JK kumuokoa Jairo na Luhanjo?

Who cares kama JK kawaomba wawe wamoja kwenye hiyo sakata ya Jaro na Luhanjo.......wenyewe wawe wamoja pamoja na dola yao lakini NGUVU ya UMMA always PREVAILS. Kama ni kweli JK kawaagiza wabunge Magamba kuwa kitu kimoja, hapo atakuwa anamwaga petroli kwenye moto.
 
Hilo nalo neeno. Km ni kweli lakini. Na km kweli ametoka alikotoka kuja kuwatetea wahalifu.
Nkosa cha kuongea, lets wait
 
Ndugu zangu tusiangaike na issues ndogo kama za Jairo na Luhanjo jambo muhimu wakati huu ni mchakato wa kuandika katiba mpya. Hii mambo ya Jairo ni ndogo sana,kwanza Pinda na Jk wangekua makini wangekwisha maliza hii maneno ya Jairo siku nyingi. Nchi yetu ni ya ajabu sana,bunge linashupalia issue ndogo kama ya Jairo wanashindwa kushupalia jambo nyeti kama mchakato wa katiba mpya ambao kama tunapata katiba nzuri kesi za akina Jairo tutazipunguza sana.

@timbilimu, nakubaliana na wewe kwamba issue kubwa ni katiba. Lakini hebu tutafakari vizuri, kama Rais anafanya juu chini ili wezi (EPA) na watoa hongo kwa chombo cha kutunga sheria ili wapindishe mambo (Jairo) iweje leo CCM wanataka tumkabidhi rais huyu huyu mamlaka ya kusimamia mkachakato wote wa katiba kuanzia kuteua wajumbe, hadi kupitisha mapendekezo? Ana uadilifu gani mpaka tumpe hilo jukumu?

Kesho inaweza kuwa siku nzuri sana maana Spika Makinda atakuja amejiandaa (well ameandaliwa) kufunika kombe mwanaharamu apite. Shida JF iko macho, watanzania watajua yote!
 
Raisi JK ameingia Dodoma kwa ndege asubuhi ya leo. Kwa muda huu inasemekana yupo ktk kikao na wabunge wote wa CCM ktk ukumbi wa Pius Msekwa.

Moja ya ajenda ya kikao hicho ni kushinikiza wabunge wote wa CCM wawe kitu kimoja hapo kesho ktk kuchangia ripoti ya tume iliyochunguza sakata la Jairo. Riport ya Jairo inategemewa kujadiliwa kesho Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Mkuu Manyanyaso, tafadhali nakuomba umpe heshima kuu Raisi wetu. Usiandike Raisi JK.
Tafadhali anza sentensi kwa kuandika: Raisi Dr Dr Dr Dr JK. ​Tunza heshima ya mkuu wa Tanzania.
 
Kamati ya Bunge ilioundwa kuchunguza tuhuma za rushwa katika sekta ya nishati na madini inayo mkabili bwana Jairo imesha wasilishwa mezani kwa spika.sasa hivi bado wanaendelea na maswali na majibu.mia
 
Mkuu Manyanyaso, tafadhali nakuomba umpe heshima kuu Raisi wetu. Usiandike Raisi JK.
Tafadhali anza sentensi kwa kuandika: Raisi Dr Dr Dr Dr JK. ?Tunza heshima ya mkuu wa Tanzania.

Hizo PhD za kishemeji mimi sizitambui, ninatambua PhD kama yangu niliyikalia darasani na kufanyia utafiti. Hizo PhD za kupeana ili usipotezewe ugali mimi zizitambui hata kidogo. Mnadhalilisha Dr. Magufuli.
 
Bunge baada ya maswali na majibu linaendelea na mswaad wa katiba.mwanasheria mkuu anajibu hoja.
 
Ndugu zangu tusiangaike na issues ndogo kama za Jairo na Luhanjo jambo muhimu wakati huu ni mchakato wa kuandika katiba mpya. Hii mambo ya Jairo ni ndogo sana,kwanza Pinda na Jk wangekua makini wangekwisha maliza hii maneno ya Jairo siku nyingi. Nchi yetu ni ya ajabu sana,bunge linashupalia issue ndogo kama ya Jairo wanashindwa kushupalia jambo nyeti kama mchakato wa katiba mpya ambao kama tunapata katiba nzuri kesi za akina Jairo tutazipunguza sana.
acha hizo tuache kushughulikia wapuuz kama hao eti kisa katiba .vyote hivi vinaenda kwa wakati mmoja uzembe wanaoufanya una madhara makubwa sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom