JK Sahani Moja na Upinzani Hotuba ya Agosti

kwakweli nawashauri msijemkasilikiliza hiyo hotuba, itawaharibia siku, aisee JK ni binadam namba moja ninayemchukia hapa duniani,
 
Hapo umenena mkuu,jamaa km kawaida yake ameshaandaa vijembe na mipasho kwa wapinzani kwan ndo silaha pekee iliyobaki kwa magwanda.utasikia kuna mpango mkakati hili neno analitumia sana na vicheko visivyo na msingi.
Haya ngoja tusubir hiyo taarabu ya agosti30.
 
kwani hamjui atasema nini mpaka sasa atasema hivi , kuhusu tatizo la umeme kuna Megawatt 100 kutoka Mnaz bay na Songosongo pia nilipokuwa south Africa nilizungumza na bwana JACOB NZUMA baada ya kumuuliza wewe vip mbona hapa hakuna mgawo? ndio akanimbia kwani Tanzania kuna mgawo nikamjibu ndio,bac akaniahidi kutafuta wawekazeji watakaozlisha Meggawatt 500, kwa hiyo mjue Serikali in nia ya thati kabisa ya kuondoa umaskini wa Mtanzania.
 
nCHI NYETU NI KAMA TIMING BOMB INASUBIRI MUDA AU KICHOCHEZI (STARTER) NDOGO TU ILIPUKE MAANA IKO KWENYE AUTO PILOT NA PILOT KALEWA CHAKARI
 
Nchi ya M ichakato na bado linafanyiwa upembuzi yakinifu, sijui kosa ni kukua kwa kiswahili au watumiaji. Maana Mkuu haya maneno yamekuwa silaha ya viongozi wazembe, na kibaya hata wafanyabishara nao wameyaiga.

Mwezi uliopita nilitafuta pair moja ya tairi low profile. Kila ukienda dukani jamaa anakwambia bado nafanya mchakatio mpaka tumeagiza NBI

Maudhui makubwa ya Hotuba za JK ni kuwataka waTZ kuwa wajinga kwa kumsikiliza na kutomchallenge nahodha ambaye hata watoto wa chekechea wanamhofia kwani wanaona dhahiri chombo kimemshinda. Kebeli kwa upinzani, onyo na tahadhari za kitoto kwa waTZ eti kwa kigezo cha amani ndizo nyimbo zitakazosikika kwenye hotuba yake ambayo kwa kawaida haijawahi make any change na huwa naona tu kama nyimbo za mipasho.

Kama atataka tumsikilize aje na implementable plans kama za upinzani na asije kutukaririsha hotuba zilizotolewa bungeni na mawaziri wake la sivyo tuta change channel na badala yake tuangalie katuni.
 
Kila jambo na wakati wake. Muda wa rais kuongea ulikuwa wakati wa mgomo wa mafuta. Nchi ilikuwa kama yatima, na kwa mara ya kwanza Tanzania iliongozwa na Bunge! Tukumbuke bunge ni chombo cha kutunga sheria na sio watendaji, lakini kutokana na uyatima uliotukumbuka kama nchi tulijikuta tunaongozwa na bunge!.

Kwa sasa sijui ataongea kitu gani maana kumekuwa na blunders nyingi mno na hakutokeza kusema chochote. Na hapa narudi kwenye hoja yangu ya siku zote kuwa kuna haja ya kupangua safu ya washauri wake hapo Magogoni. Haiwezekani nchi ikae kwenye giza, at the same time mgomo wa mafuta uwepo lakini rais aendelee kama hakuna tatizo. Hata kwa showwwww tu kwanini asingetembelea kituo kimoja cha mafuta wakati wa mgomo ili wananchi waone kweli anajali?

Yote tisa, kumi ni huu mkakati wa kuonekana kufutarisha kila siku na kuwapa zawadi walaji huku akiwa bubu kwenye mambo ya msingi. Naomba nieleweke sina tatizo na futari, ila zimekuwa ni nyingi mno na walaji wenyewe ndani yake kuna watu wa mashaka kama Mtuhumiwa Mayor Masaburi.

Na mwisho, kuna upuuzi wa kupindukia unaendelea pale kitengo cha Mawasiliano. Sijui ni idea ya nani lakini siku za karibuni wamekuwa wanarusha vipindi walivyoandaa (kurugenzi ya mawasiliano) kupita TBC1 vinavyomuonesha rais Kikwete kwenye ziara mbalimbali nje ya nchi. Nimesema huu ni upuuzi kwa sababu wakati wananchi na hata wabunge wa ccm wanahoji kauli ya serikali kuhusu umeme na mafuta wao Kurugenzi ya mawasiliano wanarusha vipindi vinavyomwonesha rais akipunga upepo ugenini! Huyu Rais amekuwa analalamikiwa kwa kusafiri kila kukicha, sasa, kwa nini uoneshe mambo ya safari wakati watu wanauliza kulikoni hasemi chochote kuhusu hali ngumu ya maisha hapa nyumbani? Ni message gani hii kurugenzu inataka watu wapate? Kwamba anasafiri sana? we already know that!

