Elections 2010 JK: Serikali haina uwezo wa kutoa huduma za jamii bure

Mnabadirisha tu gitaa na midundo. Kwani shule za kata ada yake ni kiasi gani?? Na pia naomba tu msaada ni nchi gani inayotoa elimu bure ya kujimu kifedha na fee??
Good point, MkamaP!! Unajua watu hapa JF wanashindwa kabisa kutofautisha reality na fantasy. Haya mambo ya elimu ya bure and stuff ni kejeli tu za kifikra.
 
Kuna kitabu fulani hapa wazungu wanashindwa kuelewa, ikiwa na kichwa cha habari kama ifuatavyo, ngoja nikiweke ktk kiswahili

Wazungu wanauliza

KWANINI TANZANIA NI MASIKINI WAKATI INA HONEST LEADER(NYERERE) NA MALASIA INA CORRUPT LEADER NA INAENDELEA?

Hiyo swali jiulize ukipata jibu, ndo tutajadili vizuri.
Jibu lake ni rahisi: watanzania walio wengi ni wavivu wakubwa, tena wakutupwa! Kukaa vijiweni na kuwalalamikia viongozi wa serikali kila siku ndicho wanachojua (hilo tunalishuhudia hata hapa jukwaani)! Badala ya hao wanaolalamika kila siku kuketi chini na kubuni mbinu za kujikomboa toka kwenye umasikini, wananchokifanya na kuwaza na kufikiri jinsi ya kupiga mizinga watu wengine na kuililia serikali iwa-bailout. I mean, no one is/will ever be great without working hard. It's a fact wether you like it or not. Japan, China, Singapore, Malaysia, South Korea waliliona hili mapema kabisa na kuamua kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuongeza productivity. Watanzania inabidi tuache hizi hadithi za abunuwasi tunazosimuliana hapa jukwaani kila kunapokucha. Ukweli ni kwamba, nchi zilizoendelea watu wanafanya kazi ile mbaya! Kwasababu wanajua wasipofanya kazi: (a) hawatakula. (b). Watanyang'anywa nyumba walizopangisha. (c) watakatiwa huduma za muhimu kama simu, maji na umeme (4). Watashindwa kulipia insurance premium zao. And as a result, it's high productivity all the way, baby...
 
Wakuu zangu,
Kwanza nawaombeni radhi kwa sababu namwaga shuzi ambalo litawachefua wengi hapa.

Hakuna kitu kibaya kama hawa wasomi wanaokwenda ulaya kusoma kisha baada yta masomo wanarudi nyumbani na kuanza kusimulia watu habari za Ulaya kama vile wana experience ya kutosha..Lakini ukweli ni kwamba hawajui lolotre zaidi ya masomo yaliyowaleta hivyo hizi habari za kutumia mifano ya nchi za nje kama kigezo hali hufahamu kitu ni ujinga mwinge ambao unataka pia darasa jingine.

Nasema hivi hakuna nchihata moja isiyokuwa na Public school - HAKUNA.. hata Marekani zipo shule za Public na bure ziikigharamiwa na serikali. Sasa tunapobishana sana kuhusu elimu bure sijuihwa wasomi wanafikiria kwamba Dr.Slaa atataifisha shule zote ziwe bure au wanakuwa wakifikiria kipi hata kudai kwamba elimu bure haiwezekani pasipo vigezo vya kutowezekana kwake.

Maadam nyie nyote ni wasomi ni vizuri sana unapopinga hoja na kudai Haiwezekani basi vizuri kuunganisha na mifano hai ambayo inapinga gharama au ukusanyaji wa kodi zitakazo wezesha, lakini kubisha tu huku mkitumia nchi za nje hali ukweli sivyo nashindwa hata kuwaeleweni. Na kibaya zaidi watu wamefikia kusema nchi yetu bado ni changa hivyo hatuwezi kulinganisha na hizo nchi za Ulaya lakini hao hao bado wanapendekeza mfumo wa elimu wa nchi za Ulaya hali wanashindwa kujiuliza elimu ilikuwa vipi huko Ulaya wakati wao pia wakiwa wachanga?..I repeat Public school zipo na zilikuwepo kila nchi duniani na BUREEEE!!!!

