JK: Mafisadi hatutawaonea haya

Yeye mwenye ni fisadi, aanze kujishughilikia yeye mwenye kwanza kwa kuwa yupo kwenye list of shame aliyoitaja Rais dr.Slaa tena anacheza no.11 Huyu Fisadi Kikwete, na hizo barua wanazopeana je na yeye huyu Fisadi Papa Kikwete atapewa

list of shame ushaifanya ndo gospel.common dont you have common sense.
Haya lets assume naye ni fisadi though i dont beliave,the man is a presdent of Tanzania how do you deal with that or you think one bright morning he announce,'nimegundua nami fisadi so naachia ngazi wilbroad will take ma chance as a prez,'that is the way you think,man growup
 
Ivuga, najua hizo ni habari za magazeti Nipashe in particular. Si vibaya kuvuta subira na kuona what will happen baada ya haya mapumziko. So far source yetu haiko available na hakuna kitu significant jana na leo zaidi ya hii info ya JK.
Huyo Raisi wenu(Si rahisi wangu) mpuuzi tu asijionee haya mwenyewe basi, sababu na yeye ni fisadi ,mwizi mkubwa. Kwa nini watanzania ni rahisi sana kudanganyika???
 
Huyo Raisi wenu(Si rahisi wangu) mpuuzi tu asijionee haya mwenyewe basi, sababu na yeye ni fisadi ,mwizi mkubwa. Kwa nini watanzania ni rahisi sana kudanganyika???

we mkenya nawe huna point keep kwayati
 
Siku Kikwete akijikamata na kujitia msalabani nitaamini ameshughulikia mafisadi. Maana mchawi anayetafutwa na JK na CCM si mwingine isipokuwa Kikwete mwenyewe na genge lake na familia yake.

Najua ataendelea na ahaa muache mzee Mkapa apumzike jamani. Ahaaa niache mimi na Salma tupumzike jamani. Ahaaa niwakamate hata Edward na Rostam wawezeshaji wangu wakuu! Looo! Nimkamate hata mwanangu Ridhiwani!
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu. Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.

Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu. Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu. “Ujasiri wa Rais wetu ni ujasiri aliopewa na Mwenyezi Mungu pamoja na dua tunazomwombea, tunaomba kujivua gamba huko kuwe kwa ukweli na kusiishie hapo tu,” alisema Askofu Ndegi.

Baada ya kumaliza kusema hayo, Askofu huyo aliomba maaskofu wengine waliokuwepo ukumbini kumwekea mikono Rais sehemu waliko na kumwombea dua ya kumpa ulinzi, ujasiri na hekina katika uongozi wake.

Lakini Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini na kuwataka wananchi kuvumiliana baina ya watu wa dini mbalimbali na kutowasikiliza watu wanaohubiri habari za udini kwa lengo la kutaka kuleta mafarakano nchini. Tamasha hilo ambalo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, lililenga kuchangisha fedha za kusaidia yatima, watu wenye ulemavu na mahitaji kwa wanawake wasiojiweza.

HabariLeo
 
Sasa kinachoshangaza na kusitisha magamba yanavuliwa kwa ubaguzi. Kuna haya magamba hayajavuliwa:
Kuna chama kilichotumia pesa za epa kama 40m hakijavua gamba
Kagoda haijajivua gamba
Dowans sijui
Mali za umma zimetaifishwa na chama fulani cha siasa (mf Kirumba)
Isije akawa tunatafuta mchawi, eti triplets peke yao.

Tusije tukadanganyana:yawn:
 
Hataweza kujikana mwenyewe. Kwani kwenye list of shame yupo. Wasipoangalia wanajimaliza wenyewe. Na vita ya nzige..........................,....,
 
..ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo
Honestly speaking Nape amabebeshwa mzigo amabao JK anagepaswa kuubeba ...Kuzunguka mkoa kwa mkoa ...ku jusfy .. kampeni ya kujivua gamba..

Nape ..sasa ndio kioo ..anaonekana kama yeye ndio injini ya kujivua gamba ...No Kikwete apite kila shina la chama chake afafanue na kujieleza...Kama anahuo ujasiri!!.... Ni mchakato mzito ..kutuma wajumbe kama Nape na wenzake... Mwenyekiti wa chama Hii ndiyo kazi yake ...au mwenkiti ana agenda nyingine??
 
Ngoma inogile!

Inawezekana JK akafanya kweli kama alivyosisitiza?
Anaposema "Haki Itatendeka" ana maana gani? isije ikawa ni kiini macho.

Haki itendeke kwa namna gani? Naomba tusidanganywe na kauli mbiu ya kujivua gamba kwani toka lini nyoka anapojivua gamba sumu yake ikapungua?nachojua kutokana na elimu ndogo niliyonayo kujivua gamba kwa nyoka ni kujiuwisha upya uwezo wake katika makali ya sumu.
ninamaana gani? JK hawezi kuwataja wengine wajivue magamba kwni yeye ndiye sumu namba 1,fisadi namba moja ni yeye mwenyewe ushahidi tunao aanze yeye na familia yake ndipo sumu itakuwa imepungua makali otherwise mkono wa Mungu uko juu yake.Enough is enough tumezulumiwa vya kutosha,tumeonewa vya kutosha sasa lazima tupambane.
 
binafsi naamini anafahamu fika watz wa leo sio wale wa 1995,so anafahamu madhara ya kauli za namna hii "HATUTAONEA HAYA MAFISADI" mbaya zaidi wananchi wanawafahamu wote..tunasubiri tuone
 
DSC03348.JPG


Rais ameridhika na barabara iliyojaa mchanga namna hii?
Hata Zebra crossing haionekani .... .....

Anajishaua tu miaka 6 tangu wauza unga awape muda hakuna kilichotokea itakuwa hii ya rafiki zake?
 
The problem ni kwamba tunaye RAIS MSAHAULIFU, nakumbuka alishawahi kusema kuwa MAFISADI WANA NGUVU SANA. sasa tujiulize, nguvu ya kuwashughulikia amepata kutoka wapi? Namwambia NAPE amwandikie barua na yeye fisadi mkubwa huyo!
 
Asante JK kwa msisitizo wa Kuweka MAGAMBA pembeni.

CDM wanaweweseka kwa vile sauti yao siku zote ni kuituhumu CCM na UFISADI, sasa CCM imeonyesha ujasiri wa kuondokana na magamba, CDM wanagwaya. Kila chama kina style yake ya kutekeleza maamuzi ya vikao vya juu, NAPE kapewa kazi maalum ndani ya chama, nyie msio wana CCM yanini kulalamika kuwa JK alipaswa kufanya kazi ya anayoifanya NAPE kuzunguka mikoani kutoa mrejesho maazimio ya NEC. JK anashughulikia masuala ya kiserikali wakati akina NAPE wanachanja mbuga mikoani kurudisha imani kwa wananchi kuhusu CCM pia kuvunja ngome za CDM.


CCM kutenganisha na UFISADI inawekena!!
!
 
JK ana viroja kweli.
Yeye huwa anaangalia na hadhira gani anayoongea nayo ili aifurahishe. Sijui hiyo haki itatendeka vipi ikiwa yeye atabaki kuwa Mwenyekiti wa chama chake. Ni vipi JK ataweza kujihukumu yeye binafsi huku akiwa madarakani? JK anapaswa na yeye kuachia ngazi ili chama kijisafishe maana hata yeye ni GAMBA.

Akitoka hapo, akionana na hao mapacha watatu atawaambia kuwa haki itatendeka na hakuna wa kuwaonea ndani ya chama na serikali. Sasa hapa sijui anamchezea nani!!
 
Asante JK kwa msisitizo wa Kuweka MAGAMBA pembeni. CDM wanaweweseka kwa vile sauti yao siku zote ni kuituhumu CCM na UFISADI, sasa CCM imeonyesha ujasiri wa kuondokana na magamba, CDM wanagwaya. Kila chama kina style yake ya kutekeleza maamuzi ya vikao vya juu, NAPE kapewa kazi maalum ndani ya chama, nyie msio wana CCM yanini kulalamika kuwa JK alipaswa kufanya kazi ya anayoifanya NAPE kuzunguka mikoani kutoa mrejesho maazimio ya NEC. JK anashughulikia masuala ya kiserikali wakati akina NAPE wanachanja mbuga mikoani kurudisha imani kwa wananchi kuhusu CCM pia kuvunja ngome za CDM.

CCM kutenganisha na UFISADI inawekena!!
!

NEC hawakuazimia kuwapa watu siku 90 na wala hawakuazimia kuwatosa RACHEL sasa Nepi amepata wapi maagizo ya kuwahadaa mapacha watatu yaani RACHEL na kuwapa siku 90 wakati kikao cha NEC hakikuazimia hayo?
 
Hivi TAKUKURU na mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) wako kazini kweli au taasisi zao zimevunjwa? Au inawezekana mikataba yao ya kazi haiwaruhusu kuchunguza madai ya rushwa na ufisadi ndani ya CCM. Mimi naona bora mkoloni arudi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom