JK unapotoa rambirambi kwa kanumba 10,000,000/= je wazee wa EAC utwalipa lini mafao yao?

hivi wale wazee kosa lao nini mpaka sasa hawajalipwa? dhambi gani walitenda mpaka RITZ anawabeza?
Wale wazee walishalipwa kitambo. tatizo lao hawakuridhika na pesa walizolipwa. Matokeo yake kila wakisikia njaa wanadai serikali hela. Offcourse watanzania wengi wako hivyo. Dili lolote na serikali iwe kupisha upanuzi wa barabara au ujenzi wa shule hata siku moja hawaridhiki na kiasi wanachopewa na uendelea kulalamika tu, wakidai serikali iliwapunja.
 
aisee 10 m? kazi kweli kweli, kuna kigezo chochote? maana Rais ni institution thus hiyo 10 m imetolewa na taasisi ya urais, haya bandugu tutafika......na ni yale yalemarehemu angesaidiwa hiyo 10m wakati wa uhai wake angeweza kuifanyia makuu.........kafa inatoka 10, je kwa wasanii wote itakuwa vivyo hivyo?
 
Kuna kosa gani Kikwete kuwakumbuka wasanii wenzake? Kama mambo serious yamemshinda jamani ashindwe na usanii? Hii ndiyo Bongo ambako kila mtu ni bongolala kiasi cha kuifanya bongolaland. Nyie mnadhani wakubwa wanakwenda misibani kwa sababu ya mapenzi kwa marehemu au kutumia fursa kujijenga kisiasa. Umaarufu haujengwi kwa matofali bali sarakasi na sanaa. Ama kweli Kikwete ni msanii. Ila tuwe wakweli. He has lost direction so as not to know what to do how, when and why. Kanumba amewavuta Kikwete, Salma, Riz na bado Halfani yule junior maarufu wa ukoo wa mfalme Jakaya. Mnataka mliwe vipi na mara ngapi wabongo jamani?
 
kutoa salam za rambi rambi kwa msanii maarufu kanumba sio nongwa lakini swali kama hizo rambi rambi tangu anze kutoa wakati wa utawala wake, je hakijafika kiwango cha kuwalipa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki kama zingekokotolewa hizo rambi rambi?

Complain complain complain! Ni hilo moja tu umeona ndugu? Hebu fikiria kila jambo na wakati wake na ufunguke sasa, kesi ya wazee wa EAC ipo mahakamani siyo, unafikiri wakishinda na kuamliwa walipwe haitawezekana! Well, scarcity mentality vs Abundant mentality. Na wengine woooote wenye madai yao, je, ungependa walipwe na fedha binafsi za kikwete? Too critical is too desperate and the the desperate are loosers always!
 
Wale wazee walishalipwa kitambo. tatizo lao hawakuridhika na pesa walizolipwa. Matokeo yake kila wakisikia njaa wanadai serikali hela.

This is interesting, kama unayosema ni kweli, kwa nini serikali inashindwa kuwa jasiri na kusema moja kwa moja kwamba hatudaiwi? Mbona kila siku wanatoa ahadi za kumaliza tatizo ambalo in effect halipo?
 
Complain complain complain! Ni hilo moja tu umeona ndugu? Hebu fikiria kila jambo na wakati wake na ufunguke sasa, kesi ya wazee wa EAC ipo mahakamani siyo, unafikiri wakishinda na kuamliwa walipwe haitawezekana! Well, scarcity mentality vs Abundant mentality. Na wengine woooote wenye madai yao, je, ungependa walipwe na fedha binafsi za kikwete? Too critical is too desperate and the the desperate are loosers always!

Hapo kwenye bold unaweza kufanunua kidogo, kwa sababu vitu anavyotoa na kupokea rais vina taratibu zake za tofauti sana. Hii ni pesa yake ya mfukoni mwa JK au ni pesa ya rais (taasisi)?
 
kutoa salam za rambi rambi kwa msanii maarufu kanumba sio nongwa lakini swali kama hizo rambi rambi tangu anze kutoa wakati wa utawala wake, je hakijafika kiwango cha kuwalipa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki kama zingekokotolewa hizo rambi rambi?

mara nyingi watu husahau kuwa mwenye shibe hamjui mwenye njaa! Kuna wazee Ea, wazee wale wa ukoma Tabora/shinyanga, morogoro wanahitaji kiasi cha chini ya shs million 100 tu, ili wafarijike na kujiona na Watz. Lakini viongozi wetu na wenye hela zao hatuwaoni hao, kwa vile kamela za video hazitatuonyesha.
 
