JK names 11 new High Court judges!!!

Suala siyo kuingia leo, ila ni kuangalia hoja

Hoja imetolewa, hujaijibu unaanza kuita watu washamba! Get serious man! We are talking about the fate of this country and the quest for justice.
 
Jamani twende mbele na kurudi nyuma tuongee ukweli mtupu wanawake wanaongoza kwa roho mbaya mbaya saaaaaaana nyie mtaona..kwa hili JK mwenyewe alikili mbona siku ya kukataa kunyanyaswa wanawake..tatizo wao wana WIVU sana na kupika majungu.Oh mala amemteua flani kwa vile yeye anapona pale ooh anamlipa fadhila maneno chungu nzima...hata maofisini kwenye huduma akienda mwanamke kwa mwanamke kuna kuwa na kamtima nyongo flani hivi wao wenyewe wanajua...kote na kila sector ukienda wanawake wana roho mbaya hata kule tunako pata moja moto moja baridi ukiwa alone unahudumiwa fresh akija mtu wako dah kipusa wakati huna hisa nae.
Nyie subilini tu yetu macho.
 
thought wewe ndio mgeni kumbe mwenyeji ila jina ndio geni

Well, issue hapa siyo mimi ni nani, ni hoja ya msingi kuhusu hawa watoa haki. Tusilaumu maamuzi mabovu kama tunatetea upuuzi wa Kikwete. hata kama anapelekewa mapendekezo na Jaji Kiongozi au Jaji Mkuu kama wengine wanavyosema, kwani usalama wa taifa wako wapi wasimshauri? Kumekuwa na maamuzi mabovu mahakma kuu kuliko hata Mahakma za chini sababu ya uteuzi mbovu wa majaji.
 
Usalama wa Taifa wenyewe mbona wabovu tu...unaweza kusema hapa Bongo kuna usalama wa Taifa??mm naona hakuna kitu hamna kitu hapa usalama wamelala fofofo kabisaaaaaaa watu wanatesa kama kawa kwa kulinga na kudai nchi ipo kiganjani ndio utasema kuna usalama hapa??
 
Sasa hilo ni tatizo kwa kiongozi mkuu wa nchi kutowajua watu anaowateua!
 
Jibu unalo. Inawezekana nia yake siyo kupendelea ila ni kutaka kuleta urari! Ila langu ni moja tu, usilete urari katika masuala ya haki maana kila watu wana priorities zao. Katika sheria wakristu wapo wengi and the ratio inaweza kuwa mwislamu mmoja kwa wakristo kumi (10%) sasa ukitaka kila ukiteua majaji wawemo waislamu kadhaa in almost equal proportion ni tatizo. Same with gender, ratio ni even worse!
Hebu Jobo tupe hizo stats zinazohusiana na idadi ya wakristo na waislamu kwenye judicial system ya Bongo maana inaonekana una idadi kamili. Kwa hiyo unataka kutwambia kutokana na Judicial system ya Tanzania kuwa incompetent, corrupt and it stinks basi asilimia kubwa wa majaji na wanasheria wakristo ni Corrupt na incompetent?? Na hii nafuata analogy yako ya judicial competence amongst Christians. Kwa sababu ukiniuliza mimi mahakama za bongo karibu zote ziko ovyo tu na sijaona maamuzi yeyote makubwa yatakayonifanya niamini vinginevyo. Karibu asilimia kubwa ya majaji na mahakimu ni watu ambao wanafanya maamuzi yao kisiasa na kujipendekeza kwa wanasiasa.
 
Hongera mheshimiwa JK kwa kuteua wanawake zaidi. Naona wanawake wana unafuu mkubwa kwenye ufisadi.

I hope JK hajateua makada wa CCM na badala yake kateua watu wenye uwezo.

Wanaume Tanzania tumechemsha mno na huenda wakati umefika wa kuwa na rais au waziri mkuu mwanamke.

Mpe hongera kwa kukumbuka na kuheshimu mchango wa wanawake tuu lakini kama ni habari ya unafuu wa ufisadi wa wanawake what about ANNA MKAPA ambae kachukia nafasi ya wanaume hamsini kwa ufisadi alioufanya
 
wANAWAKE mafisadi WAPO TENA WENGI TUU.

Hapa unaweza kuwataja mlolongo mzima mimi nataja wawili kwa vielelezo.

1.mama Anna Mkapa huyu sina haja ya kuelezea ufisadi wake.
2.Maria Kejo au Ndossi.
Huyu mama ni fisadi mkuu kwani alihusika kwenda kuwahonga watu pesa wakati wa IPTL na huyu ndio alikua mchukua pesa wa Chenge kwenye mikataba yote ya serikali.

Hivyo hoja kuwa wanawake sio mafisadi sio kweli kwani wapo mafisadi wa jinsia zote ,na hata wanaume ambao ni mafisadi wake zao pia wanahusika kwani mbona hawakusema ama kuwashauri juu ya ufisadi wao?

JK aangalie uwezo wa watu anaoteua kama wataweza kuimarisha mahakama zetu na sio kuwapa vyeo tuu ili kufikisha idadi sawa na wanaume.
 
