Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 752
Tatizo kubwa sana na ambalo linanikera katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne, ni Mawaziri kuongozana na vyombo vya habari kila anakokwenda ili apigwe picha, na habari yake iandikwe ili Rais aone kwamba jamaa anafanya kazi.
Sasa matokeo yake ni kwamba, unakosa cha kuzungumza, unazungumzia Mawaziri kutoanikwa hadharani kama hawajalipa kodi ya maji, halafu inageuka kuwa ishu ya kujadiliwa magazetini, mtandaoni na kwenye redio. Wastage of time and resources.
Waziri mwenye akili akitembelea mtambo wa maji wa Ruvu Chini au Juu, anatakiwa ajiandae kuwaambai Watanzania mipango ya Serikali juu ya kuwaondolea wananchi tatizo la maji, bajeti iliyopo,wafadhili, matarajio ya baadaye na kadhalika. Give out a constructive speech. Kutoka Dar mpaka Ruvu amechoma mafuta ya Serikali, kuna posho za watu alio ongozana nao, madereva na waandishi wa habari. Halafu, kwa gharama zote hizo, Profesa mzima unatoa hotuba ya kitoto namna hiyo mpaka hata mtoto wa shule anahoji kauli yako.
Ni heri kukaa kimya ukaonekana mwerevu hata kama sivyo ulivyo.