JK kutangaza idadi ya Watanzania Desemba 31, 2012

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,291
24,167
18 September 2012
Matokeo ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyikia hivi karibuni yanatarajiwa kutangazwa na Rais Jakaya Kikwete Disemba 31, mwaka huu katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka.

Akitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mahusiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Said Ameir, alisema hatua iliyopo kwa sasa ni upelekwaji wa makabrasha katika ofisi za kuhakiki takwimu zilizopo kibaha (Data Processing Centre) kwa ajili ya kuzihakiki sambamba na utoaji mafunzo kwa wahusika watakaoshiriki kuhakiki takwimu hizo na zoezi la kuhakiki litaanza Octoba 1, mwaka huu.

Alieleza kuwa vijana watakaofanyakazi kuhakiki takwimu hizo wameanza mafunzo juzi na watapata mafunzo hayo kwa muda wa miezi miwili na baadaye kuanza kuhakiki takwimu hizo.

“Zoezi kwa sasa limekamilika kwa asilimia mia, awali lilikamilika kwa asilimia 95, hivyo makabrasha yaliyotumika katika zoezi hilo kwa sasa yanapelekwa Kibaha kwa ajili ya “Data Processing” (Uhakiki wa takwimu),” alisema Ameir.

Alisema matokeo ya takwimu hizo zitatangazwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka ambapo atatangaza idadi kamili ya watanzania lakini kutakuwepo na utoaji wa taarifa nyingine ndogondogo mara kwa mara hadi mwaka wa fedha 2014/2015.

Ameir alisema taarifa za uchambuzi zitakazoendelea kutolewa kila wakati baada ya Rais Kikwete kutangaza ni pamoja na taarifa za uchumi wa watu, umri wa watu katika makundi mbalimbali, ongezeko la watu katika mikoa na wilaya, taarifa za walemavu, viwango vya elimu, idadi ya vifo vya watoto, wajawazito na watu wote kwa ujumla na taarifa kuhusu afya hadi mwaka wa fedha 2014/2015.

Zoezi hilo la sensa nchi nzima lililoamza usiku wa Agosti 25 kuamkia Agosti 26, mwaka huu lilikumbwa na changamoto mbalimbali lililopelekea kuongezewa muda wa siku saba.

CHANZO: NIPASHE :: IPPMEDIA
 
Rais kutoa matokeo ya takwimu sio sahihi. Ofisi ya Taifa ya Takwim (NBS) ndio walitakiwa watoe matokeo ya sensa pamoja na maelezo ya vipengele vilivyotumika wakati wa sensa. Pia NBS (kwa kutumia matokeo ya sensa) walitakiwa watoe tafsiri ya sensa hivyo kwa kila segment waliyohesabu.

Sijui rais anaingiaje hapa. Mara kadhaa watu wamekuwa wanasema Magogoni kuna upungufu kwenye safu wa washauri, wanatumbukiza kwenye mambo ambayo si ya office yake. Unless kama rais ni 'statistician vinginevyo alitakiwa naye apate report toka NBS including hicho tunachosema tasfiri ya vile vipengele vilivyotumika kuhesabu watu.
 
Ni yeye anayeamuru sensa ifanyike na ni yeye anayetangaza idadi ya watu kwa kindi maalumu anafanya hivyo kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge ya takwimu nadhani ya mwaka 2002 pia ya 2012 kifungu cha 1
 
Back
Top Bottom