Kabla hamjalalamika kwa nini rais anasafiri nje, someni undani wa anayokwenda kuyafanya huko nje. Rais huwa anapata mialiko mingi, mingine anawakilishwa, na mingine anaamua kwenda mwenyewe. Sasa mlitaka awakilishwe tu kila mahali? Ikiwa hivyo kutakuwa hakuna sababu ya kumwalika rais kwenye shughuli yoyote, watu wangetuma tu ujumbe ikulu kwamba wanaomba mwakilishi. Kama analoenda kufanya ni kinyume au ni nje ya majukumu ya urais ndipo tulalamike. Naomba mtu yeyote mwenye ushahidi kwamba anachoenda kufanya JK huko Ufaransa ni kinyume au ni nje ya majukumu ya rais wa nchi alete ushahidi huo hapa tuujadili. Hebu tujaribuni kudhibiti hisia zetu katika masuala kama haya. Yaani kwa kuwa hapo nyuma kumekuwepo madai kwamba rais anasafiri sana nje (pengine yana ukweli, sijui), basi kila safari aifanyayo tuilalamikie na kuitilia mashaka? Ni lini basi rais atasafiri nje nasi tuone amefanya sawa kusafiri? Tumkosoe rais inapobidi, lakini tupunguze ushabiki usio na msingi kama huu wa kuona kwamba kila safari anayofanya eti anenda "kula nchi". Jamani, tuangalie pande zote.
Kwa ufupi naomba ushahidi au hoja za kuthibitisha kwamba kwa kwenda Ufaransa leo, JK amefanya jambo ambalo ni nje au ni kinyume na majukumu yake ya urais.
Kwa ufupi naomba ushahidi au hoja za kuthibitisha kwamba kwa kwenda Ufaransa leo, JK amefanya jambo ambalo ni nje au ni kinyume na majukumu yake ya urais.