Ushauri wangu tena kwa nia njema kabisa, huu mkakati wa vipindi vinavyomwonesha rais anatumbua maisha wafute mara moja for thier own good and the good of thier man! Vinaharibu badala ya kumjengea heshma. Unless kama na wao wanam-fix boss wao kwa kumuonesha kama mtu mpenda raha wakati watu wanapanga foleni za mafuta huku wakiwa wanakaa gizani. Mkakati mbovu kabisa.
 


JK Sahani Moja na Upinzani Hotuba ya Agosti

Watanzania tuna utamaduni wa kushangaa mazuri na kufurahia mabaya kwa kutazama tu anayeyasema ni nani na wakati gani bila kuzingatia anayoyasema yana tija au ni porojo tu za jukwaa kujisafishia mkate wake.

Mpaka leo huwa najiuliza alitoa wapi ujasiri na undumilakuwili ule Mzee wangu Ben katika kampeni za mwisho za CCM pale jangwani 2010 alipoamua bayana kuwatukana wapinzani ati ni wanafiki wakubwa kwa kuhoji serikali imefanya nini kama vile hawana macho.

Ni mwaka tu sasa unakatika hata kauli hii ya Mzee Ben bado haijafutika katika masikio yetu alipoibuka ghafla kutoka Nairobi katika usuluhishi wa ghasia za baada ya Uchaguzi Nchini Kenya ambapo alirejea huku ujio wake ukitanda wingu zito la kashfa ambazo si mahala pake kuzizungumza maana si mintarafu ya makala nayokusudia leo.

Namtazama Mzee Ben kama kioo na chagizo muhimu katika kusaidia kutanzua mkwamo wa kiuchumi Nchini lakini kwa hili nasema hapana tena iliyoshiba huku nikisukumwa sasa na matokeo ya utitiri wa kauli za wanasiasa wenye njaa ambao nao wametumbukia katika mkumbo huu wa kuukebehi upinzani akiwemo mjomba wangu Mzee wa Viwango na Spidi.

Inawezekanaje katika Nchi hii ambayo leo tunaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru hali ya miundo mbinu na huduma za kijamii ni duni kuliko maelezo ya kawaida huku tukiendelea kujinasibu kwa nyimbo nyingi nzuuri za kisiwa cha amani na tuna rasilimali nyingi, ambazo kamwe hatujui zinamsaidia nani?

Wenye kuyaona haya mapema wengi wanaishia kutiwa tonge mdomoni na wengine kulambishwa asali na kuusahau shubiri hii ya ukali wa maisha unaowakabili watanzania.

Sishangai Rafiki yangu Mjomba aliyejitahidi kwa kutunga Beti zenye mantiki na ukosoaji wa hali ya juu kwa uozo huu wa serikali na yeye leo tayari domo limejaa zege maneno hayatoki tena baada ya kupewa ulaji na Adui yake Mkubwa mpango wa Malaria ambaye hata pale katika tamasha kubwa la malaria hakumwalika lakini baada ya kelele za wanahabari wakamkumbuka na leo haemi kitu tena zaidi ya kushabikia ujinga.

Akianzia kule TCRA, baadaye Zain na sasa katika dawa butu za Maralia.
Kama haitoshi kila ukifunua mdomo kuwaambia watanzania tudai haki yetu kwa nguvu ya Umma maana mazungumzo yameshindikana baadhi ya wenzetu wenye msongo wa mawazo na ufinyu wa fikara bado watakwambia nyie mmezoea vurugu tu hebu iacheni serikali ifanye kazi.

Ashkum si matusi, kazi gani hiyo ambayo bado wanataka kuifanya na wameshindwa kuimaliza katika kipindi cha miaka hamsini isiyokuwa na tija ya kuridhisha, narudia tena tija ya kuridhisha au ni wizi tu na udangayifu kwa umma.

Hakuna sababu tena ya mtanzania kusimama akipinga maandamano ya CDM, hii ndio njia sahihi iliyobakia kuonyesha nini hasa tunahitaji na si porojo na hotuba ndeefu ambazo kila siku zinaediwa kisha copy na paste.

Msingi wa hoja yangu ni hapa kuna fununu kwamba baada ya kimya kirefu Mkuu wa Nchi anajipanga kutoa Hotuba Mwisho wa mwezi huu ikiwa ni sehemu ya kureview na kupoza makali kwa hekaheka nyingi zilizolikumba Bunge la serikali yake kipindi hiki.

Na pengine kutoa mkono wa Iddi kwa waumini wa Dini ya Kiislam.
Linalotarajiwa hapa ni mkuu wa Nchi kuzungumza tena kwa ukali huku akijinasibu kwa kuvaa usiriasi usioonekana katika matendo yake zaidi ya kufanya maigizo hayo katika luninga.

