JK tulia kidogo nchini: Meli inapigwa mawimbi!!!

jairo alikuwa anafanya kazi za CCM au kazi za serikali . Mwenzae PM wa UK issue ya gazeti imefanaya tu akatishe safari. Yeye issue ya katibu mkuu wake kutoa rushwa tena kwa wabunge anaona powaaa tu.

Siku moja moja kuwa sensible

Huyo ndie Rais anaejiamini.
 
Mkuu wangu JK, Meli yako inayoitwa Tanzania inaelekea iko kwenye mawimbi ya kati hadi mazito kidogo.
Kwa sisiwadau wako tunaona ni kwa sababu nahodha uliyemuachia usukani ukiwa katika ziara zako nyingi nje ya nchi naye anayumba na Meli hiyo.
Yanayoniskitisha zaidi ni Serikali kukosa muelekeo hasa wakati huu wa Bunge.
Rushwa ya David Jairo imetushitua sana na imebidi ikusubiri kimaamuzi.

Kushitakiwa Chenge imekuwa wimbo wa itakuwa au haitakuwa, Serikali haina maamuzi ya kujionyesha iko safi.
Kwenye chama nako mambo si shwari, Sitta na Guninita wanaparurana hadharani.

Mzee mzima Rostama kaachia ngazi, hakuna wa kucomment rasmi juu ya kuvua gamba

Sie tuna uhakika Meli haizami, lakini dhoruba wananchi wanayoipata inawatia wasiwasi juu ya umahiri wa Nahodha.
Naomba tulia kidogo nchini mawimbi yaweze kutulizwa Mkuu wangu
sema ukweli tu bila chenga.......... mwambie nchi imemshinda, sio unazungukazunguka kama pia
 
Broda , kuelewa hayo uliyoainisha inataka Hikma, kitu ambacho kwa huyo ****** 'Meti-Onyo', yaani hamna kitu!
Anaongea BBC kuwa shida ya umeme Tz inaletwa na ukame, wakati anajua wazi watu wanahongana billions ili kuliua Taifa kupitia bajeti ya Wizara ya Nishati!
Anachekelea hata hayo, anashindwa kuamua, wakati anayo full-support ya Bunge lote na Wananchi wote!
My Hairs!

kaka tafadhali rejea hapo kwenye red.

mimi simo pliz.
 
Chama tawala kinaunda serikali na kinaongoza nchi.Si lazima uchangie kama huna la kuchangia,unajaza post zisizo na hoja na unasababisha urefu wa thread na wengine wanaweza kukata tamaa kusoma hata kama thread ina make sense.Tulia unawashwa mno.Aagh.

Na Rostam alietajwa kwenye hiyo post ya mwanzo ana cheo kipi Serikalini?

Msulubuni Mbowe kwanza aliyeingia muafaka na Pinda. Mbona wote mpo kimya na mnajaribu kuwaonea madiwani lakini mmemkuta Malla ngangari, kawagomea, hapo sasa. Kabla hujatazama la mwenzako kwanza tazama lako, au hulioni? Unanchekesha! Na Shibuda nae? mko kimyaaa hata baada ya kuwanyambua bungeni na hansard zipo!
 
Akija atadai hana habari kuwa Tanzania kuna mgao wa umeme,au kuna njaa,au uchumi mbovu,au vitu bei juu maana huwa hashindi nchini,so hamuwezi kumlaumu jamani,dah jamaa mjanja kinyama,cjapata ona!
 
Sitashangaa endapo hawata wawajibisha waziri na naibu wake ngeleja au kusema jairo alikua sahii kwani hayo ndo maamuzi yao tuliyoyazoea
 
Mkuu wangu JK, Meli yako inayoitwa Tanzania inaelekea iko kwenye mawimbi ya kati hadi mazito kidogo.Kwa sisiwadau wako tunaona ni kwa sababu nahodha uliyemuachia usukani ukiwa katika ziara zako nyingi nje ya nchi naye anayumba na Meli hiyo.Yanayoniskitisha zaidi ni Serikali kukosa muelekeo hasa wakati huu wa Bunge.Rushwa ya David Jairo imetushitua sana na imebidi ikusubiri kimaamuzi.Kushitakiwa Chenge imekuwa wimbo wa itakuwa au haitakuwa, Serikali haina maamuzi ya kujionyesha iko safi.Kwenye chama nako mambo si shwari, Sitta na Guninita wanaparurana hadharani.Mzee mzima Rostama kaachia ngazi, hakuna wa kucomment rasmi juu ya kuvua gamba Sie tuna uhakika Meli haizami, lakini dhoruba wananchi wanayoipata inawatia wasiwasi juu ya umahiri wa Nahodha.Naomba tulia kidogo nchini mawimbi yaweze kutulizwa Mkuu wangu
Yeye mwenyewe ni wimbi tosha hata akitulia nchini meli itayumba tu
 
kaka tafadhali rejea hapo kwenye red.mimi simo pliz.
Mkuu hujamwelewa anachosema, support aliyonayo M.kwere ni kuhusu ishu ya Jairo. Bungeni wamekomaa na raia tumekomaa kwaiyo kwa Mkwe.re kuamua ni kama kumsukuma mlevi vile. Akiamua kumtimua na kumpeleka mahakamani hatalaumiwa na Bunge wala wananchi ndo mana anasema tunamsapoti.
 
sema ukweli tu bila chenga.......... mwambie nchi imemshinda, sio unazungukazunguka kama pia
It is clear JK is walking a tight rope kati ya kutowawatimua marafiki zake wa "mtandao" na kudumisha mshikamano na dira ya chama tawala.
So far he has played an admirable game.
Lakini watendaji serikalini wako confused kutokana na stance hii.
PM Pinda anauogopa mtandao kama ukoma
Ni ajabu kuwa suala lililowazi la RUSHWA inabidi lisubiri uamuzi wa Rais amabaye wakati huo yuko nje ya nchi.
Hii ni kudhihirisha kuwa serikali iko kwenye GANZI as far as utendaji is concerned.
Ni wazi kuwa watendaji wa chama na srikali hawana confidence kutokana na msimamo wa mkuu wao.
Na ndio maana namhimiza JK kukohoa , tena kidogo tu. ili watu hawa wapate bearing ya kufanya kazi.
 
Na Rostam alietajwa kwenye hiyo post ya mwanzo ana cheo kipi Serikalini?
Nimeona post ya mdau hapo juu kwamba bila kufikiri utapost mambo ambayo ni ya kujaza tu idadi ya posti zako.
Jiulize kama Rostam hayuko serikalini ilikuwaje akahusika kwa 100% katika sakata la Richmond.
Madame FaizaFox tafadhaki tax your brain into overdrive ili mambo mengine upate kuelewa.
 
Yeye mwenyewe ni wimbi tosha hata akitulia nchini meli itayumba tu
Naamini JK si wimbi hata kidogo, na anauwezo wa kuelekeza meli kule inako weza kuelekea.
Ana miaka minne ya kutengeneza legacy yake na kukumbukwa na vizazi vijavyo.
 
Msulubuni Mbowe kwanza aliyeingia muafaka na Pinda. Mbona wote mpo kimya na mnajaribu kuwaonea madiwani lakini mmemkuta Malla ngangari, kawagomea, hapo sasa. Kabla hujatazama la mwenzako kwanza tazama lako, au hulioni? Unanchekesha! Na Shibuda nae? mko kimyaaa hata baada ya kuwanyambua bungeni na hansard zipo!
Hebu tujibu kwanza bibie FaizaF, suala la RUSHWA inayotolewa na serikali, CDM inahusika vipi?
Usiwe kama nazi koroma, kwa unazi kwa sehemu tu ya chama chako.
THINK!!!!!!
 
Nimeona post ya mdau hapo juu kwamba bila kufikiri utapost mambo ambayo ni ya kujaza tu idadi ya posti zako.
Jiulize kama Rostam hayuko serikalini ilikuwaje akahusika kwa 100% katika sakata la Richmond.
Madame FaizaFox tafadhaki tax your brain into overdrive ili mambo mengine upate kuelewa.

Hiyo ni assumption yako, Rostam hakuhusika na Richmond kabisa tena na aliyehusika na Richmond yuko mahakamani kwa sasa, wacha kuchakachuwa please. Na Richmond ni shirika au Richmond imeshakuwa serikali? Unanshangaza kuwa ukweli unaujuwa lakini unaupindisha kwa faida ya nani? ya mawazo yako? Ama kweli , aliyesema uongo ukisemwa kila siku mwishowe watu huamini kuwa ni ukweli. Ukweli ubaki kuwa ukweli. Please.
 
Hebu tujibu kwanza bibie FaizaF, suala la RUSHWA inayotolewa na serikali, CDM inahusika vipi?
Usiwe kama nazi koroma, kwa unazi kwa sehemu tu ya chama chako.
THINK!!!!!!

Ikiwa kweli ni rushwa, basi huwezi kumtuhumu kila mmoja katika serikali au chama kuwa ni mla au mtoa rushwa, na yule aliyeitoa barua ya Jairo alitoka chama gani?

Mpaka hii leo kuna sakata la madiwani wa magwanda Arusha wametuhumiwa kula rushwa ili waingie muafaka na CCM, jee, ni kwanini alitumwa Marando akachunguze? na Jee, kama kweli hao madiwani wamekula rushwa, inamaana kuwa chadema nzima wala rushwa? Tafakari.
 
Naamini JK si wimbi hata kidogo, na anauwezo wa kuelekeza meli kule inako weza kuelekea.
Ana miaka minne ya kutengeneza legacy yake na kukumbukwa na vizazi vijavyo.

Ndugu yangu Lole Gwakisa,

JK hawezi kutengeneza legacy katika miaka 4 iliyobaki, ndani ya chama na serikalini pia. Tatizo linalomsumbua JK kwa sasa ni namna ya ku-defuse tension ndani ya chama chake. Kipindi hiki cha miaka 5 ya kuelekea 2015 ni kigumu sana na hasa kwa kuzingatia ule utaratibu ulioasisiwa na yeye JK na kundi lake la mtandao ambao walianzisha siasa za makundi na kuchafuana wakati wakiwa wananyemelea kiti cha Ikulu.

JK hana msimamo na kinachomyumbisha ni wana mtandao ambao wamegawanyika. Sasa hivi Lowassa ana kundi lake, Sitta ana kundi lake na Membe naye ana kundi lake. JK anawezaje ku-defuse tension ya makundi hayo? Kumbuka hao wote walishiriki kwa nguvu moja kumwingiza Ikulu. Je, ana ujasiri wa kuwaita na kuwakemea? Je, ana ujasiri wa kuwakataza wasiendeshe hizo harakati?

Kwenye post yako ya kwanza umeeleza minyukano ya Guninita vs Sitta. UVCCM walikuwa wanaparuana Arusha, imetafutwa suluhu ya muda ya kisanii lakini hakuna muafaka wa kudumu. UVCCM makao makuu umegawanyika, kila mtu anampigia upatu mgombea wake ndo maana kila kukicha utasikia Bashe kasema hiki, mara Matefu kasema kile, mara Gambo kasema hilo mara sijui nani wa Moshi kasema kile, mara sijui mjumbe gani wa mkoa wa Mara kasema hili.

Naomba usome makala hii hapa: Huyu anajua ndipo utaelewa kwanini JK anapata kigugumizi kuchukua maamuzi magumu. Tatizo ni makundi ya urais kwa ajili ya 2015 ambayo yameishaanza kutengenezwa kuanzia kwenye chama mpaka serikalini.
 
Naamini JK si wimbi hata kidogo, na anauwezo wa kuelekeza meli kule inako weza kuelekea.
Ana miaka minne ya kutengeneza legacy yake na kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Leo Gwakisa, Leo Gwakisa, Leo Gwakisa.........kweli una roho ngumu !
  • nina hakika ulipojiunga JF November 2008 ulikuta sakata la EPA, Kagoda, Richmond, Meremeta, Dowans, Tangold, IPTL, Rada, Kiwira na mengine mengi yako pale pale !
  • nina hakika ulipojiunga JF November 2008 ulikuta matatizo ya umeme, uzururaji wa Kikwete, utendaji mbovu wa serikali, ubabaishaji na usanii yako pale pale !
  • nina hakika ulipojiunga JF November 2008 ulikuta upepo, mawimbi na dhoruba zinazoipiga merikebu yetu hii Tanzania ndio zinaanza na hadi leo ndio zinazidi !
  • nina hakika ulipojiunga JF November 2008 uliamini kuwa JK ana uwezo wa kuelekeza meli kule inakoweza kuelekea (?) na kweli inaelekea huko inakoelekea !
Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza awamu ya kwanza ya Kikwete hukusita kumpigia kura mwaka 2010 na kumkabidhi tena usukani ingawa kila dalili ilionyesha kuwa hana uwezo. Nina usemi moja tu kwako nikimnukuu Jenerali Ulimwengu;
Acha kulalamika ovyo kwa kutendewa ovyo baada ya kuchagua ovyo.

Nakushangaa sana hayo madudu aliyoyakuta Kikwete akayashughulikia ipasavyo unayasuku,a kwake, hebu kuwa mkweli japo kidogo:

  • EPA = Tumeona wakati wa Kikwete fedha zikirudi na watu kufikishwa mahakamani na juzi tu wengine wamekula miaka.
  • Kagoda = Hii ilianza kwa Mkapa na umeshaambiwa Kimya, kuna mamo ya Taifa hata Slaa hawezi kuyauliza tena.
  • Richmond = Tumeona wakati wa Kikwete kwa mara ya kwanza Mpaka waziri mkuu kapigwa chini seuse wengine na Gire yuko mahakamani au hujui?
  • Meremeta = Suala liko bungeni na hilo unalijua kwa nini.
  • Dowans = Ilipogeuka kuwa Symbian wote kimyaaaaa.
  • Tangold, = Achana na hii kitu kabisa. Usiulize.
  • IPTL = Kesi juzi imekwisha na IPTL imeamuriwa na mahakama ifilisiwe au hujui?
  • Rada = Nadhani umeona Kikwete alivyoshughulikia haya madudu ya Mkapa, na unajuwa kinachoendelea, fedha yote inarudi.
  • Kiwira = Tayari Kikwete kisha ingia mkataba na wachina watazalisha 300MW kutokana na mkaa wa hapo, au hujui?
  • na mengine mengi yako pale pale != Kama yepi?
  • umeme = 145 MW Agrekko, 100 Symbian, 300 Kiwira, 100 Wind power, nikuongezee zingine? hizo tu zimepita 600MW za kuanzia mkoloni mpaka anapochukuwa Kikwete. Au ulitaka awe kama Alladin na taa ya ajabu? akiisuguwa umeme huo! ikiwa wote kabla yake iliwachukua zaidi ya miaka:

