JK Ziarani Denmark

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Habari nilizonazo, JK yupo nchini Denmark kwa ziara ya kikazi, yeyote mwenye habari zaidi?
 
hehehe
mkuu kakosa usingizi kaamua kwenda barazani kupunga upepo kwanza.
 
Hivi huyu bwana kweli yuko serious na nchi hii? Wadanganyika tumekuwa mabwege kiasi hicho kwamba mtawala anaweza kuwa anatalii tu huku watu wanakufa njaa! Aibu ,tunashindwa na nchi ndogo kuliko sisi ya Malawi kutovumilia upuuzi wa namna hii. Rais gani huyu hatulii ofisini hata siku moja?
 
Raisi wa Tanzania ni Rostam Aziz. JK ni kama Queen wa England and Wales.
 
More than 19 kids are missing because of MLIPUKO WA MABOMU, Pinda is running around like kipepeo. Zee Comedy ndio huyo anakwenda kwa Wadenish I guess kuongelea msaada, baada ya hapo anampa hongera Mzee Zuma (aka mzee wa totos). All this is happening while 19 kids are still missing, and Mr. Lukuvi aka Boga head is just running around like a flower girl in the cousin wedding.

Kweli JK ni kama queen wa England.
 
Ndo mzee wa masafa huyo!!

Ila kweli pesa za safari za Raisi nje ya nchi kwa sasa ni nyingi kuliko wakati wowote!
 
Habari nilizonazo, JK yupo nchini Denmark kwa ziara ya kikazi, yeyote mwenye habari zaidi?

Hii ndio Tanzania, Ni kweli bwa JK yuko huko. Maafa ya Mbagala ameachiwa Lukuvi. Na inasemekana kuna Kaufisadi kameshaingia kwenye kutoa misaada.
 
8E9U8413kikwete_shangaa.JPG
JK akilakiwa na Malkia Magrethe wa pili.
 
Ni wadanganyika wenyewe siku wakiamka kutoka usingizini labda miaka 50 ijayo...
 
Hii ni Dondoo kutoka kwenye Barua ya Mjeshi Mstaafu kwa Rais Mteule Komredi Zuma:

"We plead with you Mr.President not to play the Foreign Minister, and spend more time solving African and global problems, while we pine for your presence in South Africa. Your stature in the world stage will be larger if everybody out there knows that you are solving the problems of the people of South Africa. Do not be like that township father who buys everybody a drink in a shebeen, while the wife and children have no food in the house."
 
Hivi tunapoongea mtikisiko wa kiuchumi na mambo ya kucut cost hawa watu wa serikali haiwahusu. Mimi nilitegemea wao ndio wangeonyesha mfano kwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.
Safari ya raisi na wapambe wake ni gharama zaidi kuliko angeenda waziri wake wa mambo ya nje. kwanza hao mabalozi waliopelekwa kwenye hizo nchi wana kazi gani sasa kama kila mara MKUU lazima aonekane. Kwa mtazamo wangu sidhani kama hii ni sahihi.
Mabalozi wapo, Waziri wa mambo ya ndani yupo sasa hii yote ni kupoteza hela za walipa kodi (ambao siyo wajanja). Hii nchi kwa kweli inapoelekea sijui.
Tunaacha kuangalia mambo ya msingi eti tunasema tunaenda kuomba omba na pia kukumbushia ahadi walizotoa. Hii ni aibu.
Au kuna sababu nyingine inayomfanya MKUU asikae IKULU ambayo mimi na wewe hatuijui
 
Mh, jamani huenda kweli kuna ugali wa watoto anaenda kuuhangaikia! Siyo bure itakuwa ni majukumu ya nchi.
 
haaa wapi tangu lini? huyu anajisahau sana anafikiri bado anahold post ya foreign affairs...anafanya kazi za membe abadilishane nae basi lol....
 
Mh, jamani huenda kweli kuna ugali wa watoto anaenda kuuhangaikia! Siyo bure itakuwa ni majukumu ya nchi.

Kazi ya waziri wa mambo ya nje ni nini? Basi angeamua kuchukua pia ni wizara ya mambo ya nje. Nchi nyingine hilo limefanyika mfano Rais anakuwa pia waziri wa ulinzi au waziri wa mambo ya ndani.

Ila tusimlaumu sana, utamu wa kusafiri anaujua hasa baada ya kukaa kwenye hiyo wizara kwa miaka kumi mfululizo
 
Tumeshachoka na ziara za huyu mtalii wetu anazozifanya kila siku.
Sisi hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada.
Hivi ni nchi gani imeendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi hisani??
Kazi ndio msingi wa maendeleo. Tuboreshe viwanda vyetu na tukuze kilimo chetu.
Tusitegemee soko la nje, tukuze soko la ndani ndipo tutaweza kula neema ya nchi.
 
Kazi ya membe ni hipi coz naona kama JK kamzidi flyer miles!! Au hataki membe ajenge connections nje??
 
Back
Top Bottom