JK na EMANUEL LUHAHULA wana mgodi wa dhahabu ndani ya hifadhi ya KIGOSI wilayani BUKOMBE

Ili kuwahakikishia juu ya hili wiki mbili zilizopita baraza la madiwani la bukombe lilikwenda katika eneo la tukio na mwandishi wa habari wa mwanaharisi kuhoji uhalali wa kampuni hiyo kuwepo katika eneo hilo. Wahusika walisema mmiliki anaishi NETHERLAND na mmoja ni mtanzania ambae waligoma kumtaja. Kampuni inayojihusisha na kazi hiyo inaitwa TANCAN. Mbunge aliyepita amekuwa akionekana mara kwa mara katika eneo hilo, pia Lidhiwani Kikwete amekuwa akifika Bukombe mara kwa mara. lakini hufikia Kahama kwenye hotel ya RIVERMARK na kuigia Bukombe kwa siri. Pia hakuna kiongozi aliyehoji juu ya hili isipokuwa madiwani tu, hii ni wazi watu hawa wanahusika. lakini kwa vile liko mezani kwa mwanahalisi ukweli ujulikana tu.

Hakika inashangaza kuona kwamba muda wote huu tuna-entertain pumba za ng'ombe huyu. Kilichomo humu ni uvumi na speculation za kipuuzi ambazo hazipaswi kupewa nafasi katika dunia ya leo. Eti mtu anatoa tuhuma then anazama msituni kutafuta namna ya kuhalalisha ukweli wa tuhuma na hata hivyo anashindwa. Hakuna ushahidi wowote zaidi ya ule wa kwamba TANCAN ndiyo wamiliki wa hicho kinachoitwa mgodi na shareholders wa kampuni hiyo, nje na ndani wanafahamika. Sasa leo mtu anakurupuka na michuki yake na kuanza kuingiza jina la Rais bila hata kufanya utafiti, na kuhisi kwamba eti Ridhiwan anakwenda usiku. Hivi ana sababu ya kwenda usiku kweli wakati angeweza kutuma tu watu wakamletea mzigo huo tena akiwa sebuleni kwake Dar?

Watu wajue kwamba humu JF kuna watu werevu kuliko huyu ng'ombe na kwa hiyo anapokuja na uvumi na porojo zake watu wataona kwamba huu ni mzaha ambao haustahili hata kupewa muda wa kusikilizwa. Ifike wakati tuwe responsible kwa matamshi yetu na siyo wewe kuonekana champion kwa kujaza ma-thread ya uongo na kutafuta sifa. Kila aliyechangia humu ameona kwamba thread hii ni kamba kama lilivyo jina lake na kwa kweli huyu ng'ombe ana bahati kwamba thread hii bado inaendelea kuishi!
 
hebu punguzeni kutoa allegations zisizo na proof hata kidogo.
huu ndio u great thinker au unafiki?
hii habari inatakiwa kwenda kwenye magazeti ya udaki na sii mahali patakatifu kama humu.
 
Ng'ombe na mwenye data zaidi ni vizuri akaziweka ili nasi tupate kuchangia zaidi, kwa sasa na reserve comments zangu nasubiri data zaidi
 
Kwa kifupi ni hivi, kampuni ya utafiti ya Tancan mining ambayo ina leseni ya
utafiti katika msitu wa kigosi imeanza kuchimba dhahabu kimya kimya kwa
kushirikiana na mafisadi wazoefu katika nchi hii. Wanaotajwa katika scandal hii
ni Rostam na Ridhiwani kikwete. taarifa zisizo rasmi zinasema Ridhiwan huwa
anaenda kuchukua mzigo (dhahabu) kwa siri kutoka Bukombe nyakati za usiku.

Maswali ya kujiuliza ni je lini serikali imetangaza kuwa Tanzania ina mgodi
mwingine hata kama ni mdogo kiasi gani unazalisha dhahabu? Na ilikuwaje mpaka
Ridhiwan either mara zote au siku moja moja awe ndio mbebaji wa hiyo dhahabu
kuitoa msituni?
Ninaomba wanaoweza kufuatilia wachunguze madai haya na kuleta data hadharani. Vi inzi mpo?
 