Babu yako nae mstaafu nini manake ulivyokomalia sio bure.Ushauri nenda kawambie wakagawane na ndugu wa kanumba.La sivyo watasubiri sana
 
kutoa salam za rambi rambi kwa msanii maarufu kanumba sio nongwa lakini swali kama hizo rambi rambi tangu anze kutoa wakati wa utawala wake, je hakijafika kiwango cha kuwalipa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki kama zingekokotolewa hizo rambi rambi?

Rais hawezi kuacha kushiriki maswala ya kijamii, kisa eti Serikali inadaiwa. Hebu tuwe tunatafakari mambo mengine kabla ya kutoa michango humu JF. Kama Chama kinaweza kutoa Rambirambi wakati huo huo kinapitisha bakuli la kuomba kichangiwe pesa za kambeni tena toka kwa wazee hao hao wa East Afrika, Serikali ndiyo itashindwa? Hata hivyo suala la wazee wa East Africa lilishashughulikiwa na wanachosubiri ni malipo yao.
 
mara nyingi watu husahau kuwa mwenye shibe hamjui mwenye njaa! Kuna wazee Ea, wazee wale wa ukoma Tabora/shinyanga, morogoro wanahitaji kiasi cha chini ya shs million 100 tu, ili wafarijike na kujiona na Watz. Lakini viongozi wetu na wenye hela zao hatuwaoni hao, kwa vile kamela za video hazitatuonyesha.

Kwa akili yangu naona kama watu wanaolaumu Rais kutoa rambirambi kwenye msiba wa Kanumba ni kama wamefurahishwa sana kifo cha Mpendwa wetu vile, siamini kama suala la rambirambi linaweza kuwa issue kwa binadamu aliyehai na ambaye ni marehemu mtarajiwa! Mungu atuepushe na mioyo hii ya ajabu.
 
Hapo kwenye bold unaweza kufanunua kidogo, kwa sababu vitu anavyotoa na kupokea rais vina taratibu zake za tofauti sana. Hii ni pesa yake ya mfukoni mwa JK au ni pesa ya rais (taasisi)?
Mimi nadhani ni kama fedha yake ya mfukoni kwa sababu sijadhani kuna kikao chochote kimekaa kumruhusu Rais atoe hiyo mil.10. Hapa ni suala la kuguswa na msiba wenyewe. Tusiingize hili nalo katika siasa, tunaonekana kama hatuwezi kutenganisha siasa na masuala ya kijamii. President JK is 100% perfect.
 
kutoa salam za rambi rambi kwa msanii maarufu kanumba sio nongwa lakini swali kama hizo rambi rambi tangu anze kutoa wakati wa utawala wake, je hakijafika kiwango cha kuwalipa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki kama zingekokotolewa hizo rambi rambi?

Mkuu hizo si zimetoka mfukoni mwake kaamua kujitolea? Na sidhani kama mtu unaweza kuishi ndani ya jamii hasa ya kiTz uache kutoa michango kama hii yafaa mtu kabla ya kuweka post hapa uwe makini na kufikiria kwa kina
 
Kuna kosa gani Kikwete kuwakumbuka wasanii wenzake? Kama mambo serious yamemshinda jamani ashindwe na usanii? Hii ndiyo Bongo ambako kila mtu ni bongolala kiasi cha kuifanya bongolaland. Nyie mnadhani wakubwa wanakwenda misibani kwa sababu ya mapenzi kwa marehemu au kutumia fursa kujijenga kisiasa. Umaarufu haujengwi kwa matofali bali sarakasi na sanaa. Ama kweli Kikwete ni msanii. Ila tuwe wakweli. He has lost direction so as not to know what to do how, when and why. Kanumba amewavuta Kikwete, Salma, Riz na bado Halfani yule junior maarufu wa ukoo wa mfalme Jakaya. Mnataka mliwe vipi na mara ngapi wabongo jamani?

Mwanasiasa wa kwanza kufika kwenye msiba wa Kanumba alikuwa JOHN MNYIKA, alikwenda kujijenga kiasiasa? Hili ni suala la mtu kuguswa bhana, ila sishangali wengine kitu utu is zero na ndiyo maana unaingiza matusi hata kwenye mambo serious. Huwezi kumuita Rais msanii, inaonekana ni jinsi gani hata familia yako inaku-ignore bro. Ndyo wale wale mnaowaita baba zenu DINDI na majina mengine mengine kama hayo wakati hujui maana halisi ya neno lenyewe.
 
Kwani JK ndiye aliyewaajiri wazee wa EAC?

Hao wazee wanadai toka enzi za Mwinyi akaondoka, akaja Mkapa akaondoka baada ya kuwalipa pesa kiduchu na sasa Jk ambaye bado hajamaliza muda wake. So give him a break...come with something more concrete.

siku mjema huonekana asubuhi nadhani kwa mtu mwelewa ashaliona hilo kuwa uwezekano wa kulipwa kwa hawa wazee haupo kabisa
 
Mkuu hizo si zimetoka mfukoni mwake kaamua kujitolea? Na sidhani kama mtu unaweza kuishi ndani ya jamii hasa ya kiTz uache kutoa michango kama hii yafaa mtu kabla ya kuweka post hapa uwe makini na kufikiria kwa kina

Safi sana mkuu. Ila unajua watu kama lubada hawaishi na jamii karibu angeweza kuliona kama jambo la kawaida. Hawa ndiyo wale wale shule "SCHOOL BUS", kazi ANASHIKILWA hadi kwa Ofisi, so he/she doesn't know what happen in the society. Tumuache bhana.
 
Kwa akili yangu naona kama watu wanaolaumu Rais kutoa rambirambi kwenye msiba wa Kanumba ni kama wamefurahishwa sana kifo cha Mpendwa wetu vile, siamini kama suala la rambirambi linaweza kuwa issue kwa binadamu aliyehai na ambaye ni marehemu mtarajiwa! Mungu atuepushe na mioyo hii ya ajabu.

Nafikiri wengi wameikosa point kubwa kwenye hii mada. Wengi wetu hatuna problem ya pesa aliyotoa ya rambirambi kwenye kilio cha huyu artist wetu - whether imetoka mfukoni kwake au kwenye mfuko wa ofisi ya Raisi. Problem ambayo personally naiona ni ile kwamba kwenye kilio cha mtumishi wa umma wa miaka mingi sana hakuhudhuria na viongozi wahusika kama IGP wa sasa hawakuonekana, halafu anaonekana leo kuhusika sana na kilio cha mtanzania mwingine ambaye pamoja na contribution yake kubwa kwenye culture yetu, hawezi kuwa muhimu kwa taifa kuliko mkuu wa polisi. Wale wanaosema ni wivu wanakuwa tu wavivu wa fikra na kama mwenzangu alivyosema hapo juu, watakapoketi chini na kuwaza vizuri wataona kuwa si sawa alivyofanya kiongozi wetu. And this has nothing to do with the money!!
 
Kuna kosa gani Kikwete kuwakumbuka wasanii wenzake? Kama mambo serious yamemshinda jamani ashindwe na usanii? Hii ndiyo Bongo ambako kila mtu ni bongolala kiasi cha kuifanya bongolaland. Nyie mnadhani wakubwa wanakwenda misibani kwa sababu ya mapenzi kwa marehemu au kutumia fursa kujijenga kisiasa. Umaarufu haujengwi kwa matofali bali sarakasi na sanaa. Ama kweli Kikwete ni msanii. Ila tuwe wakweli. He has lost direction so as not to know what to do how, when and why. Kanumba amewavuta Kikwete, Salma, Riz na bado Halfani yule junior maarufu wa ukoo wa mfalme Jakaya. Mnataka mliwe vipi na mara ngapi wabongo jamani?

jamani hata public ilivyoupokea msiba wa kanumba ni tofauti na ilivyoupokea msiba wa mahundi au mzee kipara. kikwete & family wameakisi feelings za wengi.
 
swala la hao wazee achane nao walishafanywa kama watoto ikirabia uchaguzi wanakua wazee wa ccm wanaitwa diamond jublee na rais wanatia maneno tele na kuongopewa, ya kwamba ooh tutakupatieni pesa zenu na nini mwisho wa cku wanaipigia ccm,wakiandamana wanapigwa virungu wazee wazima so kwa hilo acha serikali ya ccm na kikwete wao awafanye anavyotaka nahilo la sh. m10 jk kapotoka.
 
Back
Top Bottom