JK Nyerere: Mtauza (Mtabinafsisha) Kila Kitu.... hadi Ikulu mtabinafsisha.

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,277
8,492
Haya ni Maneno yaliyotamkwa na Mwalimu JK Nyerere (RIP) hapo zamani, akimsuta Mkapa kwa sera zake mbovu. Alisema watauza hadi Ikulu.

Sasa yanayoendelea kutendeka hapa nchini ni kutimiza unabii wa Mwalimu. Wameuza mashirika ya umma, wamebinafsisha reli wameua, Ndege wamemalizia, Umeme taabani.

Wameanza kuuza wanyama na bandari zetu. Bado muda sio mrefu watageukia kuuza wake na watoto wetu na watamalizia kuuza ikulu.
 
Ubinafsishaji ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishauanzisha ni lazima utawatafuna daima.
 
Hivi Tanzania sasa hivi hakuna mtu kama Nyerere, Nyerere aliyasema yanatokea sasa hivi miaka mingi iliyopita watu wakadharau sasa tunahitaji mtu mwingine kama yeye atueleze kitu gani kitatokea miaka ijayo.
 
Nyerere alikuwa focused na uelewa wa matatizo yanayowakabili waTanzania, pia alijua Tanzania aitakayo. Hayupo mtu wa namna ile. Alitaka kutokea, ndugu E.M. Sokoine, wakamuwahi. Nyerere nae wakamharakisha.

Slaa alisema kuichagua CCM na Kikwete ni janga la Kitaifa. Sasa nalishuhudia janga hili live. Wanyama wanabebwa wazima wazima, hakuna anayewajibika, wabunge wa CCM ni kama mbwa mbele ya chatu, unafiki mtupu.
 
Back
Top Bottom