Jk: Njia panda

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Kikwete aanze kipi? Chama, Serikali, Bunge ama Madaktari?

Vijana wa mtaani wanasema “ameshikwa bapaya”. Bunge wanataka ongezeko la pesa - naona hilo anajaribu kutia mkazo hakusaini, lakini hawezi kusema hadharani. Madaktari wamegoma lakini alichelewa kuona mgomo huu utafika hapa ulipo kwahiyo hawezi kuingilia sasa. Waziri Mkuu anashutumiwa anambadilisha vipi maana kambadilisha Lowasa majuzi tu - na swala amuweke nani? ili afanye nini? Eti afanye reshuffle kwa nini? Lakini unamfukuzaje Waziri na Naibu wake tu? Wabunge wa CCM wanamtishia juu ya katiba na labda kutoridhishwa na maamuzi yake ya posho.

Jamani haya mambo sio mepesi, na tusitizame kama jambo moja moja maana ikitokea tu haya mambo yakaunganika - basi tumekwisha.

Nadhani kikwete anahitaji ushauri hapa! Aanzie wapi? Unaanzaje na mgomo wakati ndani kwako ni vuruvaru?
 
kuhusu posho yeye mwenyewe alisema'' nakubali posho LAKINI wabunge watumie busara zaidi''.......hilo ni kosa la kwanza

kutotoa kauli juu ya mgomo wa madaktari kabla hajaenda davos ...lilikuwa kosa la pili

kuhusu katiba siku chadema wamemfata ile siku ya kwanza alitoa kauli moja..'' nisiposaini wenzangu ndani ya chama hawatanielewa''

hili lilikuwa kosa la tatu....

mambo yote haya yanatokana na kitu kimoja..lack of power from within'' hili ndilo tatizo la huyu jamaa.......na ndio maanakila kitu kimemshinda.........
 
Nakuhakikishia kuwa kila kitu kitakaa sawa tena bila tatizo lolote! endelea kutega masikio tu.
 
Uraisi ni kazi ya watu kama udereva ikushinda ustraabu ni kubwaga manyanga kinyume cha hapo subiri uambiwe imekushinda kwa maandamano na mawe!
 
Nakuhakikishia kuwa kila kitu kitakaa sawa tena bila tatizo lolote! endelea kutega masikio tu.

Nadhani hapo ndipo napopapenda mimi na labda tumpe Raisi heshima yake. Nakubaliana kabisa na wewe kwamba Raisi wetu anastaili ya uongozi wake - Jenerali kasema "KUTOA PASI" - lakini baada ya hapo taifa linaendela kwa amani. Nadhani tunapaswa kuelewa staili hii, yawezekana Raisi anaelewa wananchi wake kuliko tunavyojielewa sise wenyew.

Hofu yangu kwa sasa, huu ni mgomo ambao umedumu kwa muda mrefu sana, nadhani katika miaka kumi iliyopita ndio tunaweza kusema mgomo uliofanikiwa. Matokea ya mgomo huu unamadhara makubwa huko mbeleni - uishe ama usiishe kwa amani ama bila maelewano - umejenga imani kwa watu ukiwa ngangali Serikali itafyata tu.
 
Rais hana mamuzi rais gani huyu hii inaonyesha jinsi gani jk anavyotumikia watu wachache ila watanzania wengi waliopiga kura ya hapana na kura zikaibiwa basi tena tusubirie 2015
 
Kile kipindi chake cha kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi kimeishia wapi? Na uwakika kua alikianzisha ili apate taarifa na madukuduku moja kwa moja kutoka kwa wananchi. Hao wachache anaowasikiliza na kuwatii ndio wamwangushao. Pole sana kiongozi
 
Rais hana mamuzi rais gani huyu hii inaonyesha jinsi gani jk anavyotumikia watu wachache ila watanzania wengi waliopiga kura ya hapana na kura zikaibiwa basi tena tusubirie 2015
Location yako imesema yote. Vipi lema hajambo?
 
Imekula kwake, na bado still more to come labda aresign, he has got no GUTS to handle issues/
 
Kile kipindi chake cha kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi kimeishia wapi? Na uwakika kua alikianzisha ili apate taarifa na madukuduku moja kwa moja kutoka kwa wananchi. Hao wachache anaowasikiliza na kuwatii ndio wamwangushao. Pole sana kiongozi

Nilidhani angetumia kipindi hicho kurekebisha mambo! Lakini bahati mbaya alikuwa safari
 
imekula kwa wapinzani bado ni Rais wetu

True! He is the President of the Republic of Tanzania for now and for 3 years to came. As citizens we can strike and critique hoping for subtle changes at least.
 
Waganga wa Kienyeji wanawajengea Wateja wao Confo! Hata kwenye msitu wa Simba mtu unaweza kujikuta unataka kupita tu eti kwa sababu Mganga kakwambia, kwa dawa aliyokunywesha na ukivua nguo zote, Simba hawawezi kukuona! Kwa hiyo haya mambo mengine msiyaone yako hivi ni muendelezo tu wa Imani toka kwa Waganga wa Kienyeji.
 
Nakuhakikishia kuwa kila kitu kitakaa sawa tena bila tatizo lolote! endelea kutega masikio tu.

Ha ha ha ha ha ha! Mkuu hayo maelezo yako yananikumbusha mbali sana; nayafananisha na yale ya the former Saddam Hussein spokesman - Tarik Aziz. Alikuwa anaongea hivyo hivyo. Mlisoma chuo kimoja nini Mkuu? Au ndio kanuni za hiyo "kazi yenu"? Anyway, tumwombee Rais wetu na serikali yake waiongoze nchi yetu kwa hikima.
 
Mwalimu alisema Ikulu ni mzigo na mizigo yenyewe ndiyo hii urais si lele mama wanaotaka 2015 watakuwa machizi na badooooo!!!
 
Waganga wa Kienyeji wanawajengea Wateja wao Confo! Hata kwenye msitu wa Simba mtu unaweza kujikuta unataka kupita tu eti kwa sababu Mganga kakwambia, kwa dawa aliyokunywesha na ukivua nguo zote, Simba hawawezi kukuona! Kwa hiyo haya mambo mengine msiyaone yako hivi ni muendelezo tu wa Imani toka kwa Waganga wa Kienyeji.

Serikali na Bunge kufarakana, huduma za jamii kusuasua, nasikia mashirika yasiyo ya kiserikali yanaandamana leo. Kimbunga huwa kinaanza hivyo! ni vyema hizi dalili tuziendeleze kwa mzaha
 
Lile jengo la magogoni ni noma. Aliliweza mwl. Nyerere tu wengine wote dah but kwahuyu hali imekua mbaya mara 30 ya wote wa nyuma. Tuone huyo atakayefuata.
 
Back
Top Bottom