JKT mbaroni Dar kwa ujambazi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watatu waliowahi kuwa wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha sambamba na watuhumiwa wengine 44.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, watuhumiwa hao walikamatwa baada ya msako mkali wa nyumba hadi nyumba uliofanywa na jeshi hilo, maeneo ya Kawe, Mbezi Beach, Goba, Salasala, Kimara na Mbezi Juu ambao ulifanikiwa kuwanasa majambazi 17.

Aliwataja wanajeshi hao kuwa ni David Dunia (23), Swedi Tamba Suleiman (22) na Nassa Hamisi Ndiaje (21) ambapo walifanikiwa kuwatambua watuhumiwa hao kutokana mbinu walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu.

Aidha, Kova alisema watuhumiwa wengine waliokamatwa katika operesheni hiyo kuwa ni Richard Daud Shirima (36) mkazi wa Kimara Tanki Bovu ambaye ni mtuhumiwa hatari na alitoroka gereza la Segerea akiwa anatumikia kifungo cha miaka 30, Joseph Muhere Marwa (38), Idd Mbaruku (32), Kelvin Lwambano (27), Matola Rashid (26), Hiari Juma (39) na Hija Kibendo (40).

Wengine ni Obeti Mwakasanga (34), Haji Jafary ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (26), William John (30), Adam Madunda (44), Naziru Ally, Joseph Mayai (38), Erick Muha (40) ambaye ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Burundi na Fabian Mahende (27).

Alivitaja vitu walivyokamatwa navyo watuhumiwa hao kuwa ni televisheni aina ya Sumsung Flat 2, laptop aina Toshiba, Camera 2 aina ya Niccon Sonny, simu za mikononi 5 aina ya Sumsung, deki za Dvd, mashine moja ya kusafishia zulia na vingine vingi.

Aidha, katika operesheni nyingine ya Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata majambazi sugu watatu ambao walipatikana na magari 10 ya wizi pamoja na pikipiki mbili ambao walitiwa mbaroni: Harod Gamaeliel (37)mkazi wa Mikocheni na mshirika wake alijulikana kama Dids Ponsian Tem (32) mkazi wa Boko ambaye alipatikana na magari 4 ambayo alikuwa ameyaficha katika sehemu tofauti.

Alisema kati ya magari manne, mawili yalitambuliwa kwa namba za usajili T.923 BCH na T352 BHH ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo la Kimara.

Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Harold Kanza ambaye alikamatwa na magari mawili ambapo moja ni Toyota Chesser no. T.923 BCYL lililoibiwa Kimara Matangini mali ya Thomas Matiku na Nissan Hadbord namba T 684 AHD mali ya kampuni ya DT DOBIE (T) Limited na mtuhumiwa huyohuyo alikamatwa na pikipiki namba T191 BBC.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Gideon ambaye alikutwa na magari mawili yenye namba T271 APV, RAV 4 T700 AYL na RV4 nyingine rangi ya kijani

Aidha kikosi cha 999 kitengo cha pikipiki kikiwa doria kilifanikiwa kukamata pikipiki namba T.892 A ambayo ilishukiwa kutumika katika tukio la ujambazi jijini na mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Mustafa Alli (25) baada ya kuhojiwa alikubali kuhusika na tukio hilo na wenzake mtaa wa Lumumba.

Aidha, kamanda Kova amewataka wananchi kuunda vikundi vidogovidogo vya ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika maeneo yao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa sikukuu ambapo matukio ya ujambazi yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
 
...Mtu anafundishwa kutumia silaha, taifa likiwa halina uzalendo tena, viongozi wakiendekeza kujilimbikizia mali, ndugu na jamaa wakiwa hoi kwa umasikini. Unategemea nini?
 
Vetting of any applicants to our armies is so crucial. I believe if it were proper, such actions wouldnt occur! Mtu hawezi kuanza ujambazi ukubwani-never!...Ujomba na Ubinamu na madhara yake.
 
Back
Top Bottom