Joe Thomas awafunika Boyz II Men Dar katika Likizo Tyme

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
MWANAMUZIKI wa miondoko ya taratibu (Rhythm & Blues ÐR&B) Joseph Lewis Thomas “Joe Thomas”, usiku wa kuamkia leo aliweza kusahaulisha umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha la Likizo Tyme kutokuwapo kwa kundi la Boys II Men.

Katika tamasha hilo lililoandaliwa na Entertainment Masters (EM) na kufanyika katika viwanja vya Leaders, awali lilionekana kupooza na kupoteza ladha yake iliyozoeleweka kila mwaka.

Mara baada ya kutambulishwa kwa Joe Thomas saa 6:30 usiku, mashabiki walilipuka kwa shangwe na kuanza kumshangilia bingwa huyo wa muziki wa taratibu.

Joe Thomas aliweza kukonga nyoyo za mashabiki hao alipoanza na nyimbo zake kadhaa zikiwemo I'm In Love, All Or Nothing, The One For Me, All the Things (Your Man Won't Do), Don't Wanna Be a Player, I Wanna Know, Treat Her Like a Lady, Stutter (Remix), Let's Stay Home Tonight, Better Days. It Won't End, What If a Woman, More & More na Priceless.

Habari zaidi na picha zaidi za Likizo Tyme gonga hapaNIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom