JK, Kwa nini muadilifu LOWASSA asiwe naibu Waziri Mkuu!

Dah,inahitaji moyo kumtetea mtu mwizi'''nlazima uwe umehongwa wewe.

Hivi kwa akili yako unaona lowasa msafi? Ile kusema kwamba wewe mwenyekiti ulikua unajua kila kitu ndo kunamfanya kuwa msafi? Hivi hauoni kwamba alichosema ni kwamba tuliiba na tuliiba wote,sio peke yangu? Hata kama aliyafanya maamuzi mabaya ,hafai kuwa kiongozi kwa kusingizia eti alifanya maamuzi mabaya wa kulazimishwa na mwenyekiti/rais.Angejiuzulu basi kama aliona maamuzi anayoenda kuyafanya sio sahihi.Leo hii zile Billion 113 tunazodaiwa na Dowans ni zao la Richmond,Richmond ni zao la aidha maamuzi mabaya au rushwa ambayo huwezi kumtenganisha huyo bosi wako lowasa.

Bwana Jumakidogo endelea tu kulipwa hizo hela za lowasa,manake anazo nyingi kweli tangu alizoiba kule AICC,Zifaidi kidogo walau.

Huwezi kutoa hukumu bila ya ushahidi kwa kutumia zahania. Wekeni ushahidi hadharani mtu achukuliwe hatua. Acheni majungu ya kishabiki.
 
22

Dr slaa anafaa zaidi kwa nafasi hiyo sio Urais

hivi unaelewa kilichowekwa kwenye hoja au umekurupuka? slaa emetoka wapi? akili ya mtoto wa slaa aliyezaliwa juzi juzi ndio inaweza kulinganishwa na hao magamba kwa akili zao za sasa za ukubwani usimfananishe Dk slaa na nafasi hiyo labda mrema
 
EL anafaa kuwa president, sio unaibu waziri mkuu.
EL hafai kwa lolote.... KAMBARAGE alishasema hatupeani uraisi au uwaziri mkuu kwa kigezo cha urafiki au uswaiba. kama wewe EL ni rafiki yako au swaiba wako mwite nyumbani kwako mnywe naye gahawa, chai, cocoa au hata jackdaniely mkipenda na siyo kupigiana debe la uongozi wa taifa letu hapa jamvini kibaraka mkubwa weee.
 
Huwezi kutoa hukumu bila ya ushahidi kwa kutumia zahania. Wekeni ushahidi hadharani mtu achukuliwe hatua. Acheni majungu ya kishabiki.
kama unataka ushaidi nenda kule tume ya maadili ya viongozi omba file ambalo lina taarifa za utajiri anaomiliki hapa tz na zile nchi zenye tax holiday na umtake akupe maelezo ya namna alivyozipata pia ujiulize kwa nini kina nyerere, sokoine, kawawa,Abood jumbe familia zao ni za kilala hoi mpaka leo zinatunzwa na serikali - mind you brother you can not full all the people all the time - dawa yenu imeshachemka subirini kunyweshwa tuu.
 
Unaonekana mbunifu sana wa hoja. Hayo yako hewani. Tunataka ushahidi wa kumtia mtu hatiani. Matajiri wengine hamuwaoni. Umetekwa zaidi na mambo yanayojadiliwa vijiweni. Unachokizungumza hapa ni sawa na riwaya ya kubuni.
 
Mheshimiwa katika moja ya mambo ambayo ulipatia sana baada ya kuingia ikulu ni kumteua EL kuwa PM. Jamaa anapiga kazi zaidi ya punda ni kuzunguuka nchi kwa ajili ya kuwaamsha waliolala kama farasi. Nadhani hoja zake kuhusu RICHMOND zimeeleweka vyema ndo maana hakuna jeuri yeyote aliyesimama kupingana naye. Kwa kuwa aliacha u PM akiwa bado anafaa. Mpe unaibu Waziri Mkuu ili amboost mwana wa mkulima. Miaka ya nyuma kidogo nadhani unakumbuka. Kuna mtu alikuwa anaitwa Mrema. Aliwahi kupewa nafasi hiyo na mambo yakawa murua kabisa. Nadhani huu ni ushauri mzuri zaidi ya ule wa kutia saini sheria ya muswada wa mchakato wa katiba mpya wenye mapungufu.

Atakubalije na yeye ni Rais miongoni mwa wafuasi na wapambe wenzake?
 
Unaonekana mbunifu sana wa hoja. Hayo yako hewani. Tunataka ushahidi wa kumtia mtu hatiani. Matajiri wengine hamuwaoni. Umetekwa zaidi na mambo yanayojadiliwa vijiweni. Unachokizungumza hapa ni sawa na riwaya ya kubuni.

Swali hilo kamuulize Wilson Mukama pale ofisi ndogo Lumumba. Yeye ndiye ngariba katika jambo hili
 
Ni yule jamaa anayeshukiwa kwa mchezo ule?

Kila mtu ana imani yake na kuamini kile anachoona yeye kinafaa. Kama kaona EL anafaa hayo ni mapendekezo yake. Nyie tatizo lenu nini? Mnataka kutumia udikteta wa mawazo? Hatuwezi kuwa na upande mmoja tu. Mawazo yetu na itikadi zetu zinatofautiana man.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom