- Mkuu wa nchi anajiamini sana wewe safari za nje Mkapa alikuwa anamsubiri uwanjani wa ndege uliwahi kusikia wapi rais anasubiri waziri? hivi unakumbuka swali la kwanza aliloulizwa kwenye kampeni za urais, aliposema yeye kushinda sio suala la mjadala na la kushindwa halipo kabisa na akashinda anyways!
- Hajiamini ilikuwaje Kigoda chaguop la Mkapa akawekwa pembeni? Tumseme mengine lakini la kujiamini sidhani, unless kuna ushahidi zaidi ya uliotolewa hapa so far! Ndani ya CCM anakuwa makini sana maana anajua one mistake chama kinavunjika, lakini in the end siku zote anataimiza anayotaka, ingawa huenda sio kwa speed tunayoitaka hapa JF.
- Leo Mramba na Yona wamerudi lupango, anatakiwa ajiamini vipi zaidi jamani wakati so far anafanya kweli?
Mnyonge mnyongeni lakini haki tumpe!
Heshima mbele mkuu.
Suala la rais kumsubiri waziri wake uwanja wa ndege sijui unamaana gani hapa kwani sidhani kama maswala ya itifaki yanakubaliana na hili. Kama Mkapa alikuwa anamsubiri Kikwete uwanja wa ndege wa JKN sawa kwani hakuna kisichowezekana Bongo.
Kuhusu suala la ushindi, hiyo ni lugha ya kiushindani hata John McCain alikuwa anasema anashinda. HRC alikuwa anasema anashinda, Obama alisema anashinda matokeo yake mmoja wao ameshinda. Mtu mdhaifu yoyote anaweza sema hivyo mkuu.
Suala la akina Mramba na Yona ni ushahidi tosha kabisa kuwa mkuu hajiamini. Mahakama ni taasisi inayojitegemea na majukumu yake yako bayana. Kwasababu jamaa hajiamini (by definition) mkono wake uko kila mahali matokeo yake anaharibu kila kitu. Hatakiwi kutoa amri yoyote kuhusu wahalifu. angekuwa anajiamini angeacha sheria ifuate mkondo.
Ninadhani huyu ni rais mdhaifu katika historia ya Tanzania.