JK kukutana na Wazee wa Mkoa wa Dar J'nne kuwaeleza serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa

Hakuna udhaifu mkubwa kwa kiongozi kama kuruhusu wapiga kelele kukuyumbisha, Kosa kubwa la JK ni kumteua PINDA ambaye hana misimamo ni weak sana yaani anaboa ningekuwa JK ningemfukuza na kumuomba astaaf hadi ubunge.
Anaboa sana PINDA.
Pinda ndio chanzo cha matatizo serikalini. Hivi hakuna wanajeshi bungeni wapewe hii nafasi!

Kikwete alimteua Picha kwa sababu hiyo, vinginevyo asingekubali Lowasi Jabali ajiuzuru. Sababu hiyo ndiyo inayomfanya Pinda abaki kwa vile yuko tayari kwa ile kitu ya utwa na utwana.
 
kama kweli mkuu wa kaya amedhamiria kukutana na wazee wa ccm dar basi bunge linahaja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye
 
Kikwete alimteua Picha kwa sababu hiyo, vinginevyo asingekubali Lowasi Jabali ajiuzuru. Sababu hiyo ndiyo inayomfanya Pinda abaki kwa vile yuko tayari kwa ile kitu ya utwa na utwana.
Pinda is the weakest Tanzanian Prime Minister ever.
 
Baada ya Kikwete (kupitia Pinda) kutangaza hapo kesho kwamba hakuna waziri atakayejiuzulu kutokana na sakata linaloendelea, Mkuu huyo wa Kaya atakutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Sakaam siku ya J'nne Ukumbi wa Diamond kuwashitaki Wabunge wachache wa CCM wasaliti walioshirikiana na wale wa upinzani kutaka kuiyumbisha serikali yake.
Mada kuu itakuwa ni kwamba serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa.

Mwenyekiti wa Wazee ambaye anabeba tuhuma lukuki za ufisadi na ambaye hakuna chombo cha dola kinachodiriki kumgusa -- Iddi Simba ndiye atakayempokea rasmi rasmi JK ukumbini pale.

Nataka kutapika!!!!!
Kuna haja sasa ya kuwatandika bakora hao wazee watakaokuwa wanakutana na JK na kuongea pumba kila kukicha. Wakitandikwa mara moja next time wakiitwa kuelezwa ujinga hawatatokea.
 
hivi wazee wa dar wote ni ccm nikichungulia kwenye tv nakuta rangi ya kijani hasa pale anapokuwa anaongea na wazee. Natamani Nikute wazee wote wamepiga pamba za khaki kama za pipooooz pawaaaa na ishara ya vidole viwili juu kisha nione kama angeongea huyu prefect wetu.
 
Baada ya Kikwete (kupitia Pinda) kutangaza hapo kesho kwamba hakuna waziri atakayejiuzulu kutokana na sakata linaloendelea, Mkuu huyo wa Kaya atakutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Sakaam siku ya J'nne Ukumbi wa Diamond kuwashitaki Wabunge wachache wa CCM wasaliti walioshirikiana na wale wa upinzani kutaka kuiyumbisha serikali yake.
Mada kuu itakuwa ni kwamba serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa.

Mwenyekiti wa Wazee ambaye anabeba tuhuma lukuki za ufisadi na ambaye hakuna chombo cha dola kinachodiriki kumgusa -- Iddi Simba ndiye atakayempokea rasmi rasmi JK ukumbini pale.

Nataka kutapika!!!!!

Sinto shangaa akifanya hivyo.Hao wazee wake watamponza,JKambarage aliwatumia wazee mara chache sana tena kwenye ishu ambazo nchi nzima tulichanganyikiwa nazo.Sasa hapa kuna lipi la kushangaza kama sio kuvunja baraza la mawaziri? This is absurd!!!!!!!!!
 
baada ya kikwete (kupitia pinda) kutangaza hapo kesho kwamba hakuna waziri atakayejiuzulu kutokana na sakata linaloendelea, mkuu huyo wa kaya atakutana na wazee wa mkoa wa dar es sakaam siku ya j'nne ukumbi wa diamond kuwashitaki wabunge wachache wa ccm wasaliti walioshirikiana na wale wa upinzani kutaka kuiyumbisha serikali yake.
Mada kuu itakuwa ni kwamba serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa.

Mwenyekiti wa wazee ambaye anabeba tuhuma lukuki za ufisadi na ambaye hakuna chombo cha dola kinachodiriki kumgusa -- iddi simba ndiye atakayempokea rasmi rasmi jk ukumbini pale.

Nataka kutapika!!!!!
tatizo kubwa la huyu msanii ni mtu anaye endeshwa na hisia kali za udini. Hicho anachokiita hayuko tayari kushinikizwa si kweli, ukweli nikwamba tangu vita vya ufisadi vianze watu wenye majina makwabwa waliowajibika na kufikishwa mahakani ni wakristo tu. Utasema mbona ibrahim msabaha na karamage waliwajibika! Hao waliwajibika kwasababu aliyekuwa anatafutwa ni el, ili kufunika kombe mwanaharamu apite ikabidi nao wakumbwe na hiyo songombingo. Hapa kuna maazimioa ya abuja inabidi ayatekeleze, na ninyi mnamwambia watu wake ambao ni washirika wakuu ktk kutekeleza azimio hilo, halafu awatimue? Subutu!

Kwenye songo mbingo iliyoikumba serikali yake huko nyuma wafatao waliwajibishwa na kufikishwa mahakani: Basili mramba, grey mgonja na daniel yona (hakuwa kwenye serikali by then). Waliowajibika tu bila kufikishwa mahakani: Andrew chenge, msabaha na karamage.

Katika hili kkuna waziri wa fedha (mwanaabuja), waziri wa afya, waziri wa uchukuzi; atafanya mbinu na hila zote na kutumia wazee wa misikitini maarufu kama wazee wa dar kujenga zengwa na giriba za kuwalinda watu wake kwa misingi ya abuja. Angalia hata mahakama zinavyoendeshwa siku hizi, naona ni kama mahaka za kadhi maana hazitabiriki kwa facts za kisheria. Zinaendeshwa kwa misingi ya muungwana vs kafiri!!!!!!!!!!

Twende mbele turudi nyuma. Hakuna tukio baya kama kulipuka kwa mabomu ya mbagala na gongolamboto. Nani aliwajibishwa? Tume iliundwa, ripoti iko wapi? Husein mwinyi hawezi kuwajibishwa kwasababu baba yake ndiye mwasisi wa azimio la abuja. Ni yale yale ya muungwana vs kafiri, ni sharti kafiri aumie
 
Kikwete alimteua Picha kwa sababu hiyo, vinginevyo asingekubali Lowasi Jabali ajiuzuru. Sababu hiyo ndiyo inayomfanya Pinda abaki kwa vile yuko tayari kwa ile kitu ya utwa na utwana.

Hahahahahaaaaaaaa, unanikumbusha hadithi ya zamani saana nilisimuliwa na babu yangu: Zamani za kale nzige walimlilia muumba wao awaletee kiongozi wa kuwaongoza na kuwalinda. Muumba wao akamleta korongo . Akawa anawalinda wasidhuriwe na viumbe wengine lakini yeye mwenyewe kazi yake ikawa kuwadonoa mmoja mmoja mpaka wakastuka kuwa mbona wanapungua. Nzige wakamlilia muumba wao kuwa "tunakwisha muumba wetu, tuokoe na huyu korongo atatumaliza, anatudonoa badala ya kutulinda, mwondoe utuletee mwingine." Muumba wao akasikia kilio chao akamwondoa korongo akaleta gogo akaliweka katikati yao liwalinde. Kazi ya nzige ikawa kuruka ruka juu ya gogo, kulisukuma mbele na nyuma, kulizomea nk. lakini lenyewe likawa kimya. Nzige wakalia tena kwa muumba wao" oh, kiongozi gani huyu, tunamsukumasukuma, tunamzomea, tunamtia vidole machoni yeye kakaa kimya tuuu, hatumtaki." Muumba wao alibaki akitafakari kuwa viumbe hawa niwaletee nani waridhike? Mkali hawamtaki, mpole hawamtaki? Nimlete nani wakati kila mmoja ana madhaifu yake? Kazi kwako wewe , wataka JABALI au MTWANA?
 
Kama hii ni kweli inabidi tuwajue hawa wazee wa Dar wenye njaa na wezi wa nchi hii tangu uhuru watakaoaribu kupiga makofu au kuhalisha wizi unaoendelea.

Huu ni upuuzi mkubwa na hatutaendelea kwa kuwasikiliza JK pamoja na hawa wazee.
 
Hakuna udhaifu mkubwa kwa kiongozi kama kuruhusu wapiga kelele kukuyumbisha, Kosa kubwa la JK ni kumteua PINDA ambaye hana misimamo ni weak sana yaani anaboa ningekuwa JK ningemfukuza na kumuomba astaaf hadi ubunge. Anaboa sana PINDA. Pinda ndio chanzo cha matatizo serikalini. Hivi hakuna wanajeshi bungeni wapewe hii nafasi!
sijakuelewa mkuu naomba ufafanuzi wapiga kelele ni akina nani?
 
:rolleyez::rolleyez: SIJAWAHI KUWA NA IMANI NAE....naona kuwa mimi ningeweza zaid yake.....Huyu ni vasco da gama ........hahahah niliwahi kusoma mahali siku alizosafiri nje ya nchi ni nyingi kuliko alizoisha ndani ya nchi....si tumpe cheo cha waziri wa matembezi na kupunga upepo nchi za nje........
SIJUI KAMA NI GOIGOI AMA....
 
Kama ni kweli bunge limpigie kura yeye hana uwezo wa kuiongoza nchi yetu

Too late. Keshamaliza kipindi kimoja na sasa yupo nusu ya kipindi cha pili, na amejitahidi to his level best. Too late my friend. Mwache amalize apewe mwingine na kelele zitakuwa hizohizo. Kwani hata JK Nyerere aliyeleta uhuru si alilaumiwa tuu? Binadamu hawaridhiki bana. Kwani Libya walikuwa wanatunzwaje na serikali lakini bado wakamuua Gaddafi? Nani mzuri atapendwa Tz? Wewe?
 
Hakuna udhaifu mkubwa kwa kiongozi kama kuruhusu wapiga kelele kukuyumbisha, Kosa kubwa la JK ni kumteua PINDA ambaye hana misimamo ni weak sana yaani anaboa ningekuwa JK ningemfukuza na kumuomba astaaf hadi ubunge.
Anaboa sana PINDA.
Pinda ndio chanzo cha matatizo serikalini. Hivi hakuna wanajeshi bungeni wapewe hii nafasi!
Pinda aliwahi kumteua nani! Jairo? Kauli ya Pinda juu ya Jairo ilikuwaje? Jk alipokuja akafanyaje? Acha kutulisha pumba wakati jibu tunalo! Anayesafiri nje ya nchi mpaka kupachikwa Vasco Dagama kwa Kisingizio cha tusife njaa ni Pinda au jk! Ameambulia nini huko?
 
Back
Top Bottom