Jk Usiwalaum Maaskofu Kuhimiza Kura Ya Hapana, Jilaum Kwa Kushikiza Kura Kura Ya Ndio

Majuto Ngozi

JF-Expert Member
Jun 18, 2013
211
49
Hivi Karibuni Rais Kikwete Alikaririwa Akiwalaum Viongozi Wa Dini Kwa Kuwataka Waumini Wao Kuipigia Kura Ya Hapana Katiba Inayopendekezwa, Lakini Kikwete Huyu huyu Tangu Siku Ya Kuzindua Bunge Maalum La Katiba Alishadadia Na Na Kuikosoa Katiba Iliyotolewa Na Tume, Lakini Pia Yupo Mstari Wa Mbele Kuashinikiza Wananchi Kuipigia Kura Ya Ndio, Kwani Yeye Ana Haki Hiyo Kuliko Wengine?
 
Ndugu Umetoa hoja?maoni?ushauri au umeuliza swali??? maana hueleweki!!! kwani wewe unataka tukusaidie nini?
 
Hivi Karibuni Rais Kikwete Alikaririwa Akiwalaum Viongozi Wa Dini Kwa Kuwataka Waumini Wao Kuipigia Kura Ya Hapana Katiba Inayopendekezwa, Lakini Kikwete Huyu huyu Tangu Siku Ya Kuzindua Bunge Maalum La Katiba Alishadadia Na Na Kuikosoa Katiba Iliyotolewa Na Tume, Lakini Pia Yupo Mstari Wa Mbele Kuashinikiza Wananchi Kuipigia Kura Ya Ndio, Kwani Yeye Ana Haki Hiyo Kuliko Wengine?

Siku ya kuzindua Bunge Maalum la Katiba Rais alikosoa Maoni yaliyoandikwa kwenye Rasimu ya Pili ya Tume na siyo Katiba Inayopendekezwa, Katiba Inayopendekezwa imeandaliwa na Bunge Maalum baada ya kuifanyia maboresho Rasimu hiyo. Ndiyo maana Rais naye alitoa maoni yake kuhusu baadhi ya vipengele.

Watu mnamatatizo kweli, Rais akisema mnasema yupo mstari wa mbele, asiposema mnsema yupo kimya. Mnamatatizo gani? Nakubaliana na msemo wa mabadiliko ni lazima yaanze na mtu mwenyewe. Aliyeanisha mchakato ni lazima awe wa kwanza kuhamasisha wengine wamuunge mkono. Tutumie fursa tuliyopewa na NEC kuisoma Katiba Inayopendekezwa vizuri kwa manufaa yetu na taifa na hasa tuilewe katiba hiyo maana itakuwa ndiyo sehemu yetu ya maisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom