JK ndani ya mji wa Moshi....

boybsema

Senior Member
Oct 28, 2010
124
14
Rais JK kaingia ndani ya mji wa Moshi mida hii akiwa ndani ya ulinzi mkali...kila kona ni polisi waliosheheni silaha nzito,msafara wake ni zaidi ya magari 30...atakuwa kwenye lango kuu la mlima kilimanjaro (marangu gate) jirani na kwa lyatonga wa kiraracha...
 
Sasa atembelee wapi Wakuu kama kila mahali mnamkandia? Awe Tz mnasema, akienda nje, nako mnamsema.
 
Anata kupanda mlima mrefu kuliko yoyote Afrika.Itakuwa vema akaweka rekodi ya kuwa raisi wa kwanza Kuupanda.

Na kale kaugonjwa ketu kalikompatia sifa Babu wa Loliondo katamuacha kweli? Nasikia na yeye alikwenda kupiga kikombe cha babu! Nijuavyo mimi kama afya yako inahitaji msaada wa kikombe cha Babu basi ukijidai shujaa wa kupanda mlima Kilimanjaro ujue huo ndo mwisho wa maisha yako au utasababisha watu wakubebe kwenye yale machela yetu!............. Mungu ongoza mkono wako ili mheshimiwa rais wetu asikubali kupanda mlima Kilimanjaro kwani bado miaka mitatu tu tumpe heshima ya ustaafu!.........
 
Mwacheni Jemadari wetu Mkuu atutembelee kwetu na sisi tujisikie kidogo. Kuna kata moja ya mbege inamsubiri pale Marangu Mtoni wakati akisharudi kupanda mlima. Ria Mbee!! Ukishakata kiu kimbia kadili na ishu ya madaktari wetu kule jijini - acha kusuasua na issue muhimu zinazohusu maisha ya watu.
 
si unajua rais wetu ni mtalii? Amemaliza utalii wa nje ya nchi, ss ameanza wa ndani ya nchi. Huyo ndo presidoo wa TZ BWANA!

Mbona ghafla sana? Nahisi anataka kukimbia sakata la madaktari. Anamwachia pinda ahangaike nao. Pinda unali!
 
Back
Top Bottom