JK:Tuanze kukukumbusha ahadi ulizotoa 2005 Majimboni?

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
Umebaki mwaka mmoja tu Rais JK amalize muhula wake wa kwanza wa miaka 5 kuitumikia TZ kama mkuu wa nchi.Na bajeti ya mwaka huu ndiyo ya mwisho kusimamiwa kimalifu na Rais aliyepo madarakani kwani itamaliza kutumika mwakani July;miezi 3 tu kabla ya tz kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwingine.
Kinachonisikitisha ni kuwa Bajeti hii ya mwaka huu ya waziri mkulo imejaa"aya nyingi za kishetani",kama vile kutengwa bilion 34 za kusafiria viongozi wa nchi,billion 19 za chai na sambusa kwa viongozi wizarani,kufutwa kwa kodi kwenye mafuta ghafi bila kujali athari zake za wakulima hata nyumbani kwa Mkulo kijijini Kilosa na kauli mbinu ya kilimo kwanza huku kilimo kikitengewa asilimia 6 tu ya bajeti nzima,huku serikali ikiwa haijatenga pesa yeyote kwenye baadhi ya ahadi nyingi za JK alizozitoa kwenye majimbo mbali mbali wakati wa kampeni zake za uchaguzi mkuu mwaka 2005!
Sera iliyokuwepo angalau enzi za Nyerere ya kutimiza ahadi na kugawa maendeleo ndani ya majimbo bila matabaka ya sehemu wanazotoka wakuu wa vitengo wizarani au vigogo waliopo serikalini sasa hayapo,kila mkubwa amejiwekea msemo unaosomeka "kwangu kwanza yaje maendelo,kwa wengine baadae yatafuata"
Hali ya sasa ya kujipendelea waliopewa dhamana ya uwaziri inatisha,na kwa sababu mawaziri hao hawakumewa na bunge basi sasa wamegeuza kama ni katiba kujipendelea!Na huwa wala hawafikirii ahadi za mkuu wa nchi alizozitoa majimboni zilizomfanya achaguliwe.
Nani kasahau?Waziri wa zamani wa miundo mbinu mwenye kesi mahakamani ya kutumia vibaya madaraka yake mzee Basil Mramba alikuwa wa kwanza kuwafundisha mawaziri wenzake jinsi ya kupeleka keki kubwa ya tz kwenye jimbo lake,alipoipeleka asilimia kubwa ya bajeti ya wizara yake ya Ujenzi jimboni kwake Rombo.Nae Waziri wa maji kipindi hicho hicho mzee Stephen Wasira hakukawia,akapeleka bajeti yote ya wizara yake jimboni kwake Bunda!Sisi na nyie tukabaki kimywa bila ya kutekelezwa ahadi zetu na miaka ikazidi kuyoyoma.
Mwaka huu na bajeti hii ya Mkulo mambo yamekuwa yaleyale.Bagamoyo anapotoka mkuu wa nchi na waziri wa miundo mbinu Shukuru Kawambwa imetengewa pesa nyingi sana na hata barabara inayopitika ya Segera-Tanga nayo imepewa hela nyingi mno eti itanuliwe na kuwa barabara kuu yenye njia nne.Ikumbukwe kuwa barabara za miji kama ya Mpanda kule Sumbawanga,au Kipatimo-Rufiji huwa zinafungwa wakati wa masika.Je kwa nini itanuliwe barabara inayopitika misimu yote ya Segera na wala zisiwezeshwe barabara za Lindi,Manyara,Singida,Mtwara na zingine nyingi ambazo hazipitiki kabisa wakati wa mvua?Vipi kuhusu ahadi za majimbo mengine iliyotolea na mkuu wa nchi miaka zaidi ya minne iliyopita?
Pamoja na upendeleo huu wa wazi,lkn bunge letu bado halifanyi lolote kukemea na kukwamisha bajeti hizi,wanaogopa kufanya hivyo maana CCM huwa inawashughulikia kwenye uteuzi wa wabunge pindi bunge linapomaliza muda wake.Na wabunge wetu wengi wana amini kuwa hawawezi kurudi bungeni pindi CCM ikiwaacha;ni mawazo ya kiimla!
Labda sasa tuanze kukumbusha maendeleo kimajimbo,kila mtu pale alipo awe anamtuma mbunge wake amuulize waziri husika kuhusu ahadi za mkuu wa nchi enzi zile za maneno matamu ya "ari mpya,mpya nguvu mpya na TZ yenye neema inawezekana",nilikuwepo Kyela mwaka 2005,alipokuja mkuu wa nchi kwenye kampeni zake,tena tukijipanga mistari kwa masaa mengi kwenye uwanja wa mpira Mwakangale tukimsubir!
Akiwa Kyela,Jk alituhaidi kuwa ndani ya miaka 3 barabara ya kutoka Kyela mjini hadi kwenye fukwe za kisasa za Matema Beach itakuwa tayari imejengwa kwa kiwango cha lami,lkn hadi sasa mzee JK kabakiza mwaka 1 tu amalize muhula wake na kule Kyela hatujawahi kuona hata wapima ramani wa kuwezesha mradi huo uanze achilia mbali hata karandinga moja!
Je,ni kweli JK atatimiza ahadi yake kwa wapiga kura wa Kyela?barabara hii itajengwa lini?Mbona wizara husika hawasemi lolote kuhusu ahadi hii?Mbona bajeti ya mwisho ya JK kusimamiwa na yeye kabla ya uchaguzi mkuu mwingine mradi wa barabara ya Kyela-Matema haimo?Watz hasa wana Kyela tuzidi kuamini ahadi hii itatekelezwa?Sidhani kama ahadi hii ipo hata kwenye kumbukumbu zake maana sasa JK anaelekea kwenye maandaliz ya uchaguzi mkuu miezi si zaidi ya 15 ijayo.
Naam ni kuzidi kudai sasa maendeleo kwa kutumia kumbukumbu za majimbo ambayo JK alitembelea.Mtz popote ulipo nadhani ni busara kudai ahadi hizi zitekelezwe kwa nguvu ya umma za majimbo maana collectively effort ya kugeuza ahadi hizi ziwe zinaamuliwa na serikali kuu hazina dalili yeyote ya kufanikiwa maana mawaziri wetu sasa ni kama tu mnyama wa kufikirika "nguchiro"kwa tamaa za kujipendelea na tukumbuke uchaguzi mkuu ni mwakani na asipotelekeza ahadi hizi alizotuhaidi kwa kipindi hiki kilichobaki shime wote tumtandike kidemokrasia kwenye sanduku la kupigia kura.
 
Back
Top Bottom