Job Ndugai asema wabunge wa bunge la jioni hawako sawa, walevi!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Job Ndugai Naibu wa Speaker... amesema baadhi ya wabunge wa bunge lajioni wengi wanakuja wameisha lewa, wamevuta sigara mbali mbali, wanakuwa wamelamba vitu mbalimbali!!

Na kasema kampeni zinazofanyika mara nyingi ni za matusi kwenye mikutano kwa vyama vyote pamoja na chama chake cha CCM!! Amelaani sana viongozi kampeni za matusi kwenye mikutano....

Source: Star Tv medani za siasa na uchumi.
Nimemsikia akizungumza mengi, yakiwemo yanayojenga na mengine ya kipuuzi;

Yanayofaa ni kama wanasiasa wa wadhibitiwe waache matusi, kashfa na tuhuma zisizo na uthibitisho ndani na nje ya bunge.

Ya kipuuzi ni kama kusema wabunge huingia jioni wakiwa wamelewa, wanatumia madawa ya kulevya etc. kama ni kweli kwa nini asitumie nafasi yake kusaidia vyombo vinavyohusika kuwashughulikia?

Lingine la kipuuzi ni kuhusu mh. Halima Mdee kumuonyesha kidole cha kati kama ishara ya matusi, kwa nini asitumie taratibu na kanuni kuthibitisha na ili Halima aadhibiwe kwa kitendo hicho?

La kipuuzi zaidi ni yeye kushindwa kujua familia yake, hajui ana wake na watoto wangapi. Kama tunaongozwa na watu ambao hawajui hata idadi ya wanafamilia wao ni hatari kwa mustakabali wetu, mtu hawezi kuongoza familia anapewa jukumu la kuongoza taifa?
 
Mh. Job Ndugai akiongea na kipindi cha Medani za siasa cha star tv anasema baadhi ya wabunge huingia wakiwa wakunywa bia, wamevuta sigara (anamaanisha bangi) na pengine wanakuwa wamelanmba vitu vyao (Hapa anamaanisha wanalanga).

Maneno haya anayatoa wakati akizungumzia sakata la kumtupia maneno mabaya Halima Mdee wakati akitaka kutoa taarifa wakati naib spika alipokuwa anaeleza issue ya Ndugulile (mbunge wa kigamboni)
 
Akifanya interview katika kipindi cha medani za siasa katika kituo cha Startv cha kila jumapili amesema baadhi ya wabunge wanaingia Bungeni wakiwa wamevuta sigara zisizo za kawaida au unga na wengine wanaingia wakiwa wamechapa maji ndio maana bunge linakosa nidhamu. Muongozo! Taarifa! Wabunge wanatoka katika jamii yetu hiihii!
 
Job Ndugai Naibu wa Speaker...amesema baadhi ya wabunge wa bunge lajioni wengi wanakuja wameisha lewa.wamevuta sigara mbali mbali,wanakuwa wamelamba vitu mbalimbali!!.............Nakasema kampeni zinazofanyika mara nyingi ni za matusi kwenye mikutano kwa vyama vyote pamoja na chama chake cha CCM!!Amelaani sana viongozi kampeni za matusi kwenye mikutano....

Source :Star Tv medani za siasa na uchumi.

Mbona hakusema kuwa wakati wenzake wanaenda kulewa na wengine "kuvuta" yeye huwa anaenda kufanya nini? Mbona naye huonekana kuchoka na kukosa mawasiliano (coordination) mpaka akurupushwe na Muongozo wa Spika kutoka kwa mheshimiwa anayetoka kule ambapo mbegu za bangi hupikiwa mboga?
 
mmh, kumbe mijadala yao huwa ni upepo tu? inawezekana hali ikiwawarudia wanajikuta mambo yeshaharibika e.g sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii! je Ndungai alisema nini - bunge lina chukua hatua gani kuondoa tatizo hilo?
 
Naibu spika wa bunge amesema kuwa nyakati za mchana wabunge wanaingia bungeni wakiwa wamekunywa pombe na kuvuta sigara zisizo za kawaida (bangi) ndo maana kunatokea vurugu bungeni mara kwa mara.Ameyasema hayo ktk kipindi cha medani za siasa star tv
 
Akiongea ktk kipindi cha "Medani za Siasa na Uchumi" kinachorushwa na Star Tv,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la JMT ameelezea kuwa wabunge wengi wenye matendo kama Halima Mdee inasadikika kuwa wanatumia sigara kali,kuvuta unga au kunywa bia ktk kipindi cha mchana cha Bunge!amethibitisha hayo kutokana na matendo aliyofanyiwa na H.Mdee kwa kunyooshewa kidole cha kati wakati alipomkatalia kuomba mwongozo ktk sakata la Dr.Ndugulile!!....Lakini ktk hali ya kushangaza Mh.NDUGAI ameshindwa kujua ana watoto wangapi na wake wangapi!na amesema hawezi kujibu swali hilo mana hajui idadi ya wake na watoto wake!PIA AMESIKITIKA KUPATA WAKATI MGUMU KUKUTANA NA KASHFA NA MATUSI HASA KTK MTANDAO WA JAMII FORUM KUTOKANA NA KAZI YAKE YA UNAIBU SPIKA
 
Tafadhali Ndugai thibitisha hili.Kwa nini unaogopa kuwaambia huko Bungeni? Bahati yako Mh Lukuvi hakuwepo wakati unatoa taarifa hii (Kanuni namba 64 (1a) inazuia Maneno ya kuudhi). Au uthibitisho ni kwa wabunge wa Upinzani tu bwana Ndugai?
 
Kakubali kuwa yeye ni member wa Jamii forums.......ila anasema anaingia kwenye mitandao mara nyingi na amekuwa akitukanwa...lakini ndo utandawazi!!
 
Sasa kama walipitisha sheria mpya ya mamlaka ya kusimamia na kuthibiti mifuko ya hifadhi ya jamii mwezi aprili kwa kauli za "ndiyoooooo" bila kusoma wanachokubali na sasa wameanza tena kutoana macho juu ya sheria hiyo hiyo! Mimi nakubaliana na naibu speaker! Ni vyema akaeleza wengi wa hao wanaolewa wanatoka upande gani! Upinzani au tawala!!!
 
Anachosema Mh Ndugai ni kweli na msisahau amewataja wa vyama vyote na amelaumu pia jinsi wanasiasa wanavyoendesha siassa majukwaani na amalaumu wote wa CCM na wa vyama vya upinzani kwa kukosa hoja na nidhamu katika majukwaa, tukubali kuwa angalau haya anasema kweli. Nimependa jinsi alivyokuwa anakumbuka maisha asili akiyafurahia ni jambo ambalo wanasiasa wengine wanadhani sio mazuri kwa upofu wao wa kukaa mjini wakidhani ni maisha duni, wanasahau Madaktari wanatuhimiza turudi maisha ya asili kijijini ikiwemo kula na jinsi ya kuishi.
 
Akiongea ktk kipindi cha "Medani za Siasa na Uchumi",Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la JMT ameelezea kuwa wabunge wengi wenye matendo kama Halima Mdee inasadikika kuwa wanatumia sigara kali,kuvuta unga au kunywa bia ktk kipindi cha mchana wa cha Bunge!amethibitisha hayo kutokana na matendo aliyofanyiwa na H.Mdee kwa kunyooshewa kidole cha kati wakati alipomkatalia kuomba mwongozo!!....Lakini ktk hali ya kushangaza Mh.NDUGAI ameshindwa kujua ana watoto wangapi na wake wangapi!PIA AMESIKITIKA KUPATA WAKATI MGUMU KUKUTANA NA KASHFA NA MATUSI HASA KTK MTANDAO WA JAMII FORUM KUTOKANA NA KAZI YAKE YA UNAIBU SPIKA

Kama kweli kamtaja H. Mdee Mh Mdee ashitakiwe na Mh Ndugai awe shahidi kwa kuwa kubwia unga au kuvuta bangi ni kosa la jinai. Lakini Swali: Ndugai alimuona wapi? Ndiye anayemuwashia hilo ganja?
 
Amekataa kutaja ana wake wangapi na watoto wangapi,pia amesema kiti cha usipika anakiona cha moto na hapendi kukikalia.
 
Amesema mdee alimyooshea ishara ya kidole cha kati kama tusi ndio maana alimwita kituko.ila alivyoulizwa kuwa anayekalia kiti akitoa maneno ya kuudhi inakuweje
 
Ndugai anasema kwamba wakati anamwamlisha Halima mdee akae chini alipoomba kutoa taarifa wakati Naibu spika anataka kutoa maamuzi kwenye issue Mh. Ndugulile.
Mh. Ndugai anasema Mh. Mdee alikuwa akimuonyesha kidole cha kati.
Kama kuna mtu anapicha ya hilo tukio naomba aiweke hapa tuone kama anachosema ndugai ni kweli au laa...
 
Back
Top Bottom