Job Ndugai asema wabunge wa bunge la jioni hawako sawa, walevi!

Akiongea ktk kipindi cha "Medani za Siasa na Uchumi" kinachorushwa na Star Tv,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la JMT ameelezea kuwa wabunge wengi wenye matendo kama Halima Mdee inasadikika kuwa wanatumia sigara kali,kuvuta unga au kunywa bia ktk kipindi cha mchana cha Bunge!amethibitisha hayo kutokana na matendo aliyofanyiwa na H.Mdee kwa kunyooshewa kidole cha kati wakati alipomkatalia kuomba mwongozo ktk sakata la Dr.Ndugulile!!....Lakini ktk hali ya kushangaza Mh.NDUGAI ameshindwa kujua ana watoto wangapi na wake wangapi!na amesema hawezi kujibu swali hilo mana hajui idadi ya wake na watoto wake!PIA AMESIKITIKA KUPATA WAKATI MGUMU KUKUTANA NA KASHFA NA MATUSI HASA KTK MTANDAO WA JAMII FORUM KUTOKANA NA KAZI YAKE YA UNAIBU SPIKA
hapa umetia chunvi hakusema kama ulivyoandika.
 
Kawaonya watu kuwa makini na wanachokula, wasidhani kula hovyo ni afya... nadhani alikuwa anafanya reference kwa uzito wake na hali ya afya aliyokuwa nayo hivi karibuni... ethically nisingependa kucomment

Ahsante mkuu, umedhihirisha u-profesa wako hata kama ni kwa jina tu.
Ulichokiandika kitawasaidia wana JF wengi sana kiafya watakaopitia mchango wako huo.
 
kweli watanzania tumelaaniwa! wabunge mafisadi, wezi, walevi.,wavuta bangi!! nani atatutetea??
 
Naibu spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwamba Wabunge wengi wanaingia Bungeni wakiwa wamelewa pombe na kuvuta sigara ziziso za kawaida.
My take:
Kumbe zile jazba si bure.
Nadhani pia hii ni kwasababu Bunge lilipitisha bajeti ambayo kwa asilimia kubwa inaendeshwa kwa kodi za pombe na sigara.
 
Kauli ya Naibu Spika aliyoitoa alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Star tv, hata mie iliniacha hoi. Ila niliipenda kwani nadhani ina-ukweli kabisa. Bravo Ndugai!!
 
Kubali au kataa,tunatungiwa sheria na walevi na walevi hawa hawa wanapitisha miswada kibao ili iwe sheria.
Sasa katika utekelezaji wake lazima mtu mwenye akili timamu ashindwe kuzifuata au aone zina hitlafu katika utekelezaji wake maana yeye si mlevi.
Bunge linageuzwa club/Bar ya pombe hadi spika anashtukia hali hii.Tumefika mbali.
Labda wabunge hawa walipata kura kwa kuhonga vileo wapiga kura hivyo wanawakilisha watu wenye akili punguani/walevi,yaani wasioweza kutawala kauli,fikra au mtazamo wakati pombe ikiwa kichwani.
Acheni kudhalilisha Bunge na kushusha utu wenu watanzania tunawatazama.
 
Acha nyonga ikatike kabisa,
zee zima kubemenda vitoto vya wenzie,
wangeongeza kidogo hiyo dawa ya usingizi alale milele, ovyo.

Halafu Mademu wenyewe ni kama yule anayesota maabusu aliyekuwa anabeba zile tani mbili za Mwimbaji na Mbunge wa CCM ambaye siku za karibuni nyonga yake ililegea
 
Monday, 06 August 2012 22:06


Dismas Lyassa na Boniface Meena

WAKATI kashfa ya baadhi ya wabunge kuhongwa na kampuni za mafuta ili yatetee mikataba yao haijapoa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ameibua tuhuma nyingine nzito kwamba baadhi ya wawakilishi hao wamekuwa wakiingia kwenye vikao wakiwa wamelewa pombe na sigara zisizo za kawaida.

Katika siku karibuni, baadhi ya wabunge wamekuwa wakinaswa na kamera wakiwa wamelala bungeni wakati vikao vinaendelea, kwa maelezo ya uchovu, kauli ambayo huenda sasa ikaongeza mjadala miongoni kama kinachosababisha walale wakati vikao vinaendelea iwapo ni uchovu wa kazi au ulevi.

"Kuna wabunge ninavyohisi wanaingia bungeni wakiwa wamevuta sigara fulani kubwa, kulamba vitu fulani au hata kupata bia mbili tatu," alisema Ndugai akihojiwa jana asubuhi katika kipindi cha medani za siasa na uchumi cha Star tv.