Hii haitoshi kwa kuwavaa wapinzani na kusimanga juhudi zao muhimu kabisa za kushinikiza mabadiliko, tunataka kuona huduma za uhakika kwa watanzania wa leo na kwa hakika tunawajibika kuendelea kulipigia hili kelele kupitia Nguvu ya Umma hadi kieleweke.


ADIOS

Ahadi za Bwana Mkubwa hizi hapa: KWA OMBI MAALUM ndani ya Thread

JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png


Join Date : 22nd October 2009
Location : Mtimbwani
Posts : 500

Rep Power : 23

[h=2]
icon1.png
Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015[/h]
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha





Hizo ahadi zote zzimeshatimizwa, au ipi ambayo haijatimizwa hapo? naona uko nyuma kweli ki muono na kifikra.
 
1. Cement itauzwa Tsh 5000(elfu tano)
2. Elimu bure
3. Bati moja kuuzwa kwa Tsh 5000
3. Blaaa blaaa blaaa!
4.Kuondoa uonevu kwa wanyonge(hapo hapo ana ishi na mke wa Mshumbusi)
 
1. Cement itauzwa Tsh 5000(elfu tano)<br />
2. Elimu bure<br />
3. Bati moja kuuzwa kwa Tsh 5000<br />
3. Blaaa blaaa blaaa!<br />
4.Kuondoa uonevu kwa wanyonge(hapo hapo ana ishi na mke wa Mshumbusi)
<br />
<br />
Akili ni nywele! Hivi bei ya Cement kwa Tsh 5000 ingedumu kwa muda gani? Hizi sera za kuandikiwa na Freeman ni ujinga mkubwa!
 
Hizo ahadi zote zzimeshatimizwa, au ipi ambayo haijatimizwa hapo? naona uko nyuma kweli ki muono na kifikra.

Ntakuweza wake ushakunywa maji ya Bendera kwako rangi zote kijani hata ukiambiwa mzungu mweupe utasema mbona akifa anakuwa Kijani
 
<br />
<br />
Akili ni nywele! Hivi bei ya Cement kwa Tsh 5000 ingedumu kwa muda gani? Hizi sera za kuandikiwa na Freeman ni ujinga mkubwa!

Uchumi umekupita kushoto kajipange upya

Unapopunguza gharama za uzalishaji na ukadhibiti mfumko wa bei uliowashinda haya yote yanawezekana.
 
1. Cement itauzwa Tsh 5000(elfu tano)
2. Elimu bure
3. Bati moja kuuzwa kwa Tsh 5000
3. Blaaa blaaa blaaa!
4.Kuondoa uonevu kwa wanyonge(hapo hapo ana ishi na mke wa Mshumbusi)

Umeziona hizo tu kuna sitini na nane pale napost 32 soon. Majungu si mtaji tazameni ukweli acheni kupayuka wakuu
 
Tushavaa parachuti atalipuka nayo hii ndege mwenyewe this tym wajanja washaanza kuruka mmoja baada ya mwingine, waoga wameua AIR CCJ
 
kwakweli nawashauri msijemkasilikiliza hiyo hotuba, itawaharibia siku, aisee JK ni binadam namba moja ninayemchukia hapa duniani,

Kiukweli unaweza kutamani kumchomoa kwenye hasikrini I mean screen Mkuu, te te he this is serious inapofikia Mkuu wa Nchi unafagilia mipasho ni hatari sana
 
kwani hamjui atasema nini mpaka sasa atasema hivi , kuhusu tatizo la umeme kuna Megawatt 100 kutoka Mnaz bay na Songosongo pia nilipokuwa south Africa nilizungumza na bwana JACOB NZUMA baada ya kumuuliza wewe vip mbona hapa hakuna mgawo? ndio akanimbia kwani Tanzania kuna mgawo nikamjibu ndio,bac akaniahidi kutafuta wawekazeji watakaozlisha Meggawatt 500, kwa hiyo mjue Serikali in nia ya thati kabisa ya kuondoa umaskini wa Mtanzania.

Bila kusahau hadithi ya Mama Clinton nayo tutaisikia siku hiyo
 
Bila kusahau hadithi ya Mama Clinton nayo tutaisikia siku hiyo

Mkuu ifanye hii status sticky bana watu waendelee kuchangia na kujadili hizo ahadi maana naona mwaka unakatika hakuna jipya
hao wana magamba waache tuu waropoke si unajua wameambiwa wapinge kila kitu na kusifia hata pale ambapo kuna giza wanasema ni mwanga umezidi mpaka umekuwa giza
 
Mkuu ifanye hii status sticky bana watu waendelee kuchangia na kujadili hizo ahadi maana naona mwaka unakatika hakuna jipya
hao wana magamba waache tuu waropoke si unajua wameambiwa wapinge kila kitu na kusifia hata pale ambapo kuna giza wanasema ni mwanga umezidi mpaka umekuwa giza

Ngoja tuitupie katika Bango Mkuu wa baraka za Mkuu INVISSIBLE
 
Back
Top Bottom