Jk na Serikali yake wafisadi 50 billion 2009/2010, CAG abaini

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
499
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini ufisadi wa Sh50.6 bilioni serikalini ukiwamo wa malipo yanayotia shaka ya Sh15.7 bilioni katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010.

Katika ripoti yake ya ukaguzi iliyoishia Juni, 30, 2010, CAG amesema fedha nyingi zilitumika kufanya ununuzi bila kufuata taratibu.

Katika ripoti yake, amesema wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa, zilitumia fedha katika kipindi cha mwaka 2009/2010 kufanya ununuzi ambao haukuwa kwenye mpango wa mwaka.

Alisema matumizi hayo ni kinyume cha kifungu cha 45 cha Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 kinachozitaka taasisi za ununuzi kuweka mpango wa mwaka kwa lengo la kuepuka ununuzi wa dharura, kupata thamani ya fedha, kupunguza gharama za matumizi na kufanya ununuzi sahihi kwa njia ya kandarasi.

"Ukaguzi umebainisha kwamba katika mwaka wa fedha 2009/2010, taasisi zilizoonyeshwa hapa chini zilifanya ununuzi yenye thamani ya Sh50.6 bila kufuata kifungu cha sheria," imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kati ya fedha hizo, Sh650.7 milioni zilitumika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kununulia samani kwa maofisa wanaoishi katika nyumba binafsi

Wizara nyingine ni Nishati na Madini, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Maliasili na Utalii, Habari, Vijana na Michezo na Tume ya kurekebisha Sheria.

"Ununuzi wa samani kwa maofisa hao ulikuwa si sawa kwa kuwa hawana stahili ya kununuliwa vitu hivyo na ni kinyume cha waraka wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi) Na. C/CA/134/213/01/G/69 wa Januari 30, 2006, unaohusu malipo ya posho ya nyumba na ununuzi wa samani kwa nyumba za Serikali kwa maofisa wenye stahili," imesema ripoti hiyo.

CAG ameeleza pia kuwa eneo jingine ambalo fedha hizo zimetumika vibaya ni matengenezo ya magari ya serikali na taasisi zake ambako Jumla ya Sh176.7 milioni zimeliwa.

Alisema wakati kanuni ya 5 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005, ikitaka wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa kutengeneza magari yake Temesa (Wakala wa Ufundi na Umeme), au kupeleka katika karakana zilizoidhinishwa na wakala huyo, magari mengi yalikuwa yanatengenezwa kwenye karakana binafsi.

"Magari hayo yametengezwa kwenye karakana hizo bila kuwa na kibali kutoka Temesa kama sheria inavyotaka."

CAG amebaini pia kuwa serikali na taasisi zake imetumia Sh13.8 bilioni kulipia mali na vifaa ambavyo hata hivyo, havikupokewa au vilipokewa pungufu.

"Hii ni kinyume na kanuni ya 122 ya kanuni za Ununuzi ya Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005," alisema.

Taarifa hiyo ilisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010, wizara, idara, sekretarieti za mikoa mitatu zilifanya malipo yenye shaka yanayofikia Sh15.7 bilioni.

Malipo hayo yalikosa viambatanisho ambavyo vingeonyesha taarifa za kina pasipo kuacha shaka yoyote kuhusiana na usahihi wa malipo hayo.

Souse CAG abaini ufisadi wa Sh50 bilioni serikalini
 
2009-2010 kuna bilion 54 kanisa lilichota serikalini zitakuwa ndio hizo hizo. halafu huyu CAG yupo makini kweli namkubali ila sijasikia alipozungumzia hayo mabilioni ambayo KANISA linaibia kupitia mkataba feki. Tunaomba atoe mahesabu ya hayo mabilioni
 
@Mark bado CAG Anaendelea kuzitaja hizo ni za ikulu na ofisi zake tuu, hata mimi namkubali sana huyu bwana anaonekana mzalendo maana hii billion 50 zimelika ikulu na wizarani nadhani amefanya vizuri kutaja huu ufisadi unaomhusu mkuu wa kaya kwanza maana kumtaja mkuu wa kaya ni kama kumeza kaa la moto, hizo za kanisa bado hajazitaja ila anaendelea kuzitaja, nasubiria na zile JK alizowadanganyia wafanyakazi kuwaongezea bila kushirikisha bunge tunataka pia tujue amezipata wapi? hureeee kazi ipo mkuu
 
Back
Top Bottom