Jk na woga wa wagombea kutoka bara

chama cha wafu, mwenyekiti dhaifu,waziri mkuu asiyejua hata madaraka yake ni yapi,katibu mkuu kilaza

dr slaa aliwahi kusema kuwa rais jk ni dikteta mkasema ni mchonganishi sasa mnalalama nini?nendeni kwenye gazeti la uhuru mkashitaki.twanga kotekote ili tupate uhuru m4c from late ccm.vuruganeni tu.peoplez power
 
Kwa mara nyingine tena Jk amevunja katiba ya chama kwa kulazimisha maamuzi yasiofuata katiba na demokrasia ndani ya chama. Ikumbukwe kuwa Uozo ndani ya bunge la sasa imetokana na maamuzi ya JK ya kuzuia uhuru wa kugombea nafasi ya spika mwaka 2010 wakati wa uchaguzi wa spika. Sifa ya mgombea mwanamke alileta kwa lengo la kumkwepa Samwel Sita na hivyo tukapata spika mlinda mafisadi na uozo ndani ya serikali.

Safari hii wagombea wa nafasi ya mwenyekiti UVCCM taifa kutoka Bara wamezuiwa kuchukua fomu za kugombea eti nafasi hiyo ni maalum kwa watu wa zanzibar. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008 nafasi ya mwenyekiti uvccm taifa ilipelekwa zanzibar kabla ya mshindi wa nafasi hiyo kuvuliwa madaraka baada ya kutofautiana na mtoto wa Rais. Haiingii akilini kama sifa za mgombea inaweza kuangaliwa kwa mahali anakotoka, hii ni kinyume kabisa na katiba ya chama na hata demokrasia ndani ya chama. Kwa mtindo huu, ushindani ni sifuri na hivyo uwezekano wa kumpata mgombea mwenye uwezo no mdogo sana. Wanachama amkeni! chama kinazamishwa kwa maksudi.

Wengi hatutaki kujua hata habari za CCM, acha waendelee na madudu yao, sitaki kusikia herufi za C&M
 
Back
Top Bottom