JK wakati umefika hata hivyo hujachelewa!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,577
8,596
Nilisikiliza jana maelezo ya JK kuhusu bomoabomoa nikweli hapa JK Umewagusa wengi kwani ubabe uliokuwa ukifanywa na Serikali juu ya Bomobomoa niwakutisha bila kujali wewe hicho kibanda umekipataje na imekuchukua mda gani mpaka ukakisimamisha na wakati mwingine Hiyo miundombinu imewakuta lakini kwakuwa imepewa jina la Barabara ya TanRoad basi wewe unakosa unapewa 48hrs uwe umeamisha kifusi chako!
Tumeona akina mama wakilia hadi kuvua nguo hadharani kwakuwalaani TanRoad!!Hapa JK umesema na wananchi katika Mioyo yako na wamekusikia ziara kama hizi ziwenatija ikibidi wengine wanaofanya Madudu waweke ndani wakati wakuoneana haya umeisha Wewe ni Rais wa JMT!
 
mpiga debe
 
Mimi nauliza kile KITI anachokalia wakati anaongea na watendaji wa wizara mbalimbali anazotembelea sasa anahama nacho au kila wizara imemtengenezea kiti cha aina ileile? Ni kwa ajili ya lile tatizo lake la pingili za uti wa mgongo? Kwa kweli JK wetu amedhoofu sana kwa sasa angepumzika tu ingawa pumzi bado anayo.
 
Kwa mtu asiyejua dhana dhana ya uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) anaweza akampongeza JK kwa kumfokea Waziri wake hadharani. Lakini kwa mtu makini JK kafanya kosa la karne na nafikiri utawala wake anazidi kuutia doa. Haiyumkiniki mradi mkubwa kama huu wa kutengeneza barabara za kupita mabasi yaendayo kwa kasi kuwa haukujadiliwa ktk vikao mwafaka na kwamba ili uanze inabidi kuondoa majengo na vitu vilivyoingia barabarani. Mradi kama huu unahitaji upembuzi yakinifu kutoka ngazi ya wizara moja mpaka Barza la mawaziri ambalo JK ndio mwenyekiti wake. Kama Magufuri alikosea kwa kuamuru kuvunja nyumba njia mwafaka ilikuwa ni kumwita katika vikao rasmi na kumwambia asitishe au atafute njia nyingine.Lakini kukurupuka kwa kumkjeli tena ktk jimbo lake la uchaguzi la kumshindilia msumari ktk wizara yake sio kitendo kizuri ktk medani ya uongozi. JK na Pinda naona wanatakiwa wapewe darasa la dhana uongozi na uwajibikaji ili waache kuishi kama watu wa kijiweni.Kama wanafikiri kumshushua waziri hadharani ndio mtaji kisiasa wenye akili hawaoni hivyo ila wanaona ndio anguko la serikali isiyojifunza bali ya kisanii
 
Mimi nauliza kile KITI anachokalia wakati anaongea na watendaji wa wizara mbalimbali anazotembelea sasa anahama nacho au kila wizara imemtengenezea kiti cha aina ileile? Ni kwa ajili ya lile tatizo lake la pingili za uti wa mgongo? Kwa kweli JK wetu amedhoofu sana kwa sasa angepumzika tu ingawa pumzi bado anayo.

Si unaona sura ilivyomshuka? Huyu jamaa ni mgonjwa, yaani pamoja na Loliondo yuko vile,kabla ya kupata kikombe alikuwaje? Tumhurumie mkulu wetu, hata kushindwa kuchukua maamuzi magumu si hiari yake ni maradhi tu yamefika utosini.
 
Sio kwamba he feels for the people; rather he is looking for ways to get a bit of public acclamation maana maji yamemzidia
 
Tatizo la wanasiasa wa Tz including Jk na Mawaziri wake hawapo organized kiasi kwamba kila mtu anamaamuzi yake
 
jk keshaharibu sana kupitia watendaji wake sasa anatumia migongo ya hao watendaji kjuiinua tena. Sikupenda namna alivyoingilia hotuba ya Prof Tibaijuka.
 
na penye ukweli lazima tuuseme jamani kwa hili mkwere amejitahidi kilichobaki ni kusimamia statements zake in actions...
 
jk keshaharibu sana kupitia watendaji wake sasa anatumia migongo ya hao watendaji kjuiinua tena. Sikupenda namna alivyoingilia hotuba ya Prof Tibaijuka.

Bora ile ya Tibaijuka,ile ya Magufuli ndo kabisaa aliharibu kila kitu.....halafu hakuna la maana analochomekea,mradi ajionyeshe tu kwamba yeye ndo rais....he seems inferior though and weak!!:juggle:
 
Sio kwamba he feels for the people; rather he is looking for ways to get a bit of public acclamation maana maji yamemzidia
JK anachukiwa na mtu kama wewe hasa nyinyi waifia dini. Lakini kiuhalisia bado jamaa yupo sawa tu na watangulizi wake na si ajabu amewazidi kidogo. weka imani yako na ubinafsi wako bembeni halafu umjaji. then you will know what I mean.
 
Ndiyo maana siku zote nasema JK ndiye mwasisi wa siasa za udini kwa sababu watetezi wake siku zote wanajificha kwenye blanketi la udini, watu wakigusa perfomance ya JK wapambe wana kimbilia dini kwa nini?
 
Mimi nauliza kile KITI anachokalia wakati anaongea na watendaji wa wizara mbalimbali anazotembelea sasa anahama nacho au kila wizara imemtengenezea kiti cha aina ileile? Ni kwa ajili ya lile tatizo lake la pingili za uti wa mgongo? Kwa kweli JK wetu amedhoofu sana kwa sasa angepumzika tu ingawa pumzi bado anayo.

Da! maswali mengine bana!
swali la nyongeza, je hawezi kukalia kiti cha aina nyingine zaidi ya kile?
 
Akifanya kizuri mkubali tu kwani Mgufuli alikuwa anaenda vibaya, japo kumsemea hadharani si vizuri. Jiweke kwenye nafasi ya wanaobomolewa ndio utaonda umuhimu wa Rais kuingilia kati kwani kuna wengi wamepata magonjwa ya moyo pamoja na pressure kwa sababu ya ya kupewa 48hrs kubomoa nyumba pekee waliyonayo hapa duniani bila compasation
 
Nyumba zitavunjwa tu siku moja na amini maneno yangu, Kariakoo, kuna siku nayo itakwenda na maji hasa barabara ya UHURU ili kuruhusu barabara ya walau lane 4.

Usafiri si swala la mchezo na kitu pekee kinachoweza kusaidia ni kuhamisha mji mkuu Dodoma na Dar City kuhamishiwa maeneo kama Kigamboni au mbali zaidi ambako kutakuwa ni rahisi mji kupanuka pande zote nne. Nusu ya mji wa Dar ni Bahari.....

Ufaransa ilivunja nyumba ili kupanua barabara. Nchi nyingine zilisaidiwa na majeshi ya Hitler kwa kuvunja miji hiyo na walipokuwa wakipanga miji upya, walianza kwa kuweka barabara PANA sanaa kama Highway vile na hii imesaidia baadaye wapitishie Trams na Metro chini yake na au Matrain ya juu kama ilivyo Berlin.
 
Back
Top Bottom