Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,899
- 4,623
Kesho kutwa ndio sikukuu ya wafanyakazi ijulikanayo kama mei mosi. Kama ilivyo ada mkuu wa nchi huwa ndie anaealikwa kuwa mgeni wa heshima na ikitokea ana shughuli nyingine humtoma mmoja wapo wa wasaidizi wake kumwakilisha. Tofauti ya mwaka huu viongozi wa wafanyakazi poamoja na kutangaza mgomo utakaoanza tarehe tano, pia waliapa kutomwalika kiongozi yeyote wa serikali katika sherehe hizo ikiwa ni pamoja na rais wa nchi. Swali langu ni je msimamo wa wafanyakazi bado upo pale pale? Na kama upo pale pale mgeni wao wa heshima ni nani? Au walishabadilishwa msimamo kama ilivyokuwa enzi za kina Mpangala? Wasi wasi huu unasababishwa na kawaida yetu waTz kulamba chenga nyingi lakini goli halifungwi. JF kuna update gani kuhusu hili?