Jk-msijali Kuitwa Mafisadi!

Ngoma hii hapa Mh Lunyungu! Kazi kwako!
Wakandarasi wababaishaji sitaki -Kikwete

2008-05-04 10:45:16
Na Lucy Lyatuu, Singida

Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.

``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aidha, aliwataka wizara ya ujenzi wanapotoa tenda wamchague yule aliyetoa hesabu kubwa na sio kuangalia mwenye hesabu ndogo kwani wao pia ukubwa wa kazi wanaijua.

``Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali?,`` alishauri.

Aidha, amesema yapo makampuni kadhaa hapa nchini ambayo kazi yao ni kudanganya pindi wanapokuwa wamepewa tenda za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizindua barabara ya Isuna hadi Manyoni yenye urefu wa kilomita 55 baada ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kushindwa kazi kwa visingizio.

Rais Kikwete yuko mkoani humu kwa ziara ya siku sita kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka 2005.

Rais Kikwete alisema awali barabara hiyo ya Isuna-Manyoni, ilikuwa ikijengwa na mkandarasi kutoka China ambaye alishindwa kukamilisha kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kilichotokea hapo iwe ni fundisho na kwamba tatizo la namna hiyo lisijitokeze tena.

Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Kuhusu makampuni yanayodanganya alisema hapa nchini yapo kadhaa na kazi yao ndio hiyo halafu badaye huhitaji majadiliano.

``Simamieni wataalamu mlio nao, makampuni yawe yanasema ukweli kuepusha hasara katika nchi,`` alisema.

``Nchi hii ni maskini, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za wananchi, epukeni kuingia gharama mara mbili, kwani wanaofanya hivyo wanakuwa wanyonya damu,`` alisema.

Pia aliwataka kukasirika na kuwachukulia hatua makampuni yanayokiuka utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwaambia kwa herini (byebye) wakatafute tenda nyingine nje ya nchi.

Rais aliongeza kuwa mhandisi mshauri naye hatakiwi kulipwa malipo yake endapo ujenzi hautakuwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwani wasipofanya hivyo Tanzania itakuwa shamba la wajinga.

Lazima Watanzania waone uchungu na kutekeleza miradi ya wananchi katika kiwango kinachotakiwa, alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Bw. Omar Chambo alisema barabara hiyo itagharimu kiasi cha Sh. bilioni 30.43 na ujenzi wake ulisainiwa Desemba 11, mwaka 2007.

Alisema barabara hiyo ilisainiwa kati ya TANROADS na Kampuni ya China Geo Engineering kutoka nchini China na kwamba sehemu ya barabara hiyo inatarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2010.

Alisema mradi huo unasimamiwa na mhandisi mshauri Black &Veatch kutoka Afrika Kusini akishirikiana na Kampuni ya Mak Consult ya Tanzania kwa gharama ya Sh. milioni 857.23.
  • SOURCE: Nipashe
Kutokana na hotuba hii..Mh Rais haamini kwamba kuna ufisadi bali lawama ni wakandarasi na si viongozi wetu wanaotoa tenda!

Yuko upande wa vijisenti!?

Ufisadi ni msamiati wasioulewa!?

At the same time pambio ni ile ile .."Sisi ni Masikini!?"
 
Kutokana na hotuba hii..Mh Rais haamini kwamba kuna ufisadi bali lawama ni wakandarasi na si viongozi wetu wanaotoa tenda!
Yuko upande wa vijisenti!
Ufisadi ni msamiati wasioulewa!
At the same time pambio ni ile ile .."Sisi ni Masikini!"

Huku Singida kuna nini ? Mbona hii habari za Rushwa ikifika huko Viongozi wanakuwa mbogo .Huko ndiko Mkapa amewahi kuomba ushahidi akiwa jukwaani juu ya rushwa.Maana walisema kuna rushwa na hasa kwenye barabara akasema ni majungu wampe ushahidi pale pale .Leo JK anatamka haya .Kuna nini kule ?
 
Kwa ufupi hotuba hii ya rais ina maana pamoja na nyingine..Zifuatazo..

1)Rais anaweka wazi kuwa wanaopiga kelele za ufisadi ni wale waliokosa
tenda!

2)Kwamba hakuna kitu kama UFISADI!

3)Kwamba vijisenti haviwatoshi MAFISADI!