    40 Waingereza
    20 Nyerere
    10 Mwinyi
    10 Mkapa =
    Jumla Miaka 80 imewachukua Kuweka 600 MW.
  • uzururaji wa Kikwete = Si wabure, leo tanzania inawatalii mara tatu zaidi ya kabla ya Kikwete na wawekezaji kibao tu, mpaka kwa mara ya kwanza tunaona Hoteli ya Tanzania iliyopo Serengeti ikichaguliwa kuwa Hoteli bora duniani, unafikiri walikuja wenyewe wale kuwekeza bila efforts?
  • utendaji mbovu wa serikali = UN haikubaliani na wewe:
    [h=3]TANZANIA YAPATA TUZO YA UN KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII!![/h]
    021.jpg
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stephen Wassira Tuzo ya UN ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.
  • ubabaishaji na usanii yako pale pale = Upi huo uelezee tukujibu.
Point zako ya tatu na ya nne hazina mshiko ni pumba zako binafsi.
 
Nimewaza cha kusema lakini nahisi hasira inanizidi,wacha niondoke nisije nikachafua hewa!
 
Ndugu yangu Lole Gwakisa,

JK hawezi kutengeneza legacy katika miaka 4 iliyobaki, ndani ya chama na serikalini pia. Tatizo linalomsumbua JK kwa sasa ni namna ya ku-defuse tension ndani ya chama chake. Kipindi hiki cha miaka 5 ya kuelekea 2015 ni kigumu sana na hasa kwa kuzingatia ule utaratibu ulioasisiwa na yeye JK na kundi lake la mtandao ambao walianzisha siasa za makundi na kuchafuana wakati wakiwa wananyemelea kiti cha Ikulu.

JK hana msimamo na kinachomyumbisha ni wana mtandao ambao wamegawanyika. Sasa hivi Lowassa ana kundi lake, Sitta ana kundi lake na Membe naye ana kundi lake. JK anawezaje ku-defuse tension ya makundi hayo? Kumbuka hao wote walishiriki kwa nguvu moja kumwingiza Ikulu. Je, ana ujasiri wa kuwaita na kuwakemea? Je, ana ujasiri wa kuwakataza wasiendeshe hizo harakati?

Kwenye post yako ya kwanza umeeleza minyukano ya Guninita vs Sitta. UVCCM walikuwa wanaparuana Arusha, imetafutwa suluhu ya muda ya kisanii lakini hakuna muafaka wa kudumu. UVCCM makao makuu umegawanyika, kila mtu anampigia upatu mgombea wake ndo maana kila kukicha utasikia Bashe kasema hiki, mara Matefu kasema kile, mara Gambo kasema hilo mara sijui nani wa Moshi kasema kile, mara sijui mjumbe gani wa mkoa wa Mara kasema hili.

Naomba usome makala hii hapa: Huyu anajua ndipo utaelewa kwanini JK anapata kigugumizi kuchukua maamuzi magumu. Tatizo ni makundi ya urais kwa ajili ya 2015 ambayo yameishaanza kutengenezwa kuanzia kwenye chama mpaka serikalini.
Keil , nakubaliana kabisa na observation yako.
Katika maisha ya CCM sijawahi kukiona chama kikiwa so disjointed.
Namkumbuka Mzee Kawawa na kilio chake ch kila siku-"Mshikamano". Msikamano ambao leo haupo katika chama.
Sasa chama legelege, kama alivyosema Mwalimu , huunda Serikali legelege.Hilo limekumbushwa na kijana wa jana tu, Kafulila, na watu wakanuna kuambiwa ukweli.
Ukweli ndio huo, haihitaji macho kuona dalili zote za kuyumba meli iitwayo Tanzania.
Hata hivyo katika siasa , niaka 4 ni mingi sana.Na Jk akiyashika matatizo yaliyopo na kuyatatua , moja baada ya jingine, bado anaweza kuacha legacy ya kukumbukwa.
 
Back
Top Bottom