JK: Safari za Nje Sasa Basi!

Sekenke

Senior Member
Mar 3, 2008
132
29
Ilishawahi kusikika: 'Kelele za mlango hazitunyimi usingizi'

---

Wiki moja iliyopita:
'Pamoja na watu kulalamikia safari zangu, ukweli ni kuwa nalazimika kusafiri kwa kuwa safari zangu hazina mbadala'... na kwamba atasafiri kwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano siku chache zijazo.

Sasa:
... Ameamua kubadili uamuzi wa kwenda Copenhagen... badala yake amemtuma Makamu wa Rais, Dk Mohamed Shein... anayeondoka leo, kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya jana... Dk Shein ataambatana na Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk Batilda Buriani na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira wa Zanzibar Burhani Saadat.

...Kwa mujibu wa blog ya Ikulu Rais keshafikisha safari 20 nje ya nchi... anasafiri takriban mara mbili kila mwezi.

Chanzo: Safari za Nje Zamuelemea JK, Mwananchi Jumapili, Desemba 13, 2009
 
ilishawahi kusikika: 'kelele za mlango hazitunyimi usingizi'

---

wiki moja iliyopita:
'pamoja na watu kulalamikia safari zangu, ukweli ni kuwa nalazimika kusafiri kwa kuwa safari zangu hazina mbadala'... Na kwamba atasafiri kwenda copenhagen kuhudhuria mkutano siku chache zijazo.

Sasa:
... Ameamua kubadili uamuzi wa kwenda copenhagen... Badala yake amemtuma makamu wa rais, dk mohamed shein... Anayeondoka leo, kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya jana... Dk shein ataambatana na mama mwanamwema shein, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (mazingira) dk batilda buriani na waziri wa kilimo, mifugo na mazingira wa zanzibar burhani saadat.

...kwa mujibu wa blog ya ikulu rais keshafikisha safari 20 nje ya nchi... Anasafiri takriban mara mbili kila mwezi.

Chanzo: Safari za nje zamuelemea jk, mwananchi jumapili, desemba 13, 2009

kikwete is not that good upstairs. Walikuwa sahihi kumpima akili
 
Kama rais, ana mambo mengi ya kufanya, pia ni vyema mambo mengine akaonyesha kwamba ana imani na watendaji wengine. Sio lazima kila kitu afanye yeye itakuwa haina maana ya yeye kuwa na wasaidizi binafsi napongeza kama ameona kuna haja ya kutuma wawakilishi na hasa kilio cha wananchi kwamba rais wao anasafiri sana, na hivyo ana ji expose kwenye danger.

Kijijini kwetu tunasafiri inapokuwa lazima sana, kwani magari hupinduka!!
 
Hata Vasco Da Gama alijaribu wakati fulani kutulia nyumbani.. guess what.. alishindwa.
Huu mkutano wa mazingira hakuna value yoyote kwa nchi yetu afadhali amemwachia mzee shein

Usimlinganishe rais wetu na na hilo li-reno tafadhali
 
Huu mkutano wa mazingira hakuna value yoyote kwa nchi yetu afadhali amemwachia mzee shein

Usimlinganishe rais wetu na na hilo li-reno tafadhali

Kama wanalingana au kufanana basi watalinganishwa na kufananishwa... wote wana sifa kuu na kutotulia nyumbani

mimi kutoka ofisini wiki tu nakosa usingizi lakini mkulu anatoka wiki tatu!!! hii mbado mimi ona...
 
Huu mkutano wa mazingira hakuna value yoyote kwa nchi yetu afadhali amemwachia mzee shein

Usimlinganishe rais wetu na na hilo li-reno tafadhali

Kamuachia kwa ajili ya kelele zetu, I am sure usiku halali kwa ajili ya kumiss hiyo safari kwa vile alishajipanga. Nani alisema kelele za mpangaji azimnyinmi suingizi mwenye nyumba?? Kamuulize JK kwa nini kamuachia makamu??? Lakini kwa JK kuachia hii wakati tulishaambiwa ankwenda nafikiri kuna safari nyingine njiani hivi karibuni!!
 
Madhara ya kula Miguu ya Kuku alipokuwa mtoto, hawezi acha kusafiri huyo!
 
Kama wanalingana au kufanana basi watalinganishwa na kufananishwa... wote wana sifa kuu na kutotulia nyumbani

mimi kutoka ofisini wiki tu nakosa usingizi lakini mkulu anatoka wiki tatu!!! hii mbado mimi ona...

Niliwahi kusikia kipindi cha nyuma, serikali iliwataka watumishi wa serikali kutokuwa nje ya kituo cha kazi (kuhudhuria warisha, kongamano, nguvu kazi nk) kwa muda usiyozidi siku kadhaa kwa mwaka. Mwenye kumbukumbu sahihi atanisaidia. Lengo hasa ilikuwa kwamba ukiwa nje ya kituo cha kazi lazma kazi nyingi hazitalala ofsini kwako. Na huyo unayemwachia ofsi kwa kipindi icho chote ndiye anayestahili kuichukua nafasi yako, kwani inakuwazi kuwa ndiye anayefanyakazi zote pale ofsini hivyo wewe hustahili kuwepo pale? Je huu utaratibu ulifutwa au kama upo mkuu wa kaya huu utaratibu yeye haumgusi?
 
Kamuachia kwa ajili ya kelele zetu, I am sure usiku halali kwa ajili ya kumiss hiyo safari kwa vile alishajipanga. Nani alisema kelele za mpangaji azimnyinmi suingizi mwenye nyumba?? Kamuulize JK kwa nini kamuachia makamu??? Lakini kwa JK kuachia hii wakati tulishaambiwa ankwenda nafikiri kuna safari nyingine njiani hivi karibuni!!
Rais haendeshwi na kelele za nje

Ameamua kumwachia VP kwa ridhaa yake na kwa faida ya nchi!

Yuko pale kuhudumia wananchi...na safari zake ni kwa manufaa ya nchi na watu wake..
 
Hivi JK akikaa nchini kwa angalau miezi miwili akaomba ushauri wa wataalam wa uchumi, kilimo, elimu n.k.,
  1. Wakajadiliana juu ya nini nchi ifanye,
  2. Akaanza kutekeleza maoni yao,
  3. Akafuatilia utekelezaji wa waliyoafikiana na
  4. Kupima utendaji wake kila siku
Hivi haya ni magumu sana kwake au miuu inamuwasha?
 
Hivi JK akikaa nchini kwa angalau miezi miwili akaomba ushauri wa wataalam wa uchumi, kilimo, elimu n.k.,
  1. Wakajadiliana juu ya nini nchi ifanye,
  2. Akaanza kutekeleza maoni yao,
  3. Akafuatilia utekelezaji wa waliyoafikiana na
  4. Kupima utendaji wake kila siku
Hivi haya ni magumu sana kwake au miuu inamuwasha?
Majibu
1. wajadiliane nini wakati kila kiongozi na wizara zinajua ifanye nini na tayari wanafanya..mbona unauliza kama vile hakuna kinachofanyika au ni uvivu wako kuona na kupima?
2. Maoni ya nini wakati kuna election manifesto inatekelezwa hatua kwa hatua na ndio direction, maoni yanafanyika wakati wa uchaguzi sasa hivi ni utekelezaje? uchaguzi umeisha watu wana chapa kazi nchi haendeshwi kwa maoni..unafikiri ni family business hii..election manifesto imetekelezwa for almost 70% fungua ukurasa wa manifesto uone
3. Unafikiri rais kufuatilia ni mpaka afike eneo la tukio kama daktari wa upasuaji ebbo! kuna utaratibu wa kufanya wala si lazima awepo nchini ndio utekelezaji ufanyike...
5. Kupima utendaji wake wa kila -nani kakwambia hafanyi ulifikiri lazima atangaze hilo kwako..performance review inafanyika kila wakati kwa mujibu president office regulations...

Tatizo lenu mnafikiri nchi ni habari moja tu ufisadi ufisadi basi...kuna shule zinajengwa, dispensary zinajengwa, barabara zinajengwa, vyuo vikuu vinajengwa, mikopo inatolewa, sheria zinatungwa..everything is in order...

hizo kelele za wafuasi wa lowassa na wanaojiita wapiganaji ni upupu na kukosa uzalendo kwa kiwango cha hali ya juu na uki-connect DOTS unaona kabisa wote wametokea sehemu fulani (root), wengine na opportunists wengine ni wivu wengi wao ni failures
 
JK hawezi kukaa nyumbani sababu hajui maana ya kuwa Rais wa jamhuri!! Kuna mambo mengi mno ya kufanya kuhusu Kilimo, afya, elimu, infrastructure ambayo kama angeyavalia njuga basi taifa lingepiga hatua kubwa sana.

