Job Ndugai awachefua wasomi, wanaharakati

1800

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
2,215
603
WASOMI na Wanaharakati wameponda kauli ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kulinganisha posho za wabunge na majaji pamoja na wanataaluma wengine serikalini wakisema 'ni kauli ya mchumia tumbo.'

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana walisema mbunge hawezi kulinganishwa na mtu aliyesotea taaluma ya ujaji au fani yeyote, akilipa ada na kuvumilia tabu zote hadi kumaliza masomo.Walisema kauli hiyo ya Ndugai inatia shaka juu ya nia ya dhati ya viongozi wa kisiasa kuwatumikia wananchi ambao waliwapigia kura kwa kudhani kuwa wangewasaidia.

Wakili wa kujitegemea, Daniel John alimtaka Ndugai asifananishe majaji na wabunge kwani majaji ni wataalamu na wabunge ni wanasiasa."Hii ni dharau kubwa sana kwani hivi sasa viongozi hawaheshimiani kabisa, ni sawa na familia isiyojua mkubwa ni nani na nani anastahili kuheshimiwa vipi," alisema.

Aliendelea “Hivi mwanasiasa unawezaje kujilinganisha na fani ya mtu ambayo ameisotea kwa muda wa miaka mingi akivumilia shida na taabu? Kama unaona ubunge hauna maslahi kwa nini uligombea?. Huu ni ukosefu wa maadili kabisa,” alisema John.

Profesa Chris Peter Maina alisema, Ndugai asipotoshe jamii kwani hakuna jaji au mtumishi yeyote anayelipwa posho kwa kwenda mahakamani au kufanya kazi yake.Alifafanua kwamba majaji na watumishi wengine wa Serikali hulipwa posho pale wanapotoka katika vituo vyao vya kazi na wabunge kukaa bungeni ni sehemu ya majukumu ya kazi yao.

“Hivi inawezekanaje ukalipwa posho kwa kazi yako? Mbunge kukaa bungeni ni kazi yake, sasa kama kila mtumishi atataka alipwe posho kwa kufanya kazi yake, ni dhahiri hata walimu wakifundisha kipindi darasani wadai posho,”alisema profesa Maina.

Aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, Felix Kibodya alisema Wabunge wanapaswa kujiuliza kuwa hicho wanacholipwa kinalingana na wanayowafanyia wananchi badala ya kujali matumbo yao.
“Wananchi wanalalamika kuhusu posho hizo kwa sababu hawaoni kitu chochote wanachofanya Wabunge hao, jaji au mtumishi mwingine wa Serikali kulipwa posho kubwa sio hoja, hoja ni hiyo posho unayojiongezea na kujipandishia,”alisema Kibodya.

Mhadhiri wa Chuo kikuu huria cha Dar es Salaam, Hussein Bakari alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya kutetea wezi ambapo mtu ukihoji ubadhilifu unaambiwa hayo ni majungu au wivu toa kauli za maendeleo.

"Hivi kweli maendeleo yanaweza kuja wakati fedha za kuleta maendeleo hayo zinateketezwa kwa namna hiyo?", alihoji.Alisema hili ni tatizo la Chama tawala kuwa na wabunge wengi kwani wanapitisha kila kitu hata kama ni kibaya. Alisema ipo haja ya kuwa na wabunge wengi wa upinzani ili kuwapo ushindani wa hoja.

“Kauli za Ndungai mzoefu wa miaka mingi na anaelewa kinachoendelea na ana cheo kikubwa anashidwaje kukemea mambo yasiyo na tija kwa taifa letu?”alihoji.

Mkazi wa Tabata Zainab Mmari alihoji “Kwa hiyo ukimwona jambazi anapora na wewe unakuwa jambazi? Hivi kweli sasa hakuna hata kiongozi anayeweza kuiokoa nchi hii kwani kila anayetegemewa mwisho wake ni kuropoka maneno ambayo yanazidi kutuchanganya wananchi,”, alihoji.

Alisema huu ni wazimu kwani haiwezekani kiongozi mkubwa kama Ndugai atoe kauli hizo zinazokera kwa wananchi anaowaongoza.“Tanzania imefikia mahali maadili yameporomoka kabisa mpaka viongozi wetu wamefikia katika hatua ya kutamka wazi juu ya ni nani anakula zaidi badala ya kutaka kujua ni nani anawajibika zaidi na kutuletea maendeleo", alisema.
 
sijaona popote ambapo ndugai kasema vibaya. Tatizo kuna hili kundi la watu wanajiita critics. Wao huangalia makosa tu kwenye kila kauli ya mtu. Ni wapuuzi kwa namna fulani. Ndugai pamoja na kutoa mifano hai, mwisho kapendekeza nini kifanyike. Kwa nini hao critics hawajachambua pendekezo lake zaidi ya kumwita mchumia tumbo? Na kama ni taaluma hata ndani ya bunge kuna wanataaluma pia
 
Back
Top Bottom