JK: Msikilize Simba wa Africa Robert Mgabe akilonga

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Mugabe: Kamwe sitamwamini
Mzungu
Asema wazungu kwao si Afrika
“KAMWE sitamwamini Mzungu
hata siku moja, mweupe pekee
wa kumwamini ni yule aliyekufa,
wazungu kwao si Afrika, Afrika ni
ya Waafrika hivyo basi Zimbanwe
ni ya Wazimbabwe”
Huo ni usemi wa Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe (84)
ambao amekuwa akinukuliwa na
vyombo vya habari akiutumia kila
wakati kuonyesha msimamo
wake kwamba hababaishwi na
mataifa ya Magharibi na
hayaamini kama mataifa hayo
yana nia nzuri na bara la Afrika.
Rais huyo amekuwa adui wa
mataifa hayo kutokana na
misimamo yake ya uongozi.
Wanachokiona watu wa
Magharibi ni kwamba rais
Mugabe ni Mbale anayetumia
madaraka vibaya kwa kutetea
rasilimali za Wazimbabwe ili
zisichuliwe na Mataifa hayo ya
Magharibi.
Kwa msimamo wa Mugabe ni
dhahili kuwa Rais huyo
amedhamilia kutetea rasilimali za
nchi yake ili zisichukuliwe na
Mataifa ya Ughaibuni ambapo pia
amenukuliwa akisisitiza kwa
kusema kuwa “Ardhi ni yetu na
wala si ya Ughaibuni tumeichukua
na kuwapa watu wanaostahili”.
Rais huyo alisema hayo wakati
alipoamru wazungu wapokonywe
ardhi walikuwa wanaimiliki nchini
Zimbabwe na wapewe wazawa
wa nchi hiyo.
Msimamo wake daima amekuwa
akionyesha kwamba si sahihi kwa
mtu Mweupe kumiliki ardhi ya
bara la Afrika huku wazawa
wakihangaika hawana hata
sehemu ya kulima.
Anachoamini Mugabe ni kwamba
Afrika ni kwa ajili ya Waafrika,
msimamo wa aina hiyo umekuwa
ukimweka katika migogoro na
mataifa ya Ulaya na Marekani.
Mataifa mengi ya kiafrika
kuwapata viongozi kama Rais
Mugabe wenye kuzilinda rasilimali
za nchi zao zisiendelee
kuchukuliwa na Wazungu ni
wachache mno.
Labda Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na mfumo wa
Azimio la Arusha, yeye ndiye
anaweza kuwa mfano wa kuigwa
katika kutetea rasilimali za
Wazalendo kwa kuazisha mfumo
wa utawala wa Azimio la Arusha
ambalo lilikuwa na misingi ya
kuhakikisha Watanzania
wanafanyakazi bila kutegemea
misaada kutoka kwa Mataifa
mengine, Mwalimu aliwahi
kusema “Tanzania daima
itajengwa na Watanzania
wenyewe na haiwezi kujengwa
kwa misaada ya Mataifa mengine”
Katika bara África Rais Mugabe
peke yake ndiye anayeonekana
kulinda rasilimali za nchi yake kwa
manufaa ya wazalendo wa nchi
hiyo, ambapo ni ishara kubwa ya
kuonyesha anataka kuikomboa
nchi yake kutoka katika ukoloni
wa kiunyonyaji uchumi "Ukoloni
mamboleo" ambao Mataifa yote ya
afrika yanauhusudu na kuupigia
magoti ndio maana yanaendelea
kunyonywa kila kukicha huku
yakiendelea kuwa masikini ya
kutupwa.
Jambo la Zimbabwe kujikomboa
kutoka katika unyonyaji huu ni
jambo la kufurahia kwa sababu
uhuru huo ni Zimbabwe peke
yake ambayo imeupata kati ya
nchi zote za Afrika.
Kwa hiyo mabadiliko haya
mnatakiwa mshangilie kwa kuwa
uhuru wa nchi yenu umepatikana
na mnatakiwa kuondoa fikra
tegemezi mulizopandikizwa na
wazungu na kuwapumbaza ili
waendelee kuwanyonya rasilimali
zenu, huku wenyewe Wazungu
wakiendelea kiuchumi katika nchi
zao na nyinyi munaendele kuwa
na umaskini na fikra tegemezi.
Wazimbabwe wanachotakiwa ni
kufanya kazi kwa kutumia
rasilimali zao katika kuhakikisha
wanaondokana na umasikini
kwani bahati kubwa waliyoipata
ya kujikomboa kutoka kwa wezi
wa mchana wazungu ni bahati
kubwa mno.
Afrika imefanywa kama kitega
uchumi cha kuendeleza nchi za
ughaibuni! Afrika imefanywa ndio
sehemu ya kuchukua utajili na
kuuhamishia katika Mataifa ya
Ughaibuni! Afrika imefanywa
kama mtaji wa kuendeleza
uchumi wa nchi za Ughaibuni!
rasilimali za afrika kama vile
dhahabu, almas, ulanga, Tanzanite
nk. zimekuwa mtaji wa
kuendeleza na kukuza uchumi wa
Wazungu. Kwa mtindo huu lini
tutajikomboa kiuchumi?
Mbona hawa wazungu wanaione
sana Afrika? Tangia enzi za
zamani wanaidhulumu bila hata
kutuhurumia! Walitufanya
watumwa wakatuuza kwa
mataifa ya mbali. Hawakulidhika
na hilo wakaamua kututawala bila
ruhusa huku wakaendelea
kutunyonya.
Na baada ya kuondoka katika
harakati za kudai uhuru wa
bendera waliondoka huku
wakiwa na kinyongo ndio maana
tena wamekuja na njia nyingine
ya kutunyonya ya ukoloni
mamboleo.
Tanzania inabidi tuwe makini
sana katika mikataba na wazungu
kwani mbele itakuwa tatizo
kubwa sana maana watu
waliotoa mikataba watakuwa
wameshatoka katika sistimu na
utamwambia nani?tena kwahiyo
mikataba iangalie vigezo vya
mikataba hii kwa bila hivyo
baadae itakuja kuwa vita kubwa
sana hapa Tanzania juu ya
migogoro ya ardhi nadhani
mifano tunayo kabisa.
 
Waafrika akili zetu ndogo,Period! Nchi nyingi zina miaka ya uhuru zaidi ya 30 lakini hata huduma za msingi kama maji safi na salama ni shida. Wenzetu wa Mashariki ya mbali wamefanikiwa ilhali nao walikuwa katika hali kama yetu kwa hiyo hakuna jinsi nitawaelewa viongozi wa Afrika labda Mzee Mandela Peke yake! Nyerere alifeli,Mugabe Kafeli ,Kenyatta alifeli takribani wote wamefeli!
 
Back
Top Bottom