Jk kushitakiwa kwa kuvunja katiba.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Hivi kweli Kikwete anavunja maudhui ya katiba akiwa na macho makavu!! Mawaziri kwa mujibu wa katiba, I stand 2 b corrected, lazima watokane na wabunge. Na ili utambuliwe kama Mbunge lazima uwe umeapishwa na Speaker.

Kikwete yupo juu ya Katiba. Anateuwa mbunge na papo hapo anamteuwa kuwa waziri, maana ni kwamba kampa mtu uwaziri kabla hajawa mbunge! Tujadili

Chini ya ibara 55 (4 ) kuhusu Uteuzi wa Mawaziri inasema Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wabunge, ibara 68 inasema 68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.
 
Ndio mana kuna mahali watu wamehoji, je bw. Jk ataitisha bunge la dharula? Hata wasaidizi wake hawakuliona hilo? Anyway mh. Wetu yupo juu ya kila ki2, hopeful haitakuwa big deal kwa kuwa ni tanzania
 
hayo ndo maamuzi ya baba Mwanaasha. Hata hukumu ya Mahanga nayo ni uchuro tu.
 
hajavunja katiba yoyote kwasabab hawawezi fanya kazi mpaka waapishwe na bunge kwanza.
 
Hivi kweli Kikwete anavunja
maudhui ya katiba akiwa na
macho makavu!! Mawaziri kwa
mujibu wa katiba, I stand 2 b
corrected, lazima watokane na
wabunge. Na ili utambuliwe
kama
Mbunge lazima uwe umeapishwa
na Speaker. Kikwete yupo juu ya
Katiba. Anateuwa mbunge na
papo hapo anamteuwa kuwa
waziri, maana ni kwamba kampa
mtu uwaziri kabla hajawa
mbunge! Tujadili


Chini ya ibara 55 (4 ) kuhusu
Uteuzi wa Mawaziri inasema
Mawaziri na Naibu Mawaziri
wote watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wabunge,
ibara 68 inasema 68. Kila
Mbunge atatakiwa kuapishwa
katika Bunge kiapo cha uaminifu
kabla hajaanza kushiriki katika
shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika
uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.

Mkuu hata kumshtaki Rais nako ni kuvunja Katiba, usisahau hilo, unless ulimaanisha awe "impeached" na Bunge!
 
Mimi katiba siijui kabisa, ila nadhani kuna vifungu vinavyompa nguvu hio. Ninazo point 2. Kwanza uteuzi alipoufanya vyombo vya habari vilinukuu na vifungu vya katiba vinavyompa mamlaka hayo kuteua. Pili kulikua na msisitizo kwamba" UTEUZI HUO UNAANZA MARA MOJA. Sasa walio na hio katiba hebu kipitie hicho kifungu cha katiba (angalia taarifa za uteuzi wa siku hio) halafu mtujuze
 
Back
Top Bottom