Huwezi kusema eti kuna mawaziri inatosha, sasa kwa mwendo huo si tunaweza kwenda mbele zaidi na kusema hakuna haja ya mawaziri sababu kuna makatibu wakuu, wakurugenzi nk????

Rais kaa ofisini uinusuru nchi mkuu.
 
Rais haendeshwi na kelele za nje

Ameamua kumwachia VP kwa ridhaa yake na kwa faida ya nchi!

Yuko pale kuhudumia wananchi...na safari zake ni kwa manufaa ya nchi na watu wake..

Na wewe siku yeyote ukija enda Cuba wakakupime akili zako kama zipo sawa hasa kwa kushindwa kutuambia wana JF faida anayotuletea JK akisafiri nje ya nchi mara kwa mara!

Maneno yako na nadharia zako za "Makambalism"tunaomba ukawaambie Lumumba,JF for a great thinkers na usituletee propaganda za akina Tambwe!
 
Tumain
Join Date: Sat Jun 2009
Posts: 1,921
Thanks: 553
Thanked 446 Times in 310 Posts
Rep Power: 24

Otherwise kama ulibadili jina lako la zamani,mwaka huu JF tutaona mengi sana na sijui kama tutavumilia!

Great thinker aliyekuja JF miezi 4 iiliyopita na mbwembwe za kumsifia JK kama safari zake zina maslahi kwa babu zangu waliopo kijijini Lufilyo-Kyela!

Hopeful this dude is kidding!
 
Tumain
Join Date: Sat Jun 2009
Posts: 1,921
Thanks: 553
Thanked 446 Times in 310 Posts
Rep Power: 24

Otherwise kama ulibadili jina lako la zamani,mwaka huu JF tutaona mengi sana na sijui kama tutavumilia!

Great thinker aliyekuja JF miezi 4 iiliyopita na mbwembwe za kumsifia JK kama safari zake zina maslahi kwa babu zangu waliopo kijijini Lufilyo-Kyela!

Hopeful this dude is kidding!


HAYUPO PEKE YAKE, homeboy wako wa Kyela na yeye yumo.

MBUNGE wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye anayefaa kuongoza nchi na ni mhimili mkubwa katika vita ya ufisadi ila baadhi ya wasaidizi wake wanamrudisha nyuma katika vita hiyo.

Alisema hayo jana katika kongamano la miaka 10 Bila ya Baba wa Taifa lililoandaliwa na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini na kufanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii (ISW).

Mwakyembe alikuwa akijibu swali la mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesoma shahada ya elimu, Chagona Deogratias aliyetaka kufahamu iwapo hoja alizokuwa akitoa Dk. Mwakyembe katika kongamano hilo alikuwa akiogopa kumsema Rais.

"Mimi kwangu namuona Rais anafaa kuongoza…bali tunapaswa tumuondolee baadhi ya watu wanaomchafua," alisema Dk. Mwakyembe huku akiwataka watu wasimfikirie vibaya anapotoa hoja zake kuwa ni mbwembe bali anajiamini kutokana na elimu aliyonayo na hivyo anajivuna.

 
ehuuuuuu...angalau hatimaye amefuata ushauri...ahueni sana hii jamani..

sasa mheshimiwa raisi apige kambi kabisa pale ikulu, aende na kule vijijini kwenyewe kabisa ambako hata baiskeli haifiki akajionee tanzania halisi anayoiongoza, labda itasaidia kumuongezea uzalendo kwa nchi yake.
 
Usimlinganishe rais wetu na na hilo li-reno tafadhali

"Wamefikia hatua ya kumlinganisha Rais na Vasco da Gama, hii ni heshima kubwa, jina la Vasco da Gama ni kubwa, kuna majengo na mitaa vinaitwa jina lake, bila yeye leo Ureno isingekuwa hii tunayoijua. Mimi ningeitwa Vasco da Gama ningefurahi" - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kama alivyonukuliwa na Gazeti la Mtanzania la Jumamosi, Januari 19, 2008 Ukurasa wa 1: 'Membe atetea safari za Kikwete'
 
Imagine kiongozi mkubwa kabisa anakosekana nchini kwa muda wote huo! Hivi hatujajifunza kwamba muda ni mali? Kuna mtu anaweza kuonyesha faida ambayo mpaka sasa hizi safari zimetuletea sisi kama nchi?Vinginevyo ni upotezaji muda tu
 
Back
Top Bottom