KIGOSI




Mining Information

Minerals

The operation details are shown below:
  • Area: 109,541 hectares
  • Country: Tanzania
  • Operation type: Surface
  • Status: Exploration
  • Minerals: Gold
Ownership Information

Kigosi is owned by:
Further Information

There is no further information available for this operation.
 
News Release - June 17, 2010
Tanzanian Royalty Announces Arrival
of Gravity Plant at Kigosi Gold Project
Tanzanian Royalty Exploration Corporation is pleased to announce that a 20 ton per hour mobile gravity
separation plant has arrived at the Company’s Kigosi Gold Project in Tanzania. Initial testing has
confirmed the functionality of the plant and fine tuning will take place over the next month to optimize
performance and metal recoveries.
According to Tanzanian Royalty Senior Vice President, Riaan Van der Westhuizen, “Once the
optimization process has been completed, the bulk testing of surface gravels at Kigosi will begin in
earnest after which we expect to proceed to commercial production.”
More production modules have been ordered and these will be added to the existing plant to increase gold
output on a staged basis, he added.
“We also expect to receive two demonstration plants from the manufacturer that will be placed on the
Company’s Lunguya property. These will be used as exploratory tools to evaluate surface gravels and the
plants’ effectiveness for potential clients of the manufacturer,” Van der Westhuizen said.
For additional information regarding developments at Kigosi please visit the “Operational Updates”
section on the Company’s website at: Tanzanian Royalty Exploration Corporation - Home Page - Sun Mar 27, 2011
“Joseph Kahama”
Joseph Kahama
President, Director
F
 
Mi nafikiri mwana halisi la wiki hii, lilikuwa na habari kuhusu huo mgodi ambao umegubikwa na siri nyingi. Linaeleza jinsi mbunge wa bukombe prof kaiga walipotembea mgodi huo na wakaishia getini bila kuonana na wamiliki. Mi nafikiri kunaweza kuna na some informations, tunamuomba ngombe atupe fact
 
Napafahamu Kigosi, nishafanya kazi ya kutafiti madini mle ndani. Nchi yetu imebarikiwa sana, dhahabu iko nje nje, kuchimba mle ndani ni rushwa ya laki moja kwa saa. Unawalipa askari wanyamapori wanakuruhusu kuchimba. Mwl Nyerere alijua sana, sehemu nyingi zenye hazina kubwa ya madini alizifanya Hifadhi za taifa na mbuga za wanyama...sawa na williamson pale mwadui, aliamua kujenga hospitali kubwa pamoja na uwanja wa ndege maeneo yenye hazina ya almasi ila ****** na wajanja wenzie nasikia washabomoa uwanja wa ndege wanachimba, na hospitali iko mbioni. (****** anachimba almasi mwadui kwa ushirikiano na mwarabu anaitwa fantom ambaye pia kashirikiana nae kujenga international school mjini shinyanga). Pale kigosi niliacha mwaka 2007 wanamalizia paper works kampuni ya TANCAN (mali ya mwanasiasa wa siku nyingi, George Kahama) wapewe kuweka mgodi. Kama ****** anachimba ni kawaida, sishangai. Pale unakula kwa ushapu wako, maliasili za vipofu za kutafuna tu. Laki moja 1hr unapata mamilioni. Pia kuna ukataji wa miti ya mninga kwa ajili ya mbao, hiyo nayo dili ya wakubwa, ukitoa kitu kidogo unachana mbao na kuuza bila shida. Ndugu zangu wasukuma pale wamelala, na walioamka wamepewa kidogo dogo mambo poa. Tanzania yenyewe watu wanaishi kwa matukio, wanasahau haraka kama panzi wasi wasi wa nini? Orodha za mafisadi pamoja na mafisadi elimu zishasomwa, nini kimefata? Orodha ya wauza unga anayo rais, nini kimefata? Richmond, dowans? Meremeta? Kagoda? Kiwira? Nchi ya mapanzi hii !
 
inashangaza mpaka sasa thread ya kijinga kama hii haijafutwa. Mtu anaamka tu huko alikotoka anaandika upuuzi kabisa. Nasema ni upuuzi kwa sababu hakuna ushahidi wala maelezo yoyote yenye mantiki. Inakuwa kama anawaletea mada watu wa vijiweni. Si mbaya mtu kuleta habari, ila leta basi na proof. Lakini habari tu mara ooh riziwani anakwenda usiku kubeba mzigo ni maneno ya hovyovhoyo kabisa.
Napita tu wakuu

"lisamwalo lipo, na kama halipo basi laja" ...lazima kufuatilia undani wa hili.
 
hakika inashangaza kuona kwamba muda wote huu tuna-entertain pumba za ng'ombe huyu. Kilichomo humu ni uvumi na speculation za kipuuzi ambazo hazipaswi kupewa nafasi katika dunia ya leo. Eti mtu anatoa tuhuma then anazama msituni kutafuta namna ya kuhalalisha ukweli wa tuhuma na hata hivyo anashindwa. Hakuna ushahidi wowote zaidi ya ule wa kwamba tancan ndiyo wamiliki wa hicho kinachoitwa mgodi na shareholders wa kampuni hiyo, nje na ndani wanafahamika. Sasa leo mtu anakurupuka na michuki yake na kuanza kuingiza jina la rais bila hata kufanya utafiti, na kuhisi kwamba eti ridhiwan anakwenda usiku. Hivi ana sababu ya kwenda usiku kweli wakati angeweza kutuma tu watu wakamletea mzigo huo tena akiwa sebuleni kwake dar?


Watu wajue kwamba humu jf kuna watu werevu kuliko huyu ng'ombe na kwa hiyo anapokuja na uvumi na porojo zake watu wataona kwamba huu ni mzaha ambao haustahili hata kupewa muda wa kusikilizwa. Ifike wakati tuwe responsible kwa matamshi yetu na siyo wewe kuonekana champion kwa kujaza ma-thread ya uongo na kutafuta sifa. Kila aliyechangia humu ameona kwamba thread hii ni kamba kama lilivyo jina lake na kwa kweli huyu ng'ombe ana bahati kwamba thread hii bado inaendelea kuishi!

hizi siyo pumba, there is substence in it. Kumbuka wakubwa wanapojirimbikizia mali asili za nchi hawafanyi ki uwazi-wanajificha. Hivyo inahitaji nguvu ya pamoja wala si kumlaumu ng'ombe. Yeye kaanza na "tip"-naamini anakusanya data na ata upload punde, wakati huo huo inzi wa humu wataendelea uleta proof ukweli utakuwa wzi punde. Hakuna kinachoshindikana jf
 
Nimesoma kwenye Mwanahalisi ambapo wameeleza kuhus mgodi ambao Mbunge aliyeingia ndani gari lake lilibamizwa na lori na wakaweka picha.Sina uhakika kama ndio mgodi huo.
Mtoa taarifa atujuze kwa kina ila kuna viashiria kuwa mambo si shwari kwenye migodi ya dhahabu.
 
Hakuna mzalendo kama jk. Hakuwahi somesha mwanae nje ya nchi
riziwani alisoma masters hull university uk lakini mungu akumjalia kufaulu, kwa hiyo amerudi bila cheti. kama dr bana angekuwa anafundisha hull university basi riziwani lazima angefaulu maanake dr bana ni mwalimu mzuri sana.
 
Kweli siku ya ukombozi tutaumiza dungu zetu wengi mno. Kahama na Bukombe nawapenda kwa moyo wote.
 
Ndugu watanzania naomba mjue viongozi wetu walivyo wezi, jk na aliyekuwa mbunge wa bukombe (2005-2010) wanamiliki mgodi wa dhahabu ndani ya hifadhi ya Taifa ya KIGOSI kinyume na utaratibu. Hakuna kiongozi wa wilaya wala mkoa aliyekemea swala hilo, hata waziri wa maliasili na utalii anayetamba kusafisha wizara hiyo yuko kimya katika suala hilo.Wananchi wa kawaida wakikata kuni tu tatizo, naomba viongozi wa serikari, siasa, kidini, wanajf na wananchi wote tulisemee suala hili ili waondoke katika hifadhi hii kwa amani kabla nguvu ya umma haijawatoa kwa aibu.


Acha porojo tupatie data please!
 
Back
Top Bottom