Ndugai alisema amekuwa akiona hali hiyo hasa Bunge la kuanzia mchana, bila kueleza ni hatua ambazo zimekuwa zikifanyika kupambana na wawakilishi hao wa wananchi wanapobainika wamelewa.

"Wabunge ni watu kama watu wengine, wana tabia kama walivyo wanadamu wengine, wapo ambao kwa namna ninavyohisi wanaingia bungeni hasa vikao vya kuanzia mchana wakiwa wamepiga bia," alisisitiza Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa, mkoani Dodoma.

Ingawa hakufafanua, inavyofahamika sigara yenye kulevya ni bangi,kulamba vitu fulani vyenye kulewesha maana yake inaweza kuwa kuna baadhi ya wabunge wanatumia dawa za kulevya, pia ulevi mwingine wa kutumia bia.

Bila kueleza hatua ambazo Bunge linachukua kwa wabunge walevi,
Ndugai aliwataka wabunge kuweka maslahi ya taifa mbele na kujenga
tabia ya kuongea mambo wakiwa na ushahidi.

"Ni kwamba kuna wabunge wamekuwa wakizungumza mambo bila ushahidi,
hili jambo halikubali, wabunge wanapaswa kuzingatia sheria kama
walivyo Watanzania wengine, unapomtuhumu mtu lazima uwe na
ushahidi, lakini inasikitisha sana unakuta mbunge anasema jambo,
anamtaja mtu kwamba anahusika na hili na lile wakati hana hata chembe
ya ushahidi," alisema.

Pia, aliwataka wanasiasa wote kujenga tabia za kuthamini yale ambayo yanafanywa na wanasiasa wengine.

"Nimekuwa nikifuatilia mambo yanavyokwenda nchini, kuna wanasiasa wanakosea, unakuta mpinzani amekuwa akisema mabaya tu kwa chama tawala, unakuta tunaitwa mafisadi, siyo sahihi, kwa mfano Star tv kukawa na mtu mgoni, ni tatizo la huyo haina maana kwamba wafanyakazi wote ni wagoni. CCM ni taasisi kubwa, mambo haya yanaweza kutokea.

Lakini pia siyo kweli kwamba wanachama na viongozi wote wa upinzani ni wasafi," alisema Ndugai na kuongeza:

"Kuna wanasiasa wamekuwa na tabia ya kuona kila kinachofanywa na CCM
ni ushetani, hiyo siyo sawa! Kwa mfano mimi jimboni nimefanya maendeleo mengi. Wakati naingia Bungeni mwaka 2000 kulikuwa na shule chache mno za sekondari, lakini sasa ziko zaidi ya 30, hata zahanati zilikuwa chache sasa ni zaidi ya 40, ni kutokana na jitihada zangu na chama changu, mtu anapokuja kusema hatujafanya kitu tunashindwa kumuelewa."

Naibu Spika huyo alikwenda mbali zaidi na kuwashauri viongozi wa Serikali akiwamo Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na utaratibu wa kupitia kauli zinazotolewa na wanasiasa, kwa maelezo kuwa baadhi yao wamekuwa wakitoa kauli nzito, au kukashifiana bila kuchukuliwa hatua.

"Unaweza kukuta mwanasiasa anaibua kashfa nzito, lakini hachukuliwi hatua wala kuulizwa, hiyo siyo sahihi. Wanasiasa tunapaswa kubishana kwa hoja, siyo vinginevyo," alisema Ndugai.

Ndugai alipoulizwa kuwa wabunge hao hatua watakazochukuliwa kutokana na tabia zao, alisema suala hilo haina haja ya kulizungumzia zaidi ila libaki kama alivyosema.

"Hilo siwezi kulizungumzia zaidi libaki kama nilivyozungumza na walioniomba nizungumze nao," alisema.
 

Hivi Wabunge wa Zamani walikuwa wachafu kama hawa? Huu ni Mwezi mtukufu wa Ramadhani na wengine

Wanakwenda kuwasindikiza Waislamu kufuturu... na wanalewa Mchana? Kweli Wananchi wa Tanzania we are duped
 
na wanavuta sigara fulani kubwa!! Me luv this only..!! Nahisi wanafunzi wa iyunga, old moshi,box 2, musoma etc wa enzi hizooo wamehamia bungeni.
 
Basi wa kwanza atakua ni huyu lazima anapiga maji ya Gold kabla ya vikao vya bunge!
komba.jpg
 
Kwakumnukuu Naibu Spika kua kuna wabunge pia wanaingia Bungeni wakiwa wamevuta (sigara zisizo za kawaida - By Ndugai) basi bila shaka atakua ni huyu!
Mrema%2Bchapa%2BUsingizi%2B3%2B%25282%2529.jpg
 
Back
Top Bottom