JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa?

Status
Not open for further replies.
Nini linalomsababisha JK asichague wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya??Je nini kilichopo Ikulu???Je situnanyimwa haki yetu ya kikatiba??
 
Siyo lazima achague wakuu wa Wilaya wapya kama waliopo wanafaa......
Kwani Katiba imesema hivyo kwamba kila baada ya uchaguzi uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa unabidi ufanyike?
 
Siyo lazima achague wakuu wa Wilaya wapya kama waliopo wanafaa......
Kwani Katiba imesema hivyo kwamba kila baada ya uchaguzi uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa unabidi ufanyike?

Wewe nae jaribu kuelewa muanzisha thread anamaanisha nini... sio kurukia tu... Jamaa anazungumzia mikoa mipya kama Katavi,Geita na Njombe (na wilaya zake) bila kusahau Dar Es Salaam.

Sasa wewe unakua kama unakimbizwa.
 
Viroba mchezo!!!!
 
Tatizo maswahiba atawachaguaje wote?pili hiyo pesa ya kuanza mikoa na wilaya mpya ipo?na ukizingatia Dowans wapo mlangoni wanataka pesa yao.tatu hizo pesa huko hazina zipo? na ahadi alizotoa kwa wananchi atazitekelezaje we hauoni hapo ni patamu kiaina?
 
Wewe nae jaribu kuelewa muanzisha thread anamaanisha nini... sio kurukia tu... Jamaa anazungumzia mikoa mipya kama Katavi,Geita na Njombe (na wilaya zake) bila kusahau Dar Es Salaam.

Sasa wewe unakua kama unakimbizwa.

Katavi, Geita, Njombe, Simiyu haina budget mwaka huu inaanza rasmi July 2011!! Atateu tu tumpe nafasi. Nadhani anataka atuteulie wakuu watakao tupa utumishi uliotukuka
 
Mojawapo ya sababu ni UKATA. Kubadilisha Watumishi kunahitaji Fedha. Nchi yetu kwa sasa haina fedha kwani wahisani waligoma kuchangia bajeti 2010/2011. Kwa sasa hivi Wizara nyingi zina hali ngumu sana na hakuna fedha. Nyingine zimepunguziwa bajeti kwa zaidi ya 70%.
Kwa mantiki hii si wakati muafaka kuongeza gharama nyingine.
Hata fedha ya barabara nadhani sasa inatumika kuendesha mambo ya utawala badala ya kujenga barabara maana hakuna fedha. Na nadhani ni sababu mojawapo iliyomfanya Magufuli kuanza kupiga kelele kuhusu mabango na road reserve ili mradi tu asikike yupo maana hana miradi ya kukariri kichwani na kutaja kama kasuku... ili aonekane anajua na anafanya kazi!!!
 
Kutokana na ukweli kwamba bajeti ya nchi imekwama, serikali haina pesa, mikoa mipya na wilaya mipya zimeongezwa. Kuna uwezekano wa Wakuu wa mikoa na wilaya waliopo kuendelea mpaka JK atapomaliza kipindi chake cha mwisho bila kufanya uteuzi mpya.
 
Pinda alisema watatangazwa mwezi May pale watakapokamilisha taratibu za mikoa na wilaya zote mpya. Alisema kwa sasa wale waliopo wachape kazi tu. CCM chiniiiiiiiiiiiii mmh samahani juuuuuuuuuuuuuuu
 
Ni vema, ikachukua muda kuwatangaza hao Ma-DC na RCs huku system ikiwa inafanya kazi yake ya vetting ili kuwapata watu makini, hususani vijana wenye uwezo wa kufanya kazi. Tumechoka na maneno mengi bila vitendo.:embarassed2:
 
habari nlizozipata jamaa kamaliza kuandaa orodha yake tayari kwa kusomwa hadharani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom