JK: Takrima NGUMU kuikwepa

Rushwa ni adui iwa haki Mheshimiwa Rais wa Nchi ya Tanzania. Tunahitaji mtu anayechukia rushwa na tukimwangalia kwenye paji la uso wake tuone dalili hiyo ya kukataa na kukemea rushwa. Rais mwenye dhamana ndani ya nchi anathubutu kusema kuwa rushwa ni ngumu kuepukika.? Tumefikia huko kweli?
Wanajf huu ni wakati wa mabadilliko ya kweli. Tuchague viongozi wanaofaa na waenye kuchukia rushwa iliyobatizwa jina la takrima.
 
Kwa maana nyingine anasema sheria anayopigia debe hatekelezeki, kwa hiyo rushwa iendelee kama kawaida.....
 
Kwa maana nyingine anasema sheria anayopigia debe hatekelezeki, kwa hiyo rushwa iendelee kama kawaida.....

Anaandaa mazingira ya rushwa mapema ili baadae aje aseme nilisema takrima haikwepeki. shame
Sikuona mantiki ya kuifananisha mbege na takrima, ina maana mgeni akija kwako ukimpa kikombe cha chai au glass ya juice umemuhonga?
 
Katika kuthibitisha kauli yake hiyo Rais Kikwete alimtaka mmoja wa maaskofu wanaotoka Kanda ya Kaskazini kueleza endapo inawezakana kuwaita wazee wa mkoa huo bila kitochi.

Askofu huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alimjibu Kikwete "Kwa kweli hili haliwezekani. Hiyo ni sehemu ya maisha ya watu wa Kilimanjaro."


Baada ya jibu hilo la askofu, ukumbi mzima akiwa Rais Kikwete mwenyewe ulilipuka kwa kicheko na baadaye rais aliendelea kuzungumza na viongozi hao bila kusema nini kifanyanyike ili sheria hiyo iweze kutekelezeka maeneo kama hayo.


Kwa mujibu wa Rais Kikwete kabla ya kutungwa kwa Sheria hii mpya ya Gharama za Uchaguzi, hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kabla ya mtu kufikiria kugombea, alianza kufikiri kwanza jinsi ya kupata fedha za kununua watu ili wampitishe kwenye kura za maoni.

"Mwende mkawahubirie watu kuwa wawachague watu wenye nia njema, watakaoweza kuliendeleza taifa, msiengemee chama chochote na pia tuendelee kukumbushana kuyakubali matokeo," aliagiza Rais Kikwete.


Katika hatua nyingine, Rais Kikwete pia alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi hao juu ya tabia inayoanza kujitokeza ya dini moja kuikejeli dini nyingine.

Alisema ingawa Tanzania ina uhuru wa kuabudi, pale dini yoyote itakapofanya kitendo hicho hadharani, serikali itaingilia kati.


"Wengine wanasema kuwa tunaingilia uhuru wa kuabudu, lakini siyo kweli, sisi sheria zetu zinasema usikejeli dini ya mwenzako, ukifanya hivyo sisi tunaingilia kati," alisema Kikwete.


Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kushirikiana kati ya viongozi wa dini na serikali akieleza kuwa pande hizo zote zina lengo moja la kutaka upendo na maendeleo kwa jamii.


Alisema wakati mwingine serikali inaweza kufanya jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linaweza kuwakera viongozi hao wa dini na kuwa hali hiyo itakapotokea, viongozi hao wasisite kuwasiliana naye moja kwa moja au kupitia mawaziri.

"Sisi wote ni binadamu kwa hiyo tutaweza kukosea lakini, nyie mna watu, unaweza kumwambia waziri au mtu mwingine amwambie waziri mkuu kuwa mnataka kuonana naye au aniambie mimi.Pia mnaweza kutumia simu yangu iko wazi muda wote unaweza kunipigia uniambie moja kwa moja," alisisitiza Kikwete.


