiligati vs wapinzani: Vita vya maneno!

Hayo maneno ya Chiligati yanaonyesha jinsi alivyojisahau kutetea maslahi ya majority (wananchi wote wanaoathirika kwa ajili ya ufisadi). Inauma sana unapoona kiongozi bila ya aibu anaongea maneno yasiyo na busara. Ifikie wakati viongozi wetu washtuke na kubadili mtazamo wa mambo! wananchi tumechoka kunyanyaswa na kudharauriwa kwa utapeli wa wanasiasa wetu!
 
- Ndugu nimekusikia, kwamba samaki mmoja akioza wote wameoza, sasa naomba kuweka swali la nyongeza, eti Bin Laden anawakilisha mawazo ya Waisilamu wote duniani?

Ahsante.

William.

Mkuu W. J. Malecela, swali lako ni zuri sana.

Suala la imani ni gumu kulizungumzia bila kuingilia uhuru na haki za waumini. Hivyo ni vizuri kuwa makini kuzungumzia masuala ya dini.

Pamoja na kuwa Osama Bin Laden amehusisha vitendo vyake (terrorism) kwa kiasi fulani na dini yake, kwa upande mwingine amehusisha na chuki zake binafsi kwa Marekani (ambazo hazihusiani kabisa na dini yake). Kama wewe ni mfuatiliaji, utagundua kuwa vitendo vyake vimeichafua dini yake na asili yake (uarabu) kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa kuwa wengi wentu tumesikia na kufahamu kuwa kikundi chake (Al-Queda) kiliundwa na kusimamia misingi gani, inakuwa si busara wala haki kuhusisha vitendo vya Osama na dini yoyote.
 
- Mkuu heshima yako sana, naona ni lazima nikupe kwamba wewe ni mwanasiasa mtarajiwa mzuri sana jinsi unavyoweza kujaribu kuizunguka hoja, ahsante nimekusikia.

William.
 
Back
Top Bottom