JK kumpooza Masha na cheo gani?

...... Nyepesi nyepesi upo uwezekano wa JK kumrudisha Lowassa kama PM kumalizia ngwe ya mwisho.....
 
Kama rais atawateua watu waliokataliwa na wananchi (yaani walishindwa kwa kura) hiyo itakuwa ni dhalau kubwa kwa Watanzania na hata wana CCM wenyewe. Kama anajua alifanyalo hawezi kuwateua ktk viti 10 wale walioshindwa.

Wewe nawe kwani Mkwere ana akili ya kufikiria hayo? Ya kuwadharau wa-TZ unayajua wewe tu ni mangapi kayafanya ya kuwadhalilisha wa-TZ? Hata hivyo mbona viti 10 ni vichache na waliobwagwa ni wengi? Hapo mweke Makamba, Marmo, Batlida, Masha, Dialo, Mramba, Abdul-Aziz, Kamala, Chegeni, Ridhi 1, Salum Khamis Mbuzi, Luka Siame, Dan Nsanzugwanko, Hawa Ng'humbi, Ben Mpesya, Monica, Erick, Fredrick n.k Mwaka huu tutastajaab ya Musa!!
 
Kuna kila dalili Masha, Dr Kamala, Marmo, Batilda wakarudishwa kwa kupitia viti 10 vya kuteuliwa na RAIS

hiki ndio kinachoninyima usingizi, yaani nikikumbuka vile viti kumi ndo hasira inaongezeka, ndio nazidi kuona umuhimu wa kulinda kura za dk slaa, and this is exactly what jk will kama atarudi ikulu, soo sad!
 
Kuna kila dalili Masha, Dr Kamala, Marmo, Batilda wakarudishwa kwa kupitia viti 10 vya kuteuliwa na RAIS

Kuna habari nimeipata kutoka kwa mzee mmoja CCM damu damu na anajua haya mambo vizuri, anasema sheria hairuhusu kumweka mtu aliyeshindwa kwenye jimbo viti Maalumu, halafu Batilda hawezi kuchaguliwa tena coz ameshakaa bungeni miaka kumi na ndo maana alirudi jimboni. Labda apate RC au UBALOZI.
 
Kuna kila dalili Masha, Dr Kamala, Marmo, Batilda wakarudishwa kwa kupitia viti 10 vya kuteuliwa na RAIS

Ni kweli Rais anahiari ya kuchagua wasaidizi wake kikatiba. Lakini ntamshangaa sana kama atawaleta watu ambao wananchi wamewakataa ili wawe viongozi wao. Pengine hawa jamaa ndio walikuwa top perfomers wake lakini iweje wananchi wameshindwa kuliona hilo? Vinginevyo ndio yale yale tunayoyasema siku zote kwamba sikio la kufa huwa halisikii dawa. Move kama hiyo itaongeza maumivu ya watu juu ya CCM hata kwa siku za baadae.
 
Katika hali ya kuonyesha kukubali matokeo na kujipa moyo mh mstaafu amedai tena kwa nyodo kuwa hata kama wana mwanza wamemtosa lakini mkubwa atamkumbuka tu kwakuwa hawakukutana barabarani.

Wanabadiliko Tumpe Pole Huyu Jamaa kuz Anapumulia mashine.

Hongereni sana wana jamii forum kwa uzalendo wa nchi yetu.
Hili swala ni kweli kabisa ni rahisi sana kwa hawa jamaa kurudi ila pia nawapa habari nyingine katika wale wa viti maalumu nyepesi kutoka kwa wazee wa kitalu A zinasema kwamba tayari Vicky Kamata yupo ndani sasa sijui huyu mdada ni proffessional gani aliyo nayo ya kuingia mjengoni kwa viti maalumu??....UNDUGULIZATION NA URAFIKI WA KIWETE NDO UNATUPELEKA PABAYA.
 
Kama kweli atafanya ivyo,mtaamini yangu niliposema anaenda kulipa fadhira. Itakuwa dharau kwa Pinda,watanzania wote na riport ya Kamati ya Mwakyembe kwake itakuwa ameidharau. Hawezi kumrudisha 'MRICHMOND' yule.
 
Kuna habari nimeipata kutoka kwa mzee mmoja CCM damu damu na anajua haya mambo vizuri, anasema sheria hairuhusu kumweka mtu aliyeshindwa kwenye jimbo viti Maalumu, halafu Batilda hawezi kuchaguliwa tena coz ameshakaa bungeni miaka kumi na ndo maana alirudi jimboni. Labda apate RC au UBALOZI.

Hakuna kikwazo cha kisheria kuwateua hao labda mtu awafungulie kesi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kukiuka taratibu za uchaguzi na hivyo Mahakama iamuru kuwa hawana sifa ya kuwa viongozi. Vinginevyo kama Kikwete atashinda anaweza kuwateua. Dawa si kuwaita kuwa ni wabunge wa kuteuliwa bali "wabunge wa huruma ya raisi".
 
Wewe nawe kwani Mkwere ana akili ya kufikiria hayo? Ya kuwadharau wa-TZ unayajua wewe tu ni mangapi kayafanya ya kuwadhalilisha wa-TZ? Hata hivyo mbona viti 10 ni vichache na waliobwagwa ni wengi? Hapo mweke Makamba, Marmo, Batlida, Masha, Dialo, Mramba, Abdul-Aziz, Kamala, Chegeni, Ridhi 1, Salum Khamis Mbuzi, Luka Siame, Dan Nsanzugwanko, Hawa Ng'humbi, Ben Mpesya, Monica, Erick, Fredrick n.k Mwaka huu tutastajaab ya Musa!!
Akiwateua hao kwa nafasi yoyote ile atakuwa kawadharau watanzania sana.
 
Kuna habari nimeipata kutoka kwa mzee mmoja CCM damu damu na anajua haya mambo vizuri, anasema sheria hairuhusu kumweka mtu aliyeshindwa kwenye jimbo viti Maalumu, halafu Batilda hawezi kuchaguliwa tena coz ameshakaa bungeni miaka kumi na ndo maana alirudi jimboni. Labda apate RC au UBALOZI.

Ukweli nusu, na sehemu kidogo si sahihi.

Viti Maalumu vya upendeleo kupitia akina Mama, Vijana, Wafanyakazi, Vyuo na kadhalika majina yao yamekwishapelekwa kwenye Tume Ya Uchaguzi, mwisho ilikuwa Sept 30. Kwa hiyo, kwa wale ambao majina yao hayamo katika hizo orodha kupitia vyama vyao, basi ki-sheria hawawezi kuvipata hivyo Viti Maalum. (Huku ndiyo yako makorokoro mengi, wake na vimada wa vigogo, watoto wa vigogo, makuwadi, n.k).

Tume ya Uchaguzi inagawa nafasi hizo kufuata uwiano wa wingi wa Wabunge wa kuchaguliwa majimboni. Tume haichagui ni nani apewe na nani asipewe. Kila Chama kiliweka orodha yake kwa mpangilio wa yupi apewe mwanzo, na kuendelea hadi wa mwisho. Kwa maana hiyo ni kuwa Chama kinavyozidi kupata wabunge wengi wa majimbo, basi pia kinazidi kupata wabunge wengi wa viti maalumu, na kinyume chake pia.

Nafasi 10 za uteuzi wa Rais, hizi hazina sheria yo yote isipokuwa utashi wa Rais mwenyewe. Rais anaweza kumpa ye yote apendaye katika hizi nafasi 10. Ila katiba haimpi Rais nafasi ya kumteua mtu kuwa mbunge kwa nafasi 10, na pia kumteua huyo mtu kuwa Waziri au Naibu Waziri. Mawaziri au manaibu wanatokana na wabunge wa majimbo au viti maalumu.

Ugumu kwa Kikwete si kuwa ni nani apewe katika hizo nafasi 10, ila ugumu ni kwa nini fulani apewe na si fulani. Kikwete ana watu lukuki ambao wanasarandia hizo nafasi 10, pamoja na 25 za Ukuu wa Mikoa, na si ajabu kuna ambao wame-ahidiwa tayari baada ya kura za maoni. Kikwete atataka kutumia hizi nafasi 10 (na Ukuu wa Mikoa) si kufurahisha marafiki tu, bali kujaribu kuziba ufa na kutengeneza mustakabari ambao utampa nafasi ya kupumua akiachia madaraka 2015.

Ikumbukwe kuwa Uchaguzi Mkuu wa CCM ni 2012 ambao utatoa picha ni nani anajipanga vipi kwa 2015, na siyo suala la nini au nani alifanya 2005 au 2010.

Masha amekuwa kwenye siasa za ki-Taifa kwa muda wa kama miaka 5 tu, toka kupanda hadi kuporomoka. Hana mizizi iliyokomaa ya ki-siasa ndani ya CCM, Mwanza au mahali popote. Kwa kiasi fulani, utaona kuwa huo si mtaji mzuri kwa Kikwete.

Ikiwa Kikwete ameweza 'kumtosa' Karume na kumkumbatia hasimu wake Billal, pia kawatosa Malecela, Chegeni na Msekela, basi upepo kwa Masha hausharii mema kulinganisha na watu kama akina Marmo, Makamba, Mongela, Karamagi, Kamala, Batilda au hata Mbega, Mwakipesile au Abdulaziz.

Lakini kila mtu na nyota yake, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
 
Tusiende mbali Mwakipesile alipigwa chini kyela na Mwakyembe then JK akamteua kuwa RC-MBEYA.
NDO chanzo cha wanakyela kumchukia JK.
Sasa kwa mfano huo nadhani mtajua atakachofanya na akina Masha,matilda,maramba etc
 
Hatimae aliekuwa mbunge machachari aliemwagwa huko nyamagana mwanza laurence masha aka lau amewekewa matumaini ya kuula upya tena kwa ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi baada ya kuahidiwa kupewa mojawapo ya nafasi zifuatazo ili ajilie maisha na bata kama wasemavyo watanzania..akizungumza kwa kujiamini chanzo hichocha habari kimeelza kuwa jamaa ameahidiwa kati ya vifuatavyo na kazi yake ni kupendekeza anapotaka
1.ubunge wakuteuliwa ktk nafasiza raisi
2.ukuu wa mkoa/wilaya
3.uanasheria mkuu waserikali
4.kuwakilisha nchi kamabalozi wa nchi nje ya tanzania

aidha mbali na hilo ameahidiwa pia kupewa tenda ya kuchapa vitambulisho vya utaifa na dili hilo limeelezwa litampatia mpungawa kufa mtu.
 
Mbona huo utabiri wako hauna mantiki? ungesema kimoja halafu kikijatokea basi tungejua kweli una taarifa za uhakika
 
Back
Top Bottom