JK kutengeneza Mabilionea 100 watanzania 1015, New York

I have always find our President with many "good intentions" ila utekelezaji ndio unakuwa kimbembe...Mshabiki wa Maathir..sawa.Kamleta hadi Dr ..wa Gramin bank...sawa.
Hakuna impact so far. Ni kuzungushana tu.
Mipango bila utekelezaji ni kazi bure. Mh Rais ange concetrate kwenye vitu vichache ambavyo vingeleta impact mf madini ,elimu na afya.
Sasa ukishika kila kitu halafu usitoke na kitu ndio inakuwaje?
Maisha yanazidi kuwa magumu kila siku!
 
wazo hapa labda ni kuinua kiwango cha maisha cha watanzania. Ila sioni ni sahahi kama raisi wa nchi anakuwa na mkakati wa kuinua uchuki wa watu 100 tu kati ya watanzania milioni 40.

Hayo mawazo hata yakifanikiwa itakuwa ni kama zile pipi zinazotengenezwa na maprofesa wa mazingaombwe. Kwa sababu kuwa na mabilionea 100 wakati mamilioni ya watanzania wana maisha ya utata sio jawabu la matatizo ya nchi. Kama mabilionea 100 watasaidia watanzania wote wawe na huduma za uhakika za afya, wawe na elimu bora (na walimu bora) na makazi bora, kuwe na ajira zinazoeleweka na kiwango cha maisha kinachoridhisha basi huo mpango utakuwa poa!
 
lakini kama ndoto ni kuwa na mabilionea wa kuandikwa magazetini basi huo utaalamu wa kulenga shabaha ni ziro!!
 
wazo hapa labda ni kuinua kiwango cha maisha cha watanzania. Ila sioni ni sahahi kama raisi wa nchi anakuwa na mkakati wa kuinua uchuki wa watu 100 tu kati ya watanzania milioni 40.

Hayo mawazo hata yakifanikiwa itakuwa ni kama zile pipi zinazotengenezwa na maprofesa wa mazingaombwe. Kwa sababu kuwa na mabilionea 100 wakati mamilioni ya watanzania wana maisha ya utata sio jawabu la matatizo ya nchi. Kama mabilionea 100 watasaidia watanzania wote wawe na huduma za uhakika za afya, wawe na elimu bora (na walimu bora) na makazi bora, kuwe na ajira zinazoeleweka na kiwango cha maisha kinachoridhisha basi huo mpango utakuwa poa!

Ukitengeneza mabilionea 100 kama Mengi, tayari umetengeneza maelfu ya kazi, tayari umewapa vijana kibao ajira, tayari umeongeza fuko la TRA, tayari umeongeza uwezo wa serikali wa kujenga shule na hospitali, barabara nk.

Job creation ndio itakuwa solution ya matatizo ya Watanzania. Serikali pekee haina uwezo wa kutengeneza kazi za kutosha. Sector binafsi ndio jawabu. Kuanzia mabilionea wachache mpaka wenye kampuni za kusafisha ofisini. Kwa pamoja uchumi hujengeka na taifa kuendelea.

Tusiogope kuwa na mabilionea kama akina Mengi, ni jambo zuri kwa taifa kwani kila anapotumia yeye kuna maelfu wengine watafaidi. Mbaya ni hii ya kuwa na watu wanaotoa pesa nje na kuwaacha Watanzania vijiweni bila ajira.
 
LOL! Watanzania tulitongozwa na JK,tukaingia line 80%!!!!....then a year and a half later we realise that the fellow is not so good in bed!What do we do now?? heheheheh....

Jamani,hata kutengeneza mabilionea 100 lazima ikasemewe Marekani??