4)Kwamba tatizo sio mafisadi bali vijisenti zaidi vya wananchi kuendelea kuwalipa zaidi mafisadi!

5)Kwamba watanzania wako kwenye delusional thinking etc etc!

6)Kwamba nchi ni masikini!

7)Kwamba Chenge na wenzake wasijali kuitwa mafisadi kwani "Boss Mkuu yu pamoja nanyi!"

Kwamba nimesikia kilio chenu cha kuonewa na kuitwa mafisadi na kwa sababu ya wivu wao nawaongezea vijisenti licha ya kwamba sisi ni masikini?

Ndugu yangu this is sooo crazy!
 
Mods inasikitisha sana kuona kwamba suala hili nyeti kwa wananchi limepewa kauli ya "Kibweka cha Mkubwa" ama "Vibweka vya Wakubwa"
Hivi si vibweka ni issue nyeti Mods na ningeomba muuangalie upya uamuzi/maamuzi wenu/yenu!
Shukran.
Jmushi1
 
Kazi ipo, huwa napata pressure mara tu mtu atamkapo Rais, nikiangalia vita hivi naona si rahisi, juzi nimeona kwenye blog ya michuzi jinsi mkuu anavyopokelewa na mamia ya wananchi! najiuliza, wananchi wanampendea nini??? mbona si wa kufanyiwa hivyo??tutalalamika wee, tutaandika, tutasema kila kitu, mwisho wake waliofumbuka macho ni asilimia 20 na waliofumbwa macho asilimia 80, kazi hipo,si ndogo,elfu mbili na kumi tukitaka mabadiliko na mapinduzi tusiishie kuandika hapa tujaribu na means nyingine za kuwafikia wananchi, lakini pia najiuliza mbona vyama vya siasa vingi vya kisanii??? .NATAMANI VYAMA HIVI VISIPATIWE RUZUKU, ILI WANACHAMA NA WATAKAOJIUNGA NA VYAMA HIVYO WAWE KWELI WAMEDHAMIRIA,WACHANGIE NA WAPIGANE, WAJITANGAZE SIO KAMA SAA HIZI WAKAE WAJITANGAZE PESA IPO!!Sijui kama niko sahihi?
 
Umasikini ndugu yangu!
Umasikini! Rais akiingia pale na mikwala na force ya wanausalama pamoja na mbwembwe nyingi za kiitifaki!Wananchi na njaa zao wanaona ni Mesiah ameshuka! Viongozi wetu wana exploit hilo!
Ni issue ya kisaikolojia!
Tunahitaji kampeni kubwa na mabadiliko ya katiba pamoja na uongozi!
 
IMG_9143.JPG

Hii ndio siku Mh Rais alipotukejeli sisi wananchi wake kwa kuwaambia mafisadi wasijali! Hii ni huko Singida juzi tu!
Hebu tizama hao wananchi hapo mbele walivyopigika!
Hata nguo si unaona HAWANA na hawajui hata kinachoendelea wao wanaona kama ni movie flani hivi na actor ndo huyo!
Maybe wanafikiri watapewa chakula ama kazi!
Maybe kwa sababu hawana kazi,chakula na labda elimu then huyu ni Mungu mtu aliyekuja kuwakomboa!
Swali hapa ni je ujumbe alioutoa uliendana na adhira?
Je alikuwa akiwatisha wananchi ama alikuwa akiongea na wakandarasi?
Hii ni siku alipowaambia kuwa wao ni masikini!
Hii ni siku aliposema mafisadi wasijali gharama!
Is this JK'S WORST SPEECH OF ALL TIMES?
Hapo
 
Huyu mumuitae rais a.k.a Rahisi hachagui maneno ya kusema si nyumbani wala ugenini, hapo ndio utakapojudge busara yake na uwezo wake wa kutuongoza, sijui hiyo 2010 itafika lini?? Ila wabongo walivyo vipofu + viziwi watamrudisha tena madarakani, hapo ndio nitakapokuwa na kila haki ya kufumba macho na kuikana Tz ili niishi kwa amani!
 
Jk msitegemee kama anaweza akawa na muarubaini wa kupambana na ufisadi, tazama yeye ni namna gani ameendesha mchakato wa ushindani ndani ya chama chake, njia aliyoitumia kwa kiasi kikubwa ilikua ni ya kifisadi na ndiyo iliyomwezesha kushinda tusitarajie anaweza akawa kinara wa kupambana na ufisadi, ukimya wke niliutegemea, na mafisadi ndio waliokuwa ngazi yake ya kupandia alipoingia madarakani
 
Kutokana na hotuba hii..Mh Rais haamini kwamba kuna ufisadi bali lawama ni wakandarasi na si viongozi wetu wanaotoa tenda!
Yuko upande wa vijisenti!
Ufisadi ni msamiati wasioulewa!
At the same time pambio ni ile ile .."Sisi ni Masikini!"

kwnye hiyo hutuba yake(SEHEMU ULIZO BOLD)inaonekana kabisa Bwan mkubwa akijichanganya mwenyewe lbda hakusoma hiyo hutuba kabla ya kuisoma na kuona ina makosa.
Huwezi kutoa tenda kwa mkandasi mwenye kiwango(hesabu)kubwa alafu baadae useme peasa hizo zisichezewe kwani ni kodi za wananchi
 
IMG_9143.JPG

Hii ndio siku Mh Rais alipotukejeli sisi wananchi wake kwa kuwaambia mafisadi wasijali! Hii ni huko Singida juzi tu!
Hebu tizama hao wananchi hapo mbele walivyopigika!
Hata nguo si unaona HAWANA na hawajui hata kinachoendelea wao wanaona kama ni movie flani hivi na actor ndo huyo!
Maybe wanafikiri watapewa chakula ama kazi!
Maybe kwa sababu hawana kazi,chakula na labda elimu then huyu ni Mungu mtu aliyekuja kuwakomboa!
Swali hapa ni je ujumbe alioutoa uliendana na adhira?
Je alikuwa akiwatisha wananchi ama alikuwa akiongea na wakandarasi?
Hii ni siku alipowaambia kuwa wao ni masikini!
Hii ni siku aliposema mafisadi wasijali gharama!
Is this JK'S WORST SPEECH OF ALL TIMES?
Hapo

Mods mbona mumeiondoa ile picha ya JK alipokuwa akihutubia huko Singida?
Vipi wakuu mkuu kapenyeza rupia ama?
Maana naona ile thread ya MKJJ ya kutoka ahera sio kibweka lakini hii ni kibweka na inapigwa vita?
 
Inaelekea viongozi wetu wako dunia nyingine kwani maelezo katika hotuba zao zinaonyesha KIBRI cha hali ya juu na DHARAU.Ni vyema wakasoma alama za nyakati. Hii ni karne ya 21 na upeo wa watanzania kuelewa mambo sio ule wa miaka ya 60. Watu wamechoka na ni vyema wakafahamu mtu aliyenyanyasika na mbaye hana cha kupoteza, akishachoka basi hapo ujue kazi ipo. Hicho ni kizaazaa. Viongozi chukueni haya kama tahadhari. Tuendako ni kubaya na wasije kulaumu kuwa hawakuonywa. Viongozi jifunzeni kuongea busara kama hamuwezi basi nyamazeni. Msitutukane wananchi.
 
Kweli Jk Is Out Of Touch.haelewi Hata Wananchi Wake Wanahisia Gani Kuhusu Neno Fisadi.inatisha.kwahiyo Tusemeje Tuendelee Kumwekea Mantiki Kicwani Mwake I Mean How Can We Make Sensitive To The Issue Of Fisadi?anatukebehi.he Is Sensitive In A Very Negative Way-hataki Kulisikia Inamuuma Sana.marafiki Wake Wa Karibu Wote Wanaondoka Kwa Ufisadi.birds Of Feathers....

Kunakucha,kanu I Wapi,unip I Wapi,je Zanu Pf? Taka Usitake Kutakucha Jk.wafadhili Wanakudanganya.ya Kibaki Hakuwa Kipenzi Chao??
 
Very tru! Kuna wanaofikri kuwa anajaribu!
Mimi bado kuona!
 
Very tru! Kuna wanaofikri kuwa anajaribu!
Mimi bado kuona!

Mkulu.
Leo nimeenda TRA asubuhi kuchukua kadi yangu ya gari ambayo baada ya kulipa yale ma demurrage charge na macharge mengi tu ambayo hata kuyaelewa ni shida tu....nimefika ofisini nikaambiwa yule kijana aliyekuwa akishughulikia kadi yako yuko kwenye kikao rudi baadaye

Nimeenda tena pale baada ya masaa mawili nikaambiwa jamaa ameshatoka na hatarudi tena mpaka kesho.

Swali langu ni, je huu uzembe wetu kila mara tunautafutia sababu mara ajira ni ndogo mara mishara ni midogo tumlaumau JK?

Angalieni Malawi nchi masikini zaidi yetu,mishara midigo lakini wanvyochapa kazi utastaajbu
 
Hii issue nayo kweli ni mzigo!
Hata mimi huwa napata shida sana pale napokuja nyumbani kusalimia na kuona jixsi taifa letu limelala!
 
We unategemea nini wote mliolala mko huko nje mnasoma tuuuuu!!! hammalizi.
Kazi atafanya nani?
tulo Tz tunasoma tu jambo forum.
mrudi nyumbani na nyie mtufundishe kazi zinavyofanywa.
 
We unategemea nini wote mliolala mko huko nje mnasoma tuuuuu!!! hammalizi.
Kazi atafanya nani?
tulo Tz tunasoma tu jambo forum.
mrudi nyumbani na nyie mtufundishe kazi zinavyofanywa.

Maneno mazito haya Dada Haika!

Ni kweli tunatakiwa turudi nyumbani mara baada ya masomo!

Ila inabidi tupiganie mazingira bora ya kidemokrasia na pia kampeni nzito na yenye kuhitaji moyo ili kuweza kuwaelimisha wananchi kuhusu Taifa lao na njia sahihi za kusimamia haki zao pale inapokuja kwenye maendeleo yao na utajiri wao.

Ni kweli inatakiwa turudi nyumbani na kuanza kazi ya ujenzi wa taifa! Ila hilo viongozi wetu hawaoni ni muhimu.

Kwaniaba ya wale wote wenye kuguswa na ujumbe huu ninashukuru!
 
Ila Mods nina ushauri wa bure!
Thread hii si propaganda bali kauli hakika ya raisi ambayo nina data za kutosha kuweza kuitafsiri jinsi kwa jinsi nilivyofanya pamoja na vielelezo ambatanishi vya evidence za kauli hizo!

Kutoka kwenye Jukwaa la kisiasa hadi kwenye issue hii kuitwa kibweka cha mkubwa..hadi sasa kuwa ni hoja mchanganyiko tu!

Hii issue ni current! Na watu wako inerested! Kwanini usiwape uhondo ili nao wachangie kwasababu hakuna spin?

Kama wamechukizwa kwanini hao wawakilishi wa rais wasije hapa kuprove otherwise?

Ama maneno ya Jaji Warioba yana ukweli hadi hapa kwenye chombo chenu hiki cha kihistoria?
 
Ni kinamna hapo ametujibu kuwa hii kelele ya mafisadi haimkeri! Kwa maneno mengine ni kama kelele ya mlango kwake, hivyo haimkeri! Kuanza na maneno mengine haimaanishi kuwa hiyo statement ilikuwa ni by the way tu! Inawezekana hiyo ndiyo iliyokuwa message kubwa! Si unajua naye anaogopa kuandamwa! Mimi nasema huyo na Masisadi lao ni moja! Mtu aliye serious unamwoma hata kwa usoni! JK haonekani kama haya mambo kwake ni serious! Ninachomsikitikia ni kwamba 2010 inakaribia sana na hii habari ya kuishi kwa mazoea kwamba tutashinda hata tukiweka jiwe (au mbwa), itawashangaza! Anatakiwa kusoma alama za nyakati! Je, anadhani Lowassa aliwahi ku imagine after only two years atakuwa hapo alipo! Anyway, we dont need to alert JK! All we need is to have him out and get someone more serious, who can actually start by asking what JK did or did not with hawa Mfisadi! Kwa sababu nadhani sasa inabidi watu washitakiwe si tu kwa waliyoyafanya (actions) bali pia hata kwa ambayo waliyanyamazia wakati walitakiwa kuyafanya (omissions). Mzee Mwinyi tutamsamehe wa sababu ya uzee, lakini huyu JK itabidi akimaliza muda wake aulizwe kwa nini ulifuga Mafisadi? Na hilo ni kosa kama ufisadi wenyewe kwa sababu hata mmoja wa hawa mafisadi akifa kabla ya kurudisha pesa, taifa litapata hasara sana!
 
Back
Top Bottom