Mchakato wa Katiba mpya bado ni mjadala endelevu hadi hapo itakapopatikana.Mwishoni mwaka 2011 Wabunge hasa wa CHADEMA hawakuridhika na maamuzi ya Bunge kuupitisha mswada huo.Walitoka nje wakati wote wa mjadala wa Katiba ulipokuwa ukijadiliwa. Waliazimia kufanya maandamano nchi nzima kuupinga mswada. Katika hotuba ya Mwaka Mpya 2012, Rais aligusia mchakato huo. Hata hivyo, alitoa angalizo kwa wale wanaotaka kuandamana akiwakumbusha kwamba dola ipo. CHADEMA walisikia. Wakakaa chini, wakatafakari. Wakaomba kuonana na kiongozi wa nchi.Akawaruhusu. Waliwasilisha maoni yao. Hata hivyo, hawakuridhika na uamuzi wa JK kuutia sahihi mswada huo baada ya mazungumzo na wawakilishi wa chama hicho. Waliazimia tena kuandamana.Hata hivyo, busara ilichukua mkondo wake. Wakaomba kuonana na Rais kwa mara ya pili. Wamefanya. Wameweza. Rais msikivu amewasikia.Tanzania ni yetu sote: CCM.CHADEMA, CUF, NCCR, nk. Ni mwanzo mzuri wa ukuzi wa Demokrasia ambayo katika nchi yetu naweza ifananisha kama ipo katika hatua ya mchicha ila kwa hekima tutaikuza na kuwa kubwa kama mbuyu.Kumbe ujumbe unaweza kufika kwa wahusika bila maandamano?
MWAKA 2005 JK ALIPOINGIA MADARAKANI ALISEMA HIVI " Ukiona Watu wanakusifia sana na kukushangilia kwa kila jambo, ujue wamekufanya ZUZU, wanakuibia hao"
Naona umeamua kumsifia sana JK....si Bure!!!