Elections 2010 JK mhubiri hodari asiyejua akihubiricho (amekurupuka kwa hisia tu)

harrysonful

Member
Oct 27, 2010
34
0
Hali hii kweli inashangaza kabisa. Ungelitegema JK na CCM kwa kile wanachokiita ni wazoefu wa utawala wangelikuwa mstari wa mbele kusema "YOTE YANAWEZEKANA" lakini wao sasa wamekuwa mstari wa mbele kudai "YOTE HAYAWEZEKANI." Hili linashtua ...sana kwa Chama kinachodai ni mbunifu wa njozi ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" kwa CCM kukiri hadharani kumbe hakina program ya kutuletea neema hizo ni kuwadanganya watanzania kuhusu maisha bora ili wapate kura tu kisha wapotee kula maisha bora wao. OK>>Dr. Slaa na Chadema kwenye Ilani yao ya uchaguzi wamesema elimu bure hadi kidato cha sita inawezekana lakini Jk na CCM wanasema hizo ni njozi...........Sasa CCM inafikiri "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" inayopigia kelele kila kukicha yatatoka wapi kama elimu haitakuwa bure? OK>>Dr. Slaa na Chadema wanasema afya bure inawezekana lakini JK na CCM yake wanasema hapana........Sasa CCM inafikiri "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" yatatoka wapi kama afya haitakuwa bure? je maisha bora kwao ni nini haswa??? OK>>>Dr. Slaa na Chadema wanasema vifaa vya ujenzi kuondolewa kodi ili kumpunguzia mwananchi gharama za ujenzi na hivyo kuongeza kasi ya ujenzi wa makazi ya raia na kuachana na nyumba za tembe ambayo ni maisha ya kifukara,,lakini JK mhubiri mkubwa wa maisha bora kwa kasi mpya sijui tena sasa kwa hari zaidi yeye anasema haiwezekani hata kidogo na wanakuja na vihunzi vya EAC....Sasa sijui JK na CCM wanaelewa wanachokihubiri "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"? Je bila makazi bora maisha bora yatatoka wapi kama vifaa vya ujenzi vitaendelea kuwa ghali? OK>>>Dr. Slaa na Chadema wanasema ya kuwa pesa za kutoa huduma hizi zote zitatoka katika kufuta misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa ambao wanatumia mianya ya kifisadi kutochangia maendeleo ya nchi hii. Mifano wanayotoa ni pamoja na misamaha ya kodi ya zaidi ya Tshs 700 bilioni kwa wachimba madini wakubwa...CCM na haswa JK wanasema hilo hapana tutafukuza wawekezaji na hivyo kuthibitisha ya kuwa CCM ni "wataalam wa falsafa ya haiwezekani wakati wakihubiri wasichokitenda wala kukielewa" Dr. Slaa na Chadema mwishowe wasema "TANZANIA BILA CCM YAWEZEKANA na KUENDELEA KUWA NA CCM NI KIAMA" lakini JK na CCM wanang'aka haiwezekani....kwa hiyo CCM inafikiri "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" yatatoka wapi kama JK na CCM yake ambayo ni "Dr. No" wataendelea kukwamisha maendeleo kwa kuhubiri wasichokijua?????? TIRED OF LIES... NADHANI KAPUMZIKENI MTAFAKARI KAULIMBIU ZENU NA MNAYOWAWAZIA WATANZANIA

MHARIRI WA KUJITEGEMEA........harryson.johnson@yahoo.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom