JK: Machinga Complex itoeni kwa wauzaji wa "used spares"

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Jamani nimekuwa nikimsikiliza Mkuu wa Kaya miaka kadhaa iliyopita pamoja na wasaidizi wake wakijitapa kuwa wamewatafutia wafanyabiashara wadogo suluhisho la kazi zao kwa kuwajengea Machinga Complex iliyotarajiwa kutumiwa na wale wafanyabiaashara waliopo ilala na kwingineko!!

Nilishamsikia Mkuu huyo huyo wa Kaya akaiahidi kwamba sehemu kama hizo zitajengwa katika kila Wilaya ya Dar es Salaam!

Miaka takribani miwili sasa tokea ujenzi wa machinga Complex ukamilike! na kama sikosei uzinduzi ulishafanyka...kwa hotuba za mbwembwe za kisisiemu!! Lakini Machinga bado wapo pale Karume...Ilala sokoni na mitaani!! Hakunha mtu wa kwenda kufanya bioashara Machinga Complex!! Waliopo pale bado wanatandika bidhaa zao nje ya jengo!!

Mimi najiuliza hivi Mkuu wa Kaya anashauriwa na nani? Je ni kazi ya jiji au Wizara husika kuhakikisha pesa za walipa kodi zilizotumiaka kujengea Machinga Complex zinatumika kihalali?

USHAURI: Leo nimewaza kuhusu wauzaji wa "used spares" wao hawana shida ya kutembeza biashara zao, weny emagari watawafuata tu popote walipo! Hebu basi hiyo Machinga Complex itoeni kwa wauza spares chakavu.....labd aitatumika vizuri!!

Nawasilisha
 
kweli mkuu ni bora wakapewa hawa jamaa wa spares za magari maana lile jengo litaoza bila hata kuludisha hela yetu.
 
NADHANI LILE JENGO LILIJENGWA KISIASA ZAIDI, KWA HIYO KUHAMISHA KUSUDIO LAKE LA AWALI NI KUPOTEZA MALENGO YAO:director:
 
Back
Top Bottom