Madai ya kusema ati elimu bure inagharimu quality ya education ni uongo usiokuwa na maana kabisa..kwani nchi zote zinazosifika duniani kwa quality ya education wanatoa elimu bure hivyo ku raise cap ya mashindano kwa shule binafsi..Leo hii elimu nchini imeshuka kwa sababu hakuna malengo ktk quality ya education. System iliyopo imeifanya demand ya elimu kuwa kubwa sana kuliko supply hivyo raia wanawajibika kununua elimu kwa gharama yoyote iliyopo hata kama ni feki.

Tunauziwa Elimu kama mali feki kutoka nje sawasawa na mali nyinginezo kutoka India na China kwa sababu tumepoteza UHITAJI na kufikia SHIDA ya kila kitu hivyo tupo radhi kununua chochote kinachoweza kupatikana..Na kama tumefikia kiwango cha kupoteza standard ya elimu nchini hatuwezi kuendelea kulipia elimu ambayo ni feki au mtumba kwa sababu tu ndio kipimo wanachoweza kuona kinatufaa sisi kwa kuwa ati nchi yetu bado changa...I mean jamani hata mtoto mchanga sii ndiye hutegemea kutunzwa na wazazi wake iweje leo uchanga ndio unahitaji kugharamia..logic iko wapi?

Na mwisho nasikitika sana kumsikia MkamaP akisema ati wakati wa Nyerere tulisoma chini ya mwembe.. sijui ni wakati gani na shule zipi anazozungumzia kwani wengine hapa tumesoma shule za msingi mashambani kabisa na hapakuwepo kabisa na shule ya mwembeni kufikia darasa la saba. Kisha wakati akiibeza elimu ya mwalimu nyerere kwa kutuleta viongozi hawa wabaya, huyo huyo MkamaP anasifia elimu ya Tanzania leo chini ya viongozi waliosomeshwa na Nyerere..
Nimetoka mtupu!!
 
Elimu bure haipo popote duniani maana ni gharama kununua vitabu, kujenga majengo, kulipa walimu n.k Tofauti ipo kwenye mfumo unaotumika kugharamia hiyo elimu. Unaweza kusubiri nje ya darasa kama konda wa daladala ili kila anayeingia ndani akupe gharama za kusoma au.. Dr Slaa anakuja na wazo tofauti kuwa gharama za kusomesha zitakusanywa toka kwa wananchi wote kwa njia ya kodi na mapato mengine ya serkali. Na swali huyu daktari na mwalimu wanaotakiwa kuwahudumia watanzania tena kwa mishahara isiyo kuwa mikubwa sana mbona mnataka yeye tu na baba yake ndio wagharimie kusoma kwake? Kama ni hivyo na akianza kazi basi aruhusiwe kuvuna toka ofisi yake kama wanavyofanya DRC ukipewa ofisi ni mbele kwa mbele kila kinachopita mbele yako ni halali yako. Dr Slaa anaona elimu ya watanzania inanufaisha watanzania wote hivyo igharamiwe na wote. Wasioelewa mfumo wa social services ndiyo wanasema haiwezekani. Kwani tunapopita katika barabara ya lami iliyojengwa kwa billions wewe unalipia nini directly? Road tolls hazipo, lakini tunachangia gharama hizi katika kodi zetu, ndivyo itakavyokuwa katika suala la elimu n.k Ni vile watawala wetu wa sasa elimu si kipaumbele chao hivyo hawako tayari kuelekeza mapato ya serkali na kodi katika huduma ya elimu. Dr slaa tangu jana nimeamua nitakupa kura yangu hata kama mimi ni CCM.
 
Elimu bure haipo popote duniani maana ni gharama kununua vitabu, kujenga majengo, kulipa walimu n.k Tofauti ipo kwenye mfumo unaotumika kugharamia hiyo elimu.

Una uhakika ulichoongea hapo nilipo weka bold ?

Watoto wanasoma bure hadi high school kwenye jimbo la Texas-USA,serikali inagharamia kila kitu na wazazi wanakabwa kwenye kodi;mzazi yeyote anayepeleka mwanae kwenye shule za public Marekani anayajua haya!Hata Kenya na Rwanda sasa wapo kwenye mchakato wa elimu bure kwa wananchi wake

Shule bure inawezekana kama tutarekebisha priorities zetu na kuacha anasa kama vile kutenga bilion 30 kwenye kodi kwa ajili ya sambusa na chapati kwa maafisa wetu na mabilion ya pesa kutengenezea Ikulu kila mwaka,na kudhibiti mianya ya rushwa hizo pesa zote zielekezwe kwenye maendeleo!
 
Kila kata mbili zina shule ya sekondari.Hilo si dogo.Ni hatua ya kupongezwa.Sasa kilichobaki ni kulinda hizi shule na kuzipatia vifaa na walimu.Hiyo ni hatua inayofuata.Haihitaji Phd kufahamu kuwa ni ahadi iliyotekelezeka.

Wakuu ni vizuri tukiwa na busara zaidi ya kuvutwa a wanasiasa. Ukiona hizo shule unaweza ksema ni jengo lililojengwa mwaka 1901, shule zinajengwa mwaka 2005 lakini ukiziangalia leo ukilinganisha na alizojenga mkoloni unaona za mkoloni ni much much better kuliko shule zenyewe and then mtu anakuja kujidai amejenga shule. What kind of schools do we really need, what kind of education would we like to have. Tusidanganye wananchi kwa kujenga vijengo vya ovyo na kuviita shule. We can be smarter than that.
 
Una uhakika ulichoongea hapo nilipo weka bold ?

Watoto wanasoma bure hadi high school kwenye jimbo la Texas-USA,serikali inagharamia kila kitu na wazazi wanakabwa kwenye kodi;mzazi yeyote anayepeleka mwanae kwenye shule za public Marekani anayajua haya!Hata Kenya na Rwanda sasa wapo kwenye mchakato wa elimu bure kwa wananchi wake

Shule bure inawezekana kama tutarekebisha priorities zetu na kuacha anasa kama vile kutenga bilion 30 kwenye kodi kwa ajili ya sambusa na chapati kwa maafisa wetu na mabilion ya pesa kutengenezea Ikulu kila mwaka,na kudhibiti mianya ya rushwa hizo pesa zote zielekezwe kwenye maendeleo!

Mkuu Malafyale ukisikia watu wanasema haiwezekani ujue wana matatizo. Tanzania has been there before tunaweza kumuuliza JK mwenyewe kama alilipia elimu yake hadi chuo Kikuu, tunaweza kumuuliza Profesa Lipumba, tunaweza hata kumuuliza Dk Slaa tusikie majibu yao kwa wao walivyosoma then tuone kama wanachosema ni kweli au si kweli. Serikali ina uwezo wa kulipia elimu na afya burem ni kuprioritize tu, sio kutumia pesa ovyo kwenye mambo yasiyo ya maana.
 
Jibu lake ni rahisi: watanzania walio wengi ni wavivu wakubwa, tena wakutupwa! Kukaa vijiweni na kuwalalamikia viongozi wa serikali kila siku ndicho wanachojua (hilo tunalishuhudia hata hapa jukwaani)! Badala ya hao wanaolalamika kila siku kuketi chini na kubuni mbinu za kujikomboa toka kwenye umasikini, wananchokifanya na kuwaza na kufikiri jinsi ya kupiga mizinga watu wengine na kuililia serikali iwa-bailout. I mean, no one is/will ever be great without working hard. It's a fact wether you like it or not. Japan, China, Singapore, Malaysia, South Korea waliliona hili mapema kabisa na kuamua kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuongeza productivity. Watanzania inabidi tuache hizi hadithi za abunuwasi tunazosimuliana hapa jukwaani kila kunapokucha. Ukweli ni kwamba, nchi zilizoendelea watu wanafanya kazi ile mbaya! Kwasababu wanajua wasipofanya kazi: (a) hawatakula. (b). Watanyang'anywa nyumba walizopangisha. (c) watakatiwa huduma za muhimu kama simu, maji na umeme (4). Watashindwa kulipia insurance premium zao. And as a result, it's high productivity all the way, baby...

Can not agree more than this. Lakini si kweli kama viongozi wetu ni honest, at least Nyerere was. So la uvivu linaaongeza mafuta kwenye moto. That is why i believe kwa administration style tuliyonayo na kwa aina ya viongozi tuliyonayo, hata miaka 100 ijayo Tanzania itaendelea kurudi nyuma haitapiga hatua za maana. wanasiasa wengi ni waongo wanajineemesha wao kuliko nchi yao.
 
Jibu lake ni rahisi: watanzania walio wengi ni wavivu wakubwa, tena wakutupwa! Kukaa vijiweni na kuwalalamikia viongozi wa serikali kila siku ndicho wanachojua (hilo tunalishuhudia hata hapa jukwaani)! Badala ya hao wanaolalamika kila siku kuketi chini na kubuni mbinu za kujikomboa toka kwenye umasikini, wananchokifanya na kuwaza na kufikiri jinsi ya kupiga mizinga watu wengine na kuililia serikali iwa-bailout. I mean, no one is/will ever be great without working hard. It's a fact wether you like it or not. Japan, China, Singapore, Malaysia, South Korea waliliona hili mapema kabisa na kuamua kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuongeza productivity. Watanzania inabidi tuache hizi hadithi za abunuwasi tunazosimuliana hapa jukwaani kila kunapokucha. Ukweli ni kwamba, nchi zilizoendelea watu wanafanya kazi ile mbaya! Kwasababu wanajua wasipofanya kazi: (a) hawatakula. (b). Watanyang'anywa nyumba walizopangisha. (c) watakatiwa huduma za muhimu kama simu, maji na umeme (4). Watashindwa kulipia insurance premium zao. And as a result, it's high productivity all the way, baby...
Amen!
I said this before that majority of Tanzanians are lazy.
Evidence:Look at the thousands of lazy guys sitting on vijiwes in Dar running their mouths for nothing from sunshine to sundown!
 
Hiyo point! Lazima tukubali kuwa inafika wakati wazazi nao wachangie elimu za watoto wao> Hii biashara ya bure bure hii ni tamu sana masikioni lakini utekelezaji wake sio mchezo!
Kijana vipi...we mwanafunzi nini? Ada tunalipa hata tusio na watoto shule. Majina tu yamebadilika. Tunalipa PAYE, na kama haitoshi, simu unayopiga unalipia kodi, daladala unayopanda unalipia kodi, nyumba unayokaa unalipia kodi, umeme.......Hata bytes ulizotumia hapo umelipia kodi. Inaitwa Mr. VAT. Sasa pesa zote hizo unasema hatulipi ada. Kama ameshindwa, ashuke chini wapande wengine!
 
Expecting free education. free healthcare, welfare benefits......that's utopia:jaw:
Raj Patel Jr;

USA government for years provide free education up to high school and some times even to university level;Americans enjoy massive free health cares;Obamacare to extend more than 30 milion Americans who do not have any kind of medical insurances, free medicaid for children,free medicare for seniors and tremendeous welfare services such as "WIC and FOOD STAMP" for any one who do not have any job.According to Raj Patel Jr statement;Is America under utopian era simply because the government provide free services to their constituents?

Kama unakusanya kodi na unaweka priorities zako vyema huduma za bure zinawezekana kabisa,na kama Raj Patel Jr ulivyosema kuwa upo NYC basi unajionea mwenyewe ambavyo serikali ya Obama inavyotoa huduma bure kwa wanaohitaji huduma hizo!

Tuache unazi kwenye ukweli jamani,huduma bure ni haki ya msingi na ya kujivunia ya kila MTZ hasa anayeihitaji!
 
hivi ndugu yangu unajua unalolisema kweli?, nchi maskini kivipi mbona sielewi?, yale madini yote ambayo mengine yapo hapa tu jamani bado mnaongea hizi habari za nchi maskini jamani?......umeona report za madini yanayouzwa kweli? ....nchi masikini gani kuna watu wanaiibia mamia ya mabilioni?....maskini ni sisi nani maskini wa fikra ndo maana tunadanganyika eti nchi maskini hakuna kitu kama hicho hata kidogo, chagueni viongozi wazuri muone hii nchi ilivyotajiri,kubalini changes mjifunze
 
mimi mwenyewe nimesoma ugaibuni miaka 7.

WENGI WETU TUNATETEA NDUGU WATANZANIA WENZETU AMBAO HAWAJUI HATA DAR ES SALAAM IKOJE - WANAKAA VIJIJINI - NDANI SANA (REMOTE) HAWANA MAJI, HOSPITALI NA HATA KAMA KUMEJENGWA SHULE ZA KATA - HAKUNA WALIMU KWANI NYUMBA ZA WALIMU HAZIPO - NA KAMA ZIPO - WEWE ULIYESOMA UGAIBUNI 7 YEARS UKIPEWA HUWEZI KUKAA - NA HIZO SHULE HUWEZI KUMPELEKA MWANAO -