Anyways,this is my observation,come 2010...turn out ya wapiga kura itakuwa the lowest ever.Sioni nani(wachilia wapi) ataweza kuisawazishia CCM kwenye haya madudu yake.Hawana mtu wala namna ya kuwachomoka humu.This government has no spin doctor,maana huu ndio wakati wenyewe wa kuwa na mtu kama huyo.Kama hata swali la mtoto wa sekondari linashindwa kujibiwa na PM,kisa eti atakuwa anaingilia uteuzi wa Rais,si ni uchizi huo jamani!Ni dhahiri kuwa hata JK mwenyewe lazima ata feel kuwa he has been let down by his government.If he doesnt feel that,then we are in much bigger problems than we thought!
Huku anataka kumtema PM wake,pressure kutoka kwa ex presidents imekuwa kubwa ya kumtaka amteme PM,je ana ubavuuu, how does he do it? Karamagi naye ndio hivyohivyo tena na wengine wengi tu.
 
JK hakikisha kwanza mianya ya rushwa inazibwa, mikopo inatolewa kwa uwezo wa mfanyabiashara sio wa kuhonga. Tenda zinatolewa kwa uwezo wa kampuni kiutendaji na sio Tenda za Lowasa ( Richmond).

Lazima uhakikishe Elimu inapewa kipaumbele kikubwa, iendane na ushindani wa kisasa wa kibishara pamoja na technologia.

Huwezi kuwa na uchumi imara bila kuimarisha elimu. Lazima warudishe scholarship kwa uwezo wa mwanafunzi kwenda nchi mbalimbali na kuwavutia kurudi nyumbani kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kazi na biashara.

Check and balance, hii ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi viongozi wetu lazima wajue wanafanya kazi kwa ajili ya nani na kwa nini?

Wape wananchi uwezo wa kufanyakazi, walipe kama mnavyowalipa wageni. Wape wafanyabiashara wa ndani uwezo na wathaminiwe katika kazi zao.

RUSHWA BABA ITAKUMALIZA WEWE NA MAWAZO YAKO.
KULINDANA HILO NI JIPU KUU.
KUKUMBATIA WAGENI WABOVU NA WATOA RUSHWA WAKUBWA.
SIONI KAMA UNAPINDUA KWA LOWASA,RO NA MASWAHIBA WAKO WENGINE.
 
Wanatia aibu kwanza walianza kugawa pesa kama njugu wakafikiri uchumi utakuwa kwa kutoa pesa matokeo yake inflation ilipanda na kukaribia 2 digits sasa anafikiria kuwa na billionares ambao wanadhulumu mali asili ya WTZ ili anapoondoka madarakani aseme tumeweza kuwa na 100 billionares. What a stupid idea? Mikataba yote ifutwe ambayo haina maslahi kwa WTZ halafu ndio tuanze kuona nini cha kufanya.

JK anaka kujenga taifa la omba omba na mafisadi kama yeye ambao wanakomba mali asili ya wazawa bure.
 
Ingawa nakubaliana kinadharia na Mtanzania kuwa mabilionea 100 watasaidia kuunda ajira, si lazima mabilionea wote wa TZ wawe wajasiriamali kama alivyo Mengi. Kwa mfano si uwongo kuwa Lowassa ni bilionea (kwa shilingi za Tanzania) lakini ameajiri wangapi? Hawa mafisadi walioficha fedha zao Mauritius wameajiri wangapi? Nadhani serikali ingekazania basics, kama vile kuboresha elimu, madawati na vyoo katika shule zetu, huduma nzuri katika hospitali zetu na kuinua maisha ya wakulima, hapo wanaweza kusema kuwa wamejitahidi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania ifikapo mwaka wa uchaguzi 2010. Lakini hizi dana dana za New York zitaendelea kuwa poroja tu.
 
muungwana anatuletea usanii wa ze comedy....serikali mbovu washauri wabovu watendaji wabovu nani atakuwa na imani na hii mipango yake mengine mibovu..ni bora kwenda kusikiliza mama na mwana kuliko huu usanii
 
Ingawa nakubaliana kinadharia na Mtanzania kuwa mabilionea 100 watasaidia kuunda ajira, si lazima mabilionea wote wa TZ wawe wajasiriamali kama alivyo Mengi. Kwa mfano si uwongo kuwa Lowassa ni bilionea (kwa shilingi za Tanzania) lakini ameajiri wangapi? Hawa mafisadi walioficha fedha zao Mauritius wameajiri wangapi? Nadhani serikali ingekazania basics, kama vile kuboresha elimu, madawati na vyoo katika shule zetu, huduma nzuri katika hospitali zetu na kuinua maisha ya wakulima, hapo wanaweza kusema kuwa wamejitahidi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania ifikapo mwaka wa uchaguzi 2010. Lakini hizi dana dana za New York zitaendelea kuwa poroja tu.

