JK: UVCCM inavurugwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
JK: UVCCM inavurugwa

Martha Mtangoo, Dodoma
Daily News; Sunday,December 14, 2008


MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewaonya watu maarufu walio nje na ndani ya chama hicho, kuacha kujiingiza katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) na kuwashinikiza wajumbe wachague watu wanaowataka kwa maslahi yao binafsi.

Akifungua Mkutano Mkuu wa UVCCM mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema uchaguzi wa UVCCM mara zote umekuwa na vurugu kutokana na watu walio nje ya umoja huo, kujiingiza na kuwaweka watu wao na kushinikiza wachaguliwe, jambo linalosababisha ugomvi mkubwa katika chaguzi za jumuiya hiyo.

Alisema baadhi ya watu hao si vijana na umri wao umeenda na si wanachama wa umoja huo na ambao hawafanani na vijana, wamekuwa wakijiingiza katika chaguzi, jambo ambalo alisema ni baya na ni kosa.

"It's a crime (ni uhalifu), ni mbaya sana kujiingiza katika masuala ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakati we si kijana wala mwanachama, hii ni mbaya. Ni lazima kujiuliza huyu Kikwete yuko nje ya uanachama, lakini anaweka mtu wake kwenye nafasi ya uongozi na anataka ashinde, anataka nini huyu?" alihoji Rais Kikwete.

Aliwaonya wazee kuacha kujiingiza katika mambo ya vijana kwa kuwa ili demokrasia itumike katika uchaguzi huo, ni lazima wajumbe waachwe huru kuchagua viongozi wanaowataka na wanaowaona wanafaa kuwaongoza na si vinginevyo.

Alisema kinachompa taabu ndani ya UVCCM ni watu ambao si wajumbe kujiingiza na kuwataka wajumbe wasiwapatie kura na watu hao ambao wamekuwa wakitoa takrima ili watu wao wachaguliwe kwa maslahi yao binafsi.

Aliwataka wajumbe kuwakataa wote ambao wamekuwa wakitoa takrima na zawadi mbalimbali na wenye kutoa ahadi za kuwa iwapo watachaguliwa watawapatia nafasi fulani ili kuwaonyesha kuwa uongozi haununuliwi.

Alisema wajumbe wanayo haki ya kumjadili mgombea na kufanya hivyo kwa wajumbe ni haki yao ila kufanya hivyo kwa mtu ambaye si mjumbe wala mwanachama wa UVCCM, si haki wala si halali kwa kuwa kufanya hivyo ni kuharibu jumuiya na kinachotakiwa kufanyika katika uchaguzi ni kuiacha demokrasia kufanya kazi yake.

Aliwaeleza wajumbe hao kuwa hajawahi kujiingiza katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana hata siku moja na iwapo vijana watawakataa viongozi wapenda rushwa, watakuwa wanatekeleza mambo ya Umoja wa Vijana wa CCM anaoujua yeye. Alisema tabia ya watu hao wanaojiingiza katika umoja huo inakipeleka chama mahali pabaya kwa kuwa mwelekeo huo si wenyewe, na ukiendelea siku za usoni hatima ya chama itakuwa mbaya na kuongeza kuwa maradhi hayo yasiwafikie vijana.

Aliwataka vijana hao kukataa kutumiwa na watu na wasiwe vivuli vya watu na wanachotakiwa ni kuwa na vivuli vya chama au jumuiya na si kivuli cha mtu binafsi kwa kuwa wakifanya hivyo, watayumba na hawatakuwa viongozi bora ndani ya CCM.

"Nawasihi vijana mtakaochaguliwa kuwa viongozi, msirithi maadui wa wenzenu na badala yake mrithi marafiki wao na katika kurithi marafiki ni lazima muwe makini sana maana unaweza kurithi rafiki wa mwenzio kumbe hampendi mtu fulani," alisisitiza. Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika jana usiku.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi aliwaasa wanachama kujiamini katika uongozi na wasiwe na kigugumizi kwa kuwa yeyote ambaye hajiamini hafai kuwa kiongozi.

Alisema katika siku zake zote za uongozi wake, hakuwahi kuwa na kigugumizi na ndio maana ameifikisha UVCCM hapo ilipo sasa. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo pia vyama sita rafiki kutoka nchi za Afrika vilihudhuria mkutano huo.
 
By the way nasikia Beno Malisa kashinda umakamu mwenyekiti, kuna mwenye taarifa wadau? Tujuzane
 
Maneno matupu hayalambwi ndugu yangu.Rais Kikwete anahusika moja kwa moja na kuvurugwa kwa UVCCM,kwa vile hajachukuwa nafasi yake kama raisi ya kuleta uwajibikaji sehemu za kazi.Anastahili lawama zote.
 
Hivi si Kikwete huyuhuyu alishangilia wakati Somaiya alipoipata UVCCM milioni 400!!! sasa leo analalamika nini tena?
 
Back
Top Bottom