SERIKALI YA TANZANIA INAWEZA KUTOA ELUMU BURE - TENA SIO ELIMU BURE TU - BALI YENYE KIWANGO - YAANI WALIMU WENYE KIWANGO - WANAOLIPWA VIZURI, WANAOISHI VIZURI - WANAOFANYA KAZI KWA MOYO - LAKINI SERIKALI YA CCM IMESHINDWA SHAURI YA UBINAFSI - WANATUMIA HELA NYINGI MNO KUJINUIFAISHA WENYEWE - WAMEACHIA LOOPHOLES NYINGI SANA KWA FEDHA ZETU KUIBWA - MIKATABA FEKI - KUSAMEHE KODI MAKAMPUNI/WAGENI - SHAURI YA KUPOKEA RUSHWA NA KUPEWA 10% - WASINGEFANYA HIVYO -..................INGEWEZEKANA - KODI TUNAZOLIPA NI KUBWA MNO - ZINAENDA WAPI???

hivyo wewe uliyesoma nje - jaribu kujiweka kwenye NAFASI YA MTU WA KIJIJINI - NDIO UTAONA KUWA SERIKALI INATAKIWA IWASAIDIE WANANCHI WAKE

Brown bread, maziwa ya NIDO - Pizzas - hamburg - etc. zisikupofushe macho ndugu yangu - WATOTO WA WATANZANIA WOTE WANAPENDA KUSOMA NJE PIA - WATETEE - USIWAKANDAMIZE .............please - have a heart of GOD..........[SORRY KAMA NIMEKUKWAZA - ILA THINK TWICE ]
 
JK ni mjinga kabisa Kuiba mabilioni inawezekana lakini Elimu ya bure ya mamilioni haiwezekani!!!! Kweli watanzania tu wajinga na wavivu wa kufikiri . Thanks God Mungu amenipa hekima sidanganywi na mwizi wa pesa ya UMMA.
Kama mtu afikirivyo ndivyo atakavyo kuwa!
Kuna msemo usemao"In the abundancy of water the fool is thirst"
Tatizo letu si umaskini,Tatizo letu ni wizi,ubadhirifu,ufisadi,kutokuwa na uongozi wenye ubunifu,kuendelea kutawaliwa na viongozi wasio na vision na kuendekeza uomba omba wakati hao tunaowaomba wanauona utajiri na fursa tulizo nazo!
Katika kauli za JK zinazonikera ni pamoja na jinsi anavyo zungumza kwa madaha kuhusu misaada kutoka nje"Wamarekani watatusaidia hiki,wamesema watatupa pesa za kile....wameshatupa vitabu....nk...nk!
Kama tungebadilishiwa sisi twende Rwanda na wao waje hapa kwa miaka mitano.....nchi hii tunayosema ni maskini,isiyoweza lolote hata kugharamia elimu na afya ya watu wake ingetustaajabisha!
Kwa mfano.Ni mabilioni mangapi tunapoteza kwa kutosimamia vizuri uvuvi,Utalii wetu,madini,mazao pori,rasilimali watu,ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo?
Ni ajabu kabisa.Tuna maji mengi kuliko 1/3 ya afrika ukiichanganya...yet hatujitoshelezi kwa chakula...Huduma ya maji safi na salama mijini haifikii asilimia 50!
Ama kweli "Katikati ya utajiri wa maji mpumbafu ana kiu!"

Tafakari......Chukua hatua october 31,2010
 
Kwa CCM hili haliwezekani kwa sababu their number one priority ni UFISADI. This is just a question of where a country channels its money. Imagine for example:
1. EPA money 133 Billions were taken by few individuals who Mr Mengi said their number doesn't no exceed 20. How many class rooms could be build by this sum of money.
2. Economic stimuli package; Experts say the Sh1.7 trillion stimulus package was set aside in the 2009/10 budget to boost the financial states of some of the companies in Tanzania. It is obvious that the money was given to those who Dr. Slaa described MARAFIKI WA JK. In such setting where the president favors his allies, this country will never rise up. The list cont.........
3. Rada
4. IPTL
5. Richmonduli, DOWANS, etc
6. Majengo pacha
7. Deep green, meremeta,
8. Matrekta,
9. Safari za JK,
10 Mashangingi (200 m each)
11. Posho za wabunge, mawaziri, nk
12. Manunuzi ya hovyo Tanseco, Mawizani, Taasisi za umaa nk
13. Mikataba feki kama Buzwagi
14. nk, nk,nk,nk,
Conclusion: If we can block these leakages of government resources and amalgamate/consolidate/pull them together, I assure you we will be able to give free most of the social services to our people. Imagine for example if only 220 billion was used to bring water from lake victoria to Kahama (>300KM away), 133 EPA (half of 220 b) could be enough to make water services reach Tabora. This could save thousands of people in the town including the villages in vicinity of the main pipeline.

So free and quality education is possible
 
Back
Top Bottom