Jasusi,

Tunataka mabilionea wazalishaji na sio wezi wa mali za umma na ndio maana nikatumia mfano wa Mengi.

Kuboresha elimu na afya ni sawa lakini utaboresha vipi wakati huna pesa? Ndio maana ni muhimu mno kuanza kwenye uzalishaji kabla ya kuingia kwenye matumizi.

Lengo letu la baadaye liwe ni kuwaondoa watu wengi kutoka kwenye kilimo badala ya sasa asilimia kama 70 ili ije chini ya asilimia 40 na wengine wote waingie kwenye uzalishaji na services.

Bado naamini kwasasa nguvu kubwa tuweke kwenye job creation kuanzia kwenye manufacturing, services, kilimo mpaka serikalini.

Tukiongeza idadi ya wafanyakazi ikawa mara mbili ya sasa, basi faida yake itaonekana kila sehemu kuanzia kwenye huduma kama elimu na afya mpaka hata kwenye security kwa kupunguza vibaka mitaani.
 
Wezi wa fedha za umma wa Dunia ya 3 wakiiba wanajenga nyumba za thamani kubwa kuzidi thamani ya juu ya nyumba. Yaani wana over expend kwenye ujenzi na kutia nakshi lukuki bila sabau za msingi.

Nyumba nyingi za wezi wetu zina thamani kubwa unnecessarily. Sikatai, kujenga nyumba nzuru ni zuri, lakini kuendelea kudhani nyumba kali kupindukia ni maendeleo ni ujinga wa hali ya juu ni majuha tu ndo wanshabikia jambo hilo.

Nyumba ya kuishi famila moja inayogharimu TSHS 1 Billion mikocheni ingeweza jengwa Magomeni na kuwa na uwezo wa kupangisha familia 10 kila famili ikiwa na vyumba 3 vya kulala.

Nyumba hiyo ya magomeni ingetatua tatizo la nyumba na kuwa na uhakika wa kuingiza fedha kila siku,pia kwa vile fedha ni ya wizi ingeweza punguza mzigo kwa wananchi wa kawaida walau by 10% kwa kuwasaidia makazi bora.

Ukichukua majengo 500 yaliyojengwa huko Mikocheni na Beach zote za Tanzania na kuyafanya nyumba kubwa za kupangisha wananchi wa kawaida, majengo hayo 500 yangeweza geuzwa nyumba za kupangisha familia 5000 hayo yangeweza itwa maendeleo.

JAmbo jingine:

Kuna mitambo ya viwanda complete set inayo gharimu $150,000 tu lakini inafanya kazi muhimu sana kama kukamua mafuta kutoka mbegu mbali mbali, kusindika vyakula kama maziwa nyanya na matunda, Kutengezea siagi, Cheese na Raw materials za Ice cream, kutengezea makopo ya bati na plastic, kurecycle karatasi za aina mbali mbali, kutengenezea mapambo, mabomba ya baisikeli na pikipiki, vifaa vya nyumbani kama frame za milango na madirisha vitasa kufuri,visu mabakuli na vyombo vya udongo.
Mitambo hii ingeweza tawanywa kila pembe ya Tanzania na kuajiri watu kwa maelfu na hata kupunguza utegemezi wa kila kila kitu kutoka nje.

Waheshimiwa wakisha iba fedha akili zinawaruka zaidi ya kununua magari ya kifahari na nyumba za kifahari wanaanza kuota namna wawezavyo funua sketi ya kila mwanadada na kujikidhi hamu ya kiibilisi.

Wizi ungeelekezwa katika investment tungelalamika kwa staili nyingine kabisa si hii ya kuwaona wezi wamekosa uzalendo na Utanzania. Ieleweke,Sishabikii wizi.
 
NI vizuri kufanya mpango mmoja ukaumaliza kuliko ukaanza yote ushindwe kuimaliza. lakini pia unapomaliza mmoja unakupa nguvu zaidi ya kuanza ule unaofuata.

Kupanga mipango mingi bila utekelezaji kuonyesha mwelekeo, kunamchanganya sana Jk. muda nao hausubiri, unakwenda kwa spidi ya Jet. Sasa haelewi lipi ni kipaumbele na lipi lisubiri. Mara wajasiliamali, mara mabilionea 100, mara maisha bora kwa kila mtanzania, mara ajira milioni moja, mara mkukuta n.k. ili mradi nchi inapelekwa as if haina dereva. hakuna umoja tena ndani ya serikali, kila mtu anafanya vile anavyoona inamfaa yeye binafsi.

Badala yake sasa wamebaki kujikusanyia pesa kupitia safari za mikoani ili kukusanya pesa za kuhonga wapiga kura miaka mitatu ijayo kwa kisibgizio cha kuelimisha wananchi kuhusu bajeti. halafu Waziri anadiriki kuwaambia wananchi wasihoji gharama ya ziara zao. kweli serikali inafikia hatua hiyo? huyu ndiye waziri anayemwakilisha Rais ambaye anaumia sana na umasikini wa Mtanzania. Rais naye anaona sawa kawakilishwa vizuri. Mbeya wakiimba Mapepe, mapepe atawalaumu? Tusubiri na huko Tukuyu na Kyela, labda watamheshimu Mwandosya kama atakuwepo maana ndiyo silaha yako pekee ya kukuokoa Nyanda za juu.

Zinduka Ndugu yetu, zinduka, sisi ndiyo marafiki zako tunaokueleza ukweli wa mambo. mbona umesahau tulikuwa wote vijiweni ukiwa waziri (nje) na ulionyesha ungeweza? nini kimekusibu sasa mshikaji wetu?, au ngoma yao tamu kuliko mdundiko wetu tuliouzooea? wenzio tumebaki midomo wazi tusiweze kuamini kwamba umaarufu wako unapotea kwa kishindo mfano wa kura zako!!! Hao wanakuambia mzee unapendwa wanakudanganya. mambo yamebadilika sana, mawaziri wako wanazomewa mikoani, bado huzinduki? kwani haya ulishayazoea au kuyaona huko kabla?

Rekebisha serikali yako, ondoa the karamagis, unda serikali makini na safi, kama huna wasafi azima hata upinzani, weka vipaumbele vichache muhimu vissible kwa wapiga kura wako unavyoweza kuvimaliza kulingana na uwezo wa serikali yako, angalau utakuwa na la kujibu 2010.

Angalia usije ingizwa kwenye historia ya kuwa Rais wa kwanza kuiua ccm. yetu macho lakini hatutaacha kukoromea.
 
Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).

Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.

Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR
Good point FDr, Now can you take a time and defend JK? Tell me what Mr president anachoona ambacho wananchi hatuoni? Hiki sio kiini macho, useme unaweka shilling 10 inageuka million 10, haya mambo yanakuwa na plan, strategies, short term and long term goals. Huwezi kuamka asubuhi ukasema unataka kuongeza list ya mabillioner? How is the question that will rise in any intelligent thinker.

What make Mr Jk to believe he will change this overnight? Utakubaliana na mimi JK ameshajua fika kwamba mchezo umekwisha na matokeo ni kwamba amefungwa. JK alipoingia madarakani alikuwa over confidence, na mimi nikiwa mmoja wa mshabiki mkubwa wa bwana JK kwamba sasa ni mabadiliko time. Challange yakwanza ni pale alipo muweka EL kwenye uwaziri mkuu, nikasema mzee kachemsha lakini mapambano ya ukombozi yanaendelea. Zikaanza kuzuka balaa kwenye killa kona na hapo ndio bwana JK alipo kubaliana na Mwalim kwamba Ikulu si mahala pa mchezo mchezo.

We're in globalization generation, this time need globol oriented president and not Ujamaa or popularity oriented president. Tunaitaji rais mwenye best decisions, rais ambaye ataongoze nchi kwa best interest za wananchi na sio ma patner wenzie.

Jk ameweza kuzikimbia scandals nyingi sana tangu alipo ingia madarakani, kuanzia Richmond, mpaka BOT. Muheshimiwa ameonyesha weakness nyingi sana kwenye uongozi, kuanzia kushindwa kuwakemea wana CCM wenzie wanapoendesha Bunge kwa manufaa yao wenyewe, vile vile ameshindwa kusafisha corruption kwenye cabinet yake. Muheshimiwa raisi ameshindwa kutumia cheo chake cha kuajiri na kufukuza baada kuendelea kuwakumbatia watu kama karamangi na wengineo.

Muheshiwa, ameendeleza tabia yake ya ukinyonga... kwa kusema hili nchini, na kusema lile pindi awapo kwenye nchi za wadau. Serikali ya muheshimiwa imezidi kuzitumia fedha za walipa kodi pasipo kujiuliza, hii ni pamoja na unnecessary misafara ya muheshiwa na wapambe wake. Muheshimiwa, amendeleza kufanya Tanzania kuwa kama nchi ya kifalme kwamba kama wewe ni king then wanao wana enough credentials kuwa viongozi wa sector nyingine. Vile vile muheshimiwa ameajiri baadhi ya washauri wake kutokana na kujuana na sio resume, hii imesababisha Tanzania kuendelea kuseffer katika kila sector.

Mwisho... Muheshimiwa ameonyesha kuchanganyikiwa, kutolewa tena his jod duties.
 
Mtanganyika,

Nakubaliana na mengi uliyoandika kwa sababu matendo ya JK hayaonyeshi kama ana uwezo wa kufanya anayoyasema.

Ambapo sikubaliana na wewe ni kuhusu wazo lenyewe kama linawezekana. Ndio linawezekana na ndio kitu kilichotakiwa kufanywa toka enzi ya Mkapa na sasa JK. Lazima kipau mbele kiwe kuwawezesha Watanzania kuanzia wafanyabiashara wa chini, kati na juu.

Inatakiwa kubadili mindset za watanzania kutoka kwenye imani ya kwamba serikali itafanya kila kitu na sasa kuwa tutafanya kila kitu na serikali inaweza kusaidia tu kusukuma gurudumu letu ambalo tayari liko kwenye motion.

Bahati mbaya mpaka sasa kwasehemu kubwa ni maneno matupu na hakuna matendo.
 
JK kutengeneza Mabilionea 100 watanzania 1015, New York

Rais Jakaya Kikwete amesema huu ndiyo mpango wake hata kama atakuwa ametoka madarakani, mazunguzo haya yalifanyinka nchini marekani katika ziara yake ya mwaka huu Sep.2007,

akimkabizi muheshimiwa R.Mengi kazi hiyo ili kuweza kutafuta pesa za kuwasaidia wafanyabiasha hao ambao wata saidia wengi kwa kiasi kikubwa, kwa mimi niliona nimpango mzuri sana tuweze kuwa na watanzania mabilionea na kushika sehemu muhimu za uchumi wa nchi yetu ikiwa nipamoja na madini, utalii, elimu, na nyingine zilizoka Tanzania.

Muh. Mengi aliuliza pesa atapata wapi JK akamuwambia sijui nikazi nimekupa,

pesa hizo zitakuwa zina kopeshwa wafanyabiashara kwa vikundi na ni kiasi kukubwa na siyo pesa kidogo,

Rais aliongea kwa uchungu akisema uchumi wetu umeshikiliwa na wageni wakati sisi hatuna kitu,
katika safari yake hii haikuwa na wafanya biashara wakigeni kwasababu wao hawana shida na safari kama hizi

kwawale wanao jua hii habari zaidi basi watanisaidi kuongezea haya ndiyo ninayo kumbuka tu.

asanteni
Matokeo yake akaamua kuweka Tiles hadi kwenye mashamba ya mihogo huko kwao Msoga !
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom