Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
Hiki ni kichekesho cha hali ya juu. Hivi kusema ukweli ambao unajulikana na kila Mtanzania anayefuatilia mambo ya siasa nchini kwamba CCM ni chama cha mafisafi ni kashfa!!!?
Mbona mafisadi waliojaa ndani ya chama hicho akina Mkapa, Lowassa, Msabaha, Mkono, Karamagi, Mramba, Rostam Azizi, Chenge na wengineo chungu nzima hawajachukuliwa hatua yeyote kuhusiana na ufisadi wao dhidi ya nchi yetu!? Safisheni chama ambacho mmeruhusu kichafuke kwa kukumbatia mafisadi vinginevyo ukweli ndiyo huo kwamba CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi kama kilivyo miaka ya nyuma bali ni chama cha mafisadi.
BUBU, Bangusilo si fisadi kwani alishasema toka bungeni na kweli sasa inajulikana taratibu