Awali Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Iringa Dk Owdemburg Mdegella alisema kikao hicho kimepitisha maazimio saba ambayo pande zote mbili; serikali na viongozi wa dini wamekubali kuyatekeleza.


"Kwa kuwa Serikali imeona umuhimu wa kutayarisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kuwashirikisha viongozi wa dini ili kuielewa, kuijadili na kuifikisha kwa waumini; viongozi wa dini tunapongeza na kuhimiza serikali kuwa waaminifu katika kuitekeleza," alisema Askofu Dk Mdegella.


Alisoma maazimio hayo kuwa ni serikali kuweka utaratibu maalum wa kukutana na viongozi wa dini mara mbili kwa mwaka na Serikali kudumishe utaratibu wa kutumia mtandao wa viongozi wa dini kwa kupanua wigo wa ushiriki ili kufikisha taarifa sahihi kwa jamii yote.


Maazimio mengine ni viongozi wa dini washirikishwe mapema katika hatua za awali wakati wa kushughulikia masuala mbalimbali muhimu ya kitafa na viongozi wa dini wasishabikie siasa katika nyumba za ibada.


Kwa mujibu wa Askofu Mdegella maazimio mengine ni ilani za vyama vya siasa zitayarishwe kwa namna ambayo hazitawagawa Watanzania kwa misingi ya dini, kabila, rangi, jinsi ama eneo analotoka na Serikali na taasisi za dini na zile za kijamii zishirikiane kuandaa mikakati endelevu ya maadili ya kitaifa


Rais Kikwete alikubali hoja zote zilizofikiwa katika mkutano huo akipendekeza kuwa katika suala la kukutana mara mbili kwa mwaka na viongozi hao, ligawanywe katika mafungu mawili.


Alisema fungu la kwanza liwe lile la kukutana na viongozi kutoka katika madhehebu na jumuiya mbalimbali kwa nyakati tofauti na lile la pili viongozi wote wa dini na serikali wakutane kwa wakati mmoja.


Hata hivyo, kama ilivyokuwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo, wahandishi wa habari jana pia hawakuruhusiwa kuingia katika mkutano huo wakati majadiliano hayo yanaendelea.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Mkutano huo, Philip Marmo alikijiuta katika wakati mgumu jana asubuhi baada ya waandishi wa habari kumbana awape maelezo endapo hawatakiwi kwenye mkutano huo.


Waandishi hao walitaka Marmo aeleze kwanini amekiuka ahadi aliyoitoa mwanzoni kuwa waandishi wa habari wangeruhusiwa kuingia katika mkutano huo na kwanini vyombo vingine viliruhusiwa na vingine kukataliwa. Chombo kilichoruhusiwa katika mkutano huo ni TBC1 pekee.


Hata hivyo, Waziri Marmo hakutaka kujibu swali hilo akieleza kuwa ana haraka, kitendo ambacho kiliwafanya waandishi wa habari wamzuie kwa nguvu na kuendelea kumhoji.


Baadaye Marmo aliwaomba waandishi hao kutulia akiwaahidi kwamba wataingia katika majadiliano, lakini pia hakutekeleza ahadi yake hiyo.


"Jana niliona hali inataka kuchafuka ndiyo sababu nikiwa kama mwenyekiti nikachukua hatua ile ya kuwafukuza. naomba mnisamehe na hao TBC1 walirusha zile habari kimakosa walitakiwa wachukue picha kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi tu,".

 
Jamani tunaongozwa na wajinga!!!
eit..."Tumeendelea kuboresha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, lakini, lile la takrima ni gumu. Mfano katika mkoa wa Kilimanjaro huwezi kuwaita wazee ukazungumza nao bila kitochi," alisema Kikwete.

Na mwizi mwenye pychological problem? Na yeye kuacha kuiba si ngumu. Kwa hiyo tusimshtaki au vipi? This is ridicolous! Huyu jamaa nadhani hiyo degree ya economics UD aliibia tu! Huwezi kuongea ujinga ivi!
 
Huyu jamaa simwelewi kabisa wana JF hv ni mtimamu, kwani ukiambiwa na wazee wa kilimanjaro kuwa CUF, CHADEMA n.k wanaiba na wewe utaiba? Yeye kama mkuu wa nchi kama aliona hii ni ngumu kwa ni i alisign? jamaa ananichosha akili sio siri maana nikisikia anaongea na watu roho inakuwa juujuu tu maana na mimi ni kiongozi mwenzake kwenye chama nasema sijui leo atachapia kubwa then nasema bora liwe dogo lisiwe kubwa. Jamaa ni mbishi ndugu zanguni sio kwamba watu wa karibu yake, akiwa na jamaa zake atapiga story weee mpaka muda unakaribia hata hajaipitia hotuba na kusiscuss na watu wawiili watatu. na pia sio fast thinker. Yule unaweza ukamuwekea tusi akatukana jukwaani.
 
Mungu Ibariki Tanzania na Ipitishe salama katika kipindi hiki kigumu, Na mwenyezi Mungu tunakuomba akitoka huyu bwana tupate mtu mwingine ambaye atakuwa na uwezo wa kuiongoza nchi yetu. Amen.
Jamani watanzania lililobaki ni maombi tu tupite salama hii ni sawa na gari bila dereva.
 
kwanini isiwezekane kama mtu ameamua kutofanya kitu illegal? huo ni uhamasishaji kwa wanasisiemu ccm kuanza kuandaa elfu kumikumi vitenge na kanga kwaajili ya kampeni....anafagilia kosa mbele ya raia? mbona watajimwagaaa
 
Hakuna haramu yoyote rahisi kuikwepa, isipokuwa kwa kupitia sheria tu. Mila za Kichagga zinaendana na takrima in good faith..kama vile mtu au chama chochote kinapoandaa mkutano wanapoweka vinywaji. Harusi, sherehe inapokuwa na vinywaji na vyakula lakini Unapogawa Takrima kwa malengo ya kuhadaa ili kuchaguliwa au kupendwa - hii ndiyo tofauti.

Sidhani kama Jk mwenyewe hawezi kutofautisha Takrima hasi na chanya. Kweli kuna a thin line baina yake, pamoja na hivyo ni rahisi sana kutambua na kukana takrima yenye malengo mabaya.

Mfano mdogo ni kwamba sidhani kama yeye JK anaweza kukubali au kuona Uhalali wa hongo la fedha au mali ili binti yake amkubali bwana. Mapenzi yanapoingiza fedha mbele ndipo Uhalali wa Kupendana unapoondoka na fedha kuwa sababu. Tatizo la kutumia fedha badala ya mapenzi ni pale mwanao anapohadaika na fedha badala ya tabia ya bwana.
Hii ndio hofu kubwa ya Takrima.
 
Mimi nadhani tufike mahala sasa tuseme basi!!! Tuchague watu wenye uwezo wa kupambanua na kusimamia yale wanayo amini. Soft people, play boys na waswahili will never take as anywhere. Ila wana faida kwa mafisadi kwani hupata nafasi ya kufanya upupu wao. Mafisadi hawa wameonekana kututeka na kutufanya tuamini na kufanya mambo kwa matakwa yao.

Ni lazima tubadilike na kufanya maamuzi bila ushawishi wa waru katika kufanya maamuzi. Hapo ndipo tutaondokana na watu kama akina jk. Ambao kamwe hawatatuongoza kuelekea maendeleo ya kweli. Watu ambao hawajui dhamana ya nafasi walio nayo katika jamii wanayoingoza
Mmmmh seems umesahau ni chaguo la MUNGU usimwite hivyo tafadhali

HAKI HUINUA TAIFA,BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE Mithali 14:34
 
Hamna chochote sheria usaini mwenyewe alafu unaanza ooh kutekeleza
kifungu ....itakuwa ngumu bila takrima haya sasa umeanza kutapatapa
huyu ndio atakuwa wakwanza kutoa takrima jamani kaeni chonjo huyu
jamaa hayuko serious.
 
Back
Top Bottom