Job Ndugai asema wabunge wa bunge la jioni hawako sawa, walevi!

Ndugai anasema kwamba wakati anamwamlisha Halima mdee akae chini alipoomba kutoa taarifa wakati Naibu spika anataka kutoa maamuzi kwenye issue Mh. Ndugulile.
Mh. Ndugai anasema Mh. Mdee alikuwa akimuonyesha kidole cha kati.
Kama kuna mtu anapicha ya hilo tukio naomba aiweke hapa tuone kama anachosema ndugai ni kweli au laa...
Nadhani Ndugai atakuwa nayo hiyo picha, muombe tu
 
Kama kuna mtu anapicha ya hilo tukio naomba aiweke hapa tuone kama anachosema ndugai ni kweli au laa...
Hiyo picha ipo ila itabidi ungoje wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ndipo itatolewa hadharani.
 
Nadhani Kipindi hiki kifocus kuongea na waheshimiwa hawa tuwapime na tujue uwezo wao, nimefurahishwa na mazungumzo ya Mh Ndugai, ninachopima ni kiwango cha unafiki na uhalisia wa habari, hata kama siridhishwi lakini nafurahishwa sana na jinsi ambavyo Mheshimiwa huyu kama alivyokuwa akiongea Mh Membe katika Dk 45 unauona uhalisia kwa kiwango kikubwa. Pia kwa waheshimiwa kama hawa ni raihisi ahata kuona maeneo ya kibinadamu, kisiasa na ya kikazi zaidi na hawazungushi, tuendelee kupima, natamani kuona wengi wanaletwa kwenye media forums hizi maana hawa wenzangu wa CCM waliingia mitini kutokana na fikra finyu za Katibu Mkuu wa kipindi hicho na wenzake kudhani ni hatari nna sio opportunity kusimama nkwenye media Forum nna kuargue mambo, tena ilikuwa aibu zaidi maana kilikuwa chombo cha serikali TBC, na uchafu zaidi na ushenzi ni kumtimua Jembe la ukweli. Ah Hongera Star TV, TBC matatizo tu kwa sasa, sikumbuki mara ya mwisho niliangalia lini na niliacha baada ya kukerwa na habari za kinafiki na zilizo jaa uzembe na udhaifu wa kitaaluma kiasi kwamba unaona kabisa kinachoelezwa kinatufanya sisi wote wajinga. Any way kila la kheri Waandishi wa Habari tuleteeni zaidi hawa watu tuwapime
 
Heshima kwenu wanabodi.
Kwanza napenda kutoa pongezi kwa member mwenzetu wa JF Naibu Spika Job Ndugai, hii inaonesha JF imefika mbali zaidi hadi ndani ya bunge letu.

Turudi kwenye hoja ya Ndugai kuhusu ulevi wa wabunge wetu ni aibu mbunge kuingia bungeni huku umetoka bar kunywa bia au valeur...kweli utatoa mchango gani zaidi ya matusi.
 
Mbona hakusema kuwa wakati wenzake wanaenda kulewa na wengine "kuvuta" yeye huwa anaenda kufanya nini? Mbona naye huonekana kuchoka na kukosa mawasiliano (coordination) mpaka akurupushwe na Muongozo wa Spika kutoka kwa mheshimiwa anayetoka kule ambapo mbegu za bangi hupikiwa mboga?

unamaanisha VI LUKU, yule mzee wa miongozo, au!?
 
hana cha picha wala nini, ingekuwepo inge-pamba front page ya gazeti la uhuru
 
Tatizo la mbunge wangu hana utulivu wa nafsi pumziko wakati mwingine anakurupuka.
 
Nimemsikia akizungumza mengi, yakiwemo yanayojenga na mengine ya kipuuzi;

Yanayofaa ni kama wanasiasa wadhibitiwe waache matusi, kashfa na tuhuma zisizo na uthibitisho ndani na nje ya bunge.

Ya kipuuzi ni kama kusema wabunge huingia jioni wakiwa wamelewa, wanatumia madawa ya kulevya etc. kama ni kweli kwa nini asitumie nafasi yake kusaidia vyombo vinavyohusika kuwashughulikia?

Lingine la kipuuzi ni kuhusu mh. Halima Mdee kumuonyesha kidole cha kati kama ishara ya matusi, kwa nini asitumie taratibu na kanuni kuthibitisha ili Halima aadhibiwe kwa kitendo hicho?

La kipuuzi zaidi ni yeye kushindwa kujua familia yake, hajui ana wake na watoto wangapi. Kama tunaongozwa na watu ambao hawajui hata idadi ya wanafamilia wao ni hatari kwa mustakabali wetu, mtu ambaye hawezi kuongoza familia anapewa jukumu la kuongoza taifa?
 
Hebu angalia hizo thread - maudhui na muda ambao zimeanzishwa. Nadhani JF kwa sasa kuna "utoto" mwingi sana. Yaani in short mtu akiona thread fulani humu naye anaanzisha "kitu kama hicho hicho". Inakuwa kama amekumbushwa na aliyetangulia. This is stupid.

Job Ndugai asema wabunge wa bunge la jioni hawako sawa, walevi! (Started by KakaKiiza, Today 11:10; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nge-wa-bunge-la-jioni-hawako-sawa-walevi.html)

Job Ndugai: sijui nina watoto wangapi! (Started by GreenCity, Today 11:26; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299613-job-ndugai-sijui-nina-watoto-wangapi.html)

Mdee alimuonyesha Ndugai kidole cha kati.Je ni kweli? (Started by MI6, Today 11:30; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...yesha-ndugai-kidole-cha-kati-je-ni-kweli.html)
 
Nadhani yeye ndio atakuwa mlevi kuongea maneno kama yale.
 
Back
Top Bottom