Jk ni msikivu: CHADEMA pia wamemsikia-hakuna maandamano sasa!

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
725
Mchakato wa Katiba mpya bado ni mjadala endelevu hadi hapo itakapopatikana.

Mwishoni mwaka 2011 Wabunge hasa wa CHADEMA hawakuridhika na maamuzi ya Bunge kuupitisha mswada huo. Walitoka nje wakati wote wa mjadala wa Katiba ulipokuwa ukijadiliwa. Waliazimia kufanya maandamano nchi nzima kuupinga mswada. Katika hotuba ya Mwaka Mpya 2012, Rais aligusia mchakato huo. Hata hivyo, alitoa angalizo kwa wale wanaotaka kuandamana akiwakumbusha kwamba dola ipo. CHADEMA walisikia. Wakakaa chini, wakatafakari. Wakaomba kuonana na kiongozi wa nchi. Akawaruhusu. Waliwasilisha maoni yao. Hata hivyo, hawakuridhika na uamuzi wa JK kuutia sahihi mswada huo baada ya mazungumzo na wawakilishi wa chama hicho. Waliazimia tena kuandamana.Hata hivyo, busara ilichukua mkondo wake. Wakaomba kuonana na Rais kwa mara ya pili. Wamefanya. Wameweza. Rais msikivu amewasikia.

Tanzania ni yetu sote: CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, nk. Ni mwanzo mzuri wa ukuzi wa Demokrasia ambayo katika nchi yetu naweza ifananisha kama ipo katika hatua ya mchicha ila kwa hekima tutaikuza na kuwa kubwa kama mbuyu.

Kumbe ujumbe unaweza kufika kwa wahusika bila maandamano?
 
Na amini usiamini, maandamano hayo ndio yamemsabishia ****** kuwa mpole, maana Peoples Power si kitu ya mzaha!
 
Mchakato wa Katiba mpya bado ni mjadala endelevu hadi hapo itakapopatikana.Mwishoni mwaka 2011 Wabunge hasa wa CHADEMA hawakuridhika na maamuzi ya Bunge kuupitisha mswada huo.Walitoka nje wakati wote wa mjadala wa Katiba ulipokuwa ukijadiliwa. Waliazimia kufanya maandamano nchi nzima kuupinga mswada. Katika hotuba ya Mwaka Mpya 2012, Rais aligusia mchakato huo. Hata hivyo, alitoa angalizo kwa wale wanaotaka kuandamana akiwakumbusha kwamba dola ipo. CHADEMA walisikia. Wakakaa chini, wakatafakari. Wakaomba kuonana na kiongozi wa nchi.Akawaruhusu. Waliwasilisha maoni yao. Hata hivyo, hawakuridhika na uamuzi wa JK kuutia sahihi mswada huo baada ya mazungumzo na wawakilishi wa chama hicho. Waliazimia tena kuandamana.Hata hivyo, busara ilichukua mkondo wake. Wakaomba kuonana na Rais kwa mara ya pili. Wamefanya. Wameweza. Rais msikivu amewasikia.Tanzania ni yetu sote: CCM.CHADEMA, CUF, NCCR, nk. Ni mwanzo mzuri wa ukuzi wa Demokrasia ambayo katika nchi yetu naweza ifananisha kama ipo katika hatua ya mchicha ila kwa hekima tutaikuza na kuwa kubwa kama mbuyu.Kumbe ujumbe unaweza kufika kwa wahusika bila maandamano?

Kwa muda mrefu sana tuliwaambia kwamba suluhu ya migongano ya itikadi za kisiasa ni kukaa pamoja mezani wao wakasema ni barabarani na kususia vikao... wangeanza hivyo sasa hivi tungeshaanza kuhama toka kwenye mchicha tunekuwa kwenye (CHINOHE - kwa lugha moja ya hapa nchini maana yake ni kambuyu kachanga)

View attachment 47405


View attachment 47406


View attachment 47407
 
VGL: Umegongomelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la malalamiko.Umetuwekea ushahidi wa Rais Msikivu na CHADEMA mpya yenye utii kwa kiongozi wao wa nchi. tufika tu kwenye ukuzi wa demokrasia kuwa chinoe [sic];toka mchicha hadi mbuyu!
 
Kwa PINDA kuliona hilo mapema ambalo matunda yake hata wewe unayafurahia huoni kwamba ni busara?

Pinda hapa aliona mbali. CHADEMA nao sasa wametumia darubini wameona mbali ambako Pinda alikwisha ona.Angalau matunda ya ukomavu wa kisiasa tutaanza kuyaona.
 
hakuna kisichowezekana kama watu wakiamua kukaa pamoja na kufanya 'meaningful, genuine and result-oriented discussion' kwa mustakabali wa taifa lao
 
hakuna kisichowezekana kama watu wakiamua kukaa pamoja na kufanya 'meaningful, genuine and result-oriented discussion' kwa mustakabali wa taifa lao

Ukomavu huo pia umedhihirishwa na Mbowe pale mjengoni aliposisitiza:Maslahi ya nchi kwanza; vyama baadaye.
 
Msikivu sana ndio maana hata mambo serious ya kitaifa anasubiri aambiwe nini cha kufanya badala ya kuongoza na kuonyesha njia.
 
Msikivu sana ndio maana hata mambo serious ya kitaifa anasubiri aambiwe nini cha kufanya badala ya kuongoza na kuonyesha njia.

Nguvumali. Urais ni taasisi. Unahitaji sana uamuzi wa pamoja. Ikitokea rais anayeamua aonavyo inafaaa kwakuwa tu yeye ni rais, huyo mhesabie siku: Atageuka kuwa dikteta!
 
Nguvumali. Urais ni taasisi. Unahitaji sana uamuzi wa pamoja. Ikitokea rais anayeamua aonavyo inafaaa kwakuwa tu yeye ni rais, huyo mhesabie siku: Atageuka kuwa dikteta!

hata mwili wa nyoka unabeba vitu kibao ili aweze kutambaa lakini bado kichwa kinakuwa na ukali zaidi ya sehemu nyingine ya mwili sasa hata yeye anatakiwa awe kama kichwa cha nyoka
 
Sio usikivu wala nini alipigwa mkwala ma mabalozi (wazungu) siku CCM wakicheza mdundiko bungeni chadema wakiwa wametoka. Usikivu ameanza lini???? na maswala mengine ni ukubwa wa misafara yake ilitoka indirectly akaamua kusema pia kapunguza. Zungu prayer si mchezo
 
JK mwenyewe anakunwa sana na CHADEMA na ingekuwa kuna kubadilishana angehamia CDM coz ameona jamaa walivyo na hoja za nguvu,haijawahi kutokea Rais kuwageuka wabunge wake, na alikiri kabisa kuwa alisaini kwa kuogopa kutengwa na wenzie hata walioporomosha mashairi bungeni,sheria iliporudi wamejikuta wakila matapishi yao,muulizeni Sendeka.

Kimsingi kama tutafika kwenye demokrasia ya masikilizano mazuri ni jambo jema sana,katika hili la katiba hauna mshindi na mshindwa,ni faida ya watanzania wote!Japokuwa waanzilishi wa vuguvugu walikuwa CDM.

Jk angekuwa pia msikivu kwenye RICHMOND,DOWANS,EPA,Vyuo vikuu,madaktari n.k nadhani tungefika pazuri.mi siafiki kuwa marekebisho haya yametokana na usikivu tu wa JK.big NO,ni kwamba hali ilikuwa mbaya kwani wahisani walitishia kuacha kutupia rupia kwenye kombe la matonya kama anawabana wapinzania na kupitisha sheria kandamizi!

Tuna safari ndefu sana kuelekea ule usikivu halisi wa kidemokrasia,ila inawezekana ni suala la wananchi kufunguka kifikra!
Waliokwazika tusameheane,ndo uhuru wa mawazo wenyewe!
 
Back
Top Bottom