Elections 2010 JK na CCM wameonyesha sura zao halisi

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Vituko katika kampeni za CCM na JK, vimehusisha uchochezi wa sms ambapo wamiliki wa simu walipata messages za uchochezi bila ridhaa yao. Pia CCM na timu ya JK walijikita katika kampeni za udini kinyume na matarajio ya wananchi wa Tanzania ambao wanathamini umoja wa kitaifa kama ulivyojengwa na baba wa taifa. Vituko vingine ni vitisho vya jeshi, Shehe Yahaya kutoa vitisho vya vifo vya watu watakaogombea na JK, kuwa atakayegombea na JK atakufa ghafla. Kama hii haitoshi kampeni za CCM na JK zilijikita kuwatisha wananchi ili kuwasingizia vyama vya upinzani kuwa ni waleta vita wakati havina jeshi, polisi wala green guard kama CCM. Kwa ujumla CCM na JK wameonyesha sura zao halisi kuwa hawana chembe hata kidogo ya kujali masilahi ya Tanzania na wananchi. Hata kama taifa linaangamia kwa misuguano ya udini si kitu kwao ilimradi wanajitahidi kutumia kila mbinu zisizofaa kujaribu kupata madaraka. Hii ndiyo sura halisi ya JK na CCM.
 
Noted!
 
Back
Top Bottom