Unajua tatizo hapa mkuu Jobo JK kaweka pamba kwenye masikio yake wananchi tunaweza tukalalamika yeye aah kimyaaaaaaaaa sasa tunadanganyana humu eti wanawake si mafisadi kama wanaume duh hii sasa kali wafuatilieni hao wanawake walio kula vitengo muone kama si mafisadi......hii unajua sawa na mtu anaye uza gari USED utasikia alikuwa anatumia mama akimaanisha kuwa halijatumika sana lakini si alikuwa anaendesha??ndo hapo sasa unamwamini mtu kumbe duh ndo soo..
 
Huo ni utetezi ambao hauna maana! Just imagine mtu anasema Jaji kateuliwa kwa sababu siyo fisadi, hivi hiyo ndo sababu?
 
Hebu Jobo tupe hizo stats zinazohusiana na idadi ya wakristo na waislamu kwenye judicial system ya Bongo maana inaonekana una idadi kamili. Kwa hiyo unataka kutwambia kutokana na Judicial system ya Tanzania kuwa incompetent, corrupt and it stinks basi asilimia kubwa wa majaji na wanasheria wakristo ni Corrupt na incompetent?? Na hii nafuata analogy yako ya judicial competence amongst Christians. Kwa sababu ukiniuliza mimi mahakama za bongo karibu zote ziko ovyo tu na sijaona maamuzi yeyote makubwa yatakayonifanya niamini vinginevyo. Karibu asilimia kubwa ya majaji na mahakimu ni watu ambao wanafanya maamuzi yao kisiasa na kujipendekeza kwa wanasiasa.

Nililiona hili swali lakini nikachelea kutoa jibu bila kufikiria. Kwa mfano, Mahakama ya Rufani kwa sasa ina Majaji wapatao kumi na watatu. Kati ya hao waislamu ni mmoja wa kutokea Zanzibar (at least kabla ya uteuzi wa mwaka huu mwanzoni ambao data zake sina). Mahakama Kuu, ukiachilia hawa majaji walioteuliwa karibuni, idadi ya Waislamu haikuwa kubwa. Kabla ya Kikwete, kati ya Majaji 30 wa Mahakama Kuu, waislamu walikuwa siyo zaidi ya watatu. Sasa hivi idadi ya Waislamu ni kubwa na wengi wao wanawachomoa kwenye Uwakili binafsi maana hawakuwepo kwenye system ya serikali.
 
Last edited:
Udini, Ukabila, Jinsia haya lazima kimoja kitakuja kutumaliza. Tatizo liko kwa raia pamoja na viongozi wao. Rais au kiongozi wa serikali anapoteua kwa kubalance au kupendelea dini, ukabila, au jinsia na siyo compitency yao hafai hata kidogo. Na raia ambaye kila kukicha ni mtu wa kulalamika kuwa huyu kateuliwa kwa sababu ya dini, kabila au jinsia na wakati haiko hivyo ni muuaji mkubwa wa taifa hili. Ingawa hayaepukiki kutokana na utashi wa watu lakini hatuna budi kuendesha nchi kufuata taratibu zilizo ktk katiba yetu.

Majaji wameteuliwa hatuna uwezo wa kuwarudisha nyuma kuwa wa kawaida au kutengua uteuzi wao ila tunachosubiri ni kuona wanachapa kazi ili kupunguza idadi ya mahabusu ukizingatia wengine wapo gerezani kwa kusingiziwa tu. Compitancy yao itapimwa na matokeo ya kazi watayo deliver kwa taifa letu.
 
Eti Mama

Kwa nini unasema hafai?

Asha

Asha, tuliza ball Suzy ana yake na yanakuja though ufisadi ni ufisadi uwe mdogo au mkubwa. Huyo alikuwa napokea rushwa ili kutoa vyumba kwa wanafunzi pale UDSM; mtu wa hivyo unamweka kwenye kundi gani?
 
Mama, ulilipishwa naye nini? Hata mimi hii niliisikia lakini ufisadi wake ni wa kiwango cha chini ingawa kama unavyosema ufisadi ni ufisadi ni ufisadi tu!
 
Udini, Ukabila, Jinsia haya lazima kimoja kitakuja kutumaliza. Tatizo liko kwa raia pamoja na viongozi wao. Rais au kiongozi wa serikali anapoteua kwa kubalance au kupendelea dini, ukabila, au jinsia na siyo compitency yao hafai hata kidogo. Na raia ambaye kila kukicha ni mtu wa kulalamika kuwa huyu kateuliwa kwa sababu ya dini, kabila au jinsia na wakati haiko hivyo ni muuaji mkubwa wa taifa hili. Ingawa hayaepukiki kutokana na utashi wa watu lakini hatuna budi kuendesha nchi kufuata taratibu zilizo ktk katiba yetu.

Majaji wameteuliwa hatuna uwezo wa kuwarudisha nyuma kuwa wa kawaida au kutengua uteuzi wao ila tunachosubiri ni kuona wanachapa kazi ili kupunguza idadi ya mahabusu ukizingatia wengine wapo gerezani kwa kusingiziwa tu. Compitancy yao itapimwa na matokeo ya kazi watayo deliver kwa taifa letu.

Ingawa waswahili wanasema subira yavuta heri, kwa kweli mimi imani na hawa wateule sina kabisa. But the reality must be said, there must be a professional criteria for which appointment to offices must be made! Ni makosa kuteua kwa ubaguzi wowote ule. For me positive discrimination must be based on competence and no more!
 
